Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, October 16, 2012

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KWA KUTUMIA MASHINE NA UZITO


Mara nyingi watu walio wengi wamekuwa na ufahamu mdogo wa kufanya mazoezi kwa kutumia mashine hususan kinadada.
Mazoezi ya kutumia mashine ni muhimu sana, hii ikiwa katika kuutanganisha mwili wako kwa kuondoa yale mafuta yaliyojificha  kwenye mwili wako.Kwa kufanya mazoezi ukiwa unatumia mashine hukusaidia kujenga misuli ili kufidia ile sehemu uliyoondoa mafuta kwa kufanya mazoezi ya aerobics(muscle tune).
Hii husaidia kuufaya mwili wako kuwa umekaza badala ya kutepeta na kukuweka nadhifu kwenye muonekano pindi uvaapo nguo zako huwa unapendeza zaidi.







  
Kama picha inavyoonyesha namna ya kutumia mashine aina ya cross traing
                        mdau wa mzoezi Jaqline anavyoanza zoezi hilo katika gym ya UDSM



                                Hapa inaonyesha jinsi ya kumalizia zoezi hilo la cross training
                             









Friday, September 28, 2012

AINA YA VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA ILI KUPUNGUZA TUMBO KWA KUFANYA ZOEZI

Mara nyigi binadamu huwezi pungua mwili bila ya kufanya mazoezi ikiwa imeambatana na kupunguza mlo unaokula.

Aina ya vyakula ambavyo  unatakiwa kula ni kujaribu kupata chakula ambacho hakina mafuta mengi,pia kupunguza ulaji wa sukari nyingi na hata chimvi ujaribu kupunguza katika maisha yako ya kila siku, hali kadhalika  kupunguza vyakula vya wanga.
Jambo lingine ni kufanya mazoezi ya tumbo kila siku uamkapo asubuhi na jioni ili uondoe manyama uzembe.


















Mazoezi ya tumbo namna ya unvyoanza ukiwa umekaa
kitako na kukunja miguuyako kama  picha inavyoonyesha


















Hapa ni namna ya kumalizia zoezi la tumbo kwa
kunyoosha na kukunja tena kama mwazo mara 50






Monday, September 17, 2012

AINA YA MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO (KITAMBI)

Mara nyingi sana katika maisha watu wengi hupata tatizo la kuwa na tumbo kubwa na baadae humletea madhara. Ili kuepuka tatizo hili ni kuamua kufanya mazoezi  kupunguza  ya mafuta katika chakula na kufanya mazoezi ya tumbo hii ndio njia pekee hakuna njia mbadala.

                                                           
                                        Zoezi hili ni kufanya kwa kutumia mashine(abs board)





Hapo ni zoezi ambalo utumia mpira maalum. uanzapo;

                                            Zoezi  la mpira maalum umaliziapo kwa kunyaua juu.




                                         Hapa ni mazoezi ya tumbo kwa kutumia mpira maalum




                                          Kwa kutumia bench la zoezi la tumbo unavyoanza

                                          Namna unvyomalizia  zoezi kwa kunyanyuka.




                                          Zoezi la tumbo kwa kutumia hypic chair unavyoanza.

                                         Zoezi la tumbo unavyomalizia kwa kutumia hypic chair





                                         Zoezi la aina nyingine kwa kutumia mpira wa zoezi hilo

Monday, September 10, 2012

MAZOEZI HAYANA UMRI WA KUYAFANYA HATA WAZEE WANAHITAJI MAZOEZI NI MUHIMU

Watu wengi hudhani mazoezi ni kwa ajili ya mtu au watu wenye umri fulani tu , hiyo hapana pia ni fikra potofu kwa wale ambao hawajui au hawajawahi kufanya mazoezi kwenye maisha yao yote.

Mazoezi ni muhimu sana haswa pale umri unapoenda kwa sababu utakuwa hufanyi tena kazi au kuwa na pilika pilika kama ulipokuwa kijana.

Mazoezi madogodogo husaidia watu wenye umri mkubwa kujisikia kijana kila siku aamkapo na pia kutosumbuliwa na mardhi ya mara kwa mara.

Pia mazoezi husaidia watu wenye umri mkubwa kuwa na nguvu hata kumlinda kuwa na kumbukumbu zake bila kusahau mambo.

 Mzee Alhaj Juma Mtale akiwa katika mazoezi 
                                           ya kunyoosha mgongo ni mzee mwenye umri zaidi ya                       
                                            miaka70 pia hujisiki poa akifanya mazoezi yake.


                                                                                                                                                                        
















Mzee Alhaj Juma Mtale akiwa kwenye
aina nyingine ya mashine cross training










y

Monday, September 3, 2012

MAZOEZI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUTUMIA SPIN BIKE

Mazoezi ya spin bike yamekuwa na msisimko mkubwa sana hapa Dar es salaam, imekuwa hivyo kutokana na kuwa na wapenzi wengi wa mazoezi hayoambayo yanasaidia sana katika kupunguza uzito kwa muda mfupi na kukuweka kuwa na pumzi na kuwa na afya bora.
Mazoezi hayo yametokea kuwa na umaarufu lakini kukiwa na waalimu wachache sana ambao wanafundisha zoezi hilo.
Hivyo hima waalimu wajitokeze katika kujifunza namna yakuendesha zoezi hilo ambalo linaongozwa kwa kutumia muziki maalum kwa kweli ni burudani tosha.

















Katika picha hapo juu ni wadau wa mazoezi ya spin bike.
















Hapa ni wadau wa mazoezi ya spin bike waliobobea katika zoezi

















Amakweli zoezi la spin bike limetokea kupendwa sana hapa Bongo

Saturday, August 18, 2012

JINSI YA KUCHUNGA KUONGEZEKA UZITO WA MWILI ULOKITHIRI BILA YA KUFANYA MAZOEZI.

Ni kawaida yetu kufanya mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ulokithiri,hii ikiwa ni lengo la muda mrefu mpaka kufikia uzito ambao unakubalika.
Haya matatizo ya kuongezeka uzito huwa yanajitokeza pindi unapokula bila ya mpangilio wowote ule,ikiwa ni pamoja ya kula bila mpangilio na bila kujua chakula cha aina gani na wakati gani.
Leo niwakumbushe  kwamba unaweza kufanya mazoezi madogodogo kama vile kujihusisha na shughuli ndogondogo hapo nyumbani kwako,ikiwa ni kufanya zoezi la kufanya usafi kama kufyeka bustni na kupalilia maua au kukata majani kwa kutumia mashine ya kukatia huku ukitembea. Haya ni mazoezi tosha kwa wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda gym.Usisahau kupunguza mlo na kupata mlo mwepesi wakati wa mlo wa usiku.

Wednesday, August 8, 2012

AINA YA MAZOEZI YA SURCKET TRAINING YANAVYOTAKIWA KUFANYA



Katika picha zinzonyesha namna ya kufanya zoezi la surcket training huwa unafanya mazoezi aina mbalimbali kwa muda wa takribani dakika 40 . Ikiwa kila zoezi unachukua dakika  nne na kuhamia zoezi lingine na kuanza tena.Zoezi hili unaweza kukata kalori 860.














Hapa juu ni mazoezi ya kukimbia kwenye mashine ya
treadmill na total body power mshine



















Hapa ni zoezi la step aerobics ambalo huwa
linakwenda sambamba na mazoezi mengine




















Katika picha hapo juu ni zoezi tofauti, juu kabisa
ni zoezi linalosaidia kukukuza sehemu ya misuli ya nyuma
ya mikono(tricept muscles).


















Hapa ni zoezi la kukuza au kuondoa manyama uzembe
upande wa mgongo na upande(obliq muscle)
Zoezi hili hutegemea uzito unaoweka yaani uzito mdogo
kwa ajili ya kuondoa mafuta.
Na uzito mkubwa kwa ajili ya kujenga sehemu ya mgongo
(lat pull down)




Sunday, July 22, 2012

MAZOEZI YA SARKET YANAVYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

Mazoezi ya surket training  ni mazoezi mchanganyiko ambayo hufanywa kwa kubadili zoezi kila baada ya dakika tano na kuhamia zoezi lingine, bila ya kupumzika kama vile ikionyesha kwenye picha hapo chini.
Mazoezi haya yanasaidia kupunguza uzito wako kwa kipindi kifupi ikiwa utazingatia mwalimu anavyoongoza ikiwa ni pamoja na kuzingatia chakula bora (diety)















Hapa ni  wadau wa mazoezi wakifanya mazoezi kwa
bidii kuendana na muda waliopangiwa.
















Bila kusahau umuhimu wa mazoezi ya tumbo ikiwa na
umuhimu wake wa kipekee.

Wednesday, July 4, 2012

MAZOEZI NA LISHE BORA(DIETY)

Mara nyingi mtu ukiwa unafanya mazoezi huwa na lengo lako ,ama uwe una tatizo la uzito au unafanya kwa afya yako ili uwe na afya bora  ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara.

Nikizungumzia mazoezi na lishe nina maana wakati unapofanya mazoezi yoyote yale hutokea kupata hamu ya kula baada ya mazoezi.

Sasa uachotakiwa wewe ni kujaribu kupunguza kiasi cha mlo unaokula hii itakusaidia kupunguza uzito ambao ulokithiri. Kwa kawaida ya binaadam anatakiwa kupata kalori 1500 kwa siku kutoka katika mlo wake wa siku, ndio maana unatakiwa kufanya mazoezi ili kile chakula unachokula kitumike vyema kwa muda muafaka.

Tafadhali kama una swali lolote au maoni  uliza kupitia email yangu omaryswai@gmail.com

Wednesday, June 20, 2012

TOFAUTI YA MAZOEZI YA AQUA AEROBICS NA KUOGELEA






Watu wengi wanashindwa kutofautisha  kati ya Aqua Aerobics na  kuogelea.
Kuna tofauti kubwa kati ya haya mazoezi mawili hata kwa kuangalia picha hapo,
kwa vile zoezi hilo hufanyika ukiwa kwenye maji.
Zoezi la aqua  unafanya kama vile zoezi la aerobics uwapo darasa la kawaida yaani
bila maji,lakini zoezi hili hukulinda kutokuumia magoti kwa urahisi.na pia mtu yeyote
anafanya hata kama hajui kuogelea,na pia umalizapo zoezi hilo ambalo linachukua
takriban ya dakika 40 tu utasikia misuli  na viungo vyako vya mwili vimepata
zoezi tosha

 Mazoezi ya kuogelea inabidi ujue namna ya kuelea kwenye maji na hii pia inahitaji
mafunzo maalum ili umudu kuogelea.Pia hilo ni zoezi la mwili ambalo linasaidia pia.






















Katika picha ya juu inaonyesha mazoezi ya Aqua aerobics darasa maalum
 katika bwawa la chuo kikuu (UDSM) N mwalimu Swai.



















Mazoezi ya kuogelea kwa kuelea juu ya maji.




Zoezi la kuogelea kama picha inavyoonyesha  hapo juu chuo kikuu (UDSM)

Friday, June 1, 2012

MAOEZI YA AQUA AEROBICS YAANZA CHUO KIKUU MLIMANI

 Mazoezi ya Aqua yakiwa yamefana sana katika bwawa la kuogelea la Chuo Kikuu ch Mlimani (UDSM).
Mazoezi haya hufanyika kila siku ya Jumatano katika bwawa hilo chini ya Mwalimu O.Swai.
 Zoezi hilo ni kwa mtu yeyote hata kama hajui kuogelea humudu kulifanya bila ya matatizo.Hivyo wadau wengine kutoka popote pale mnakaribishwa.


















 Mwalimu wa mazoezi ya Aerobics O.Swai akiwa na
wadau wa Aerobics katika bwawa la UDSM.
(aliyevaa nguo nyekundu akifundisha aqua aerobics)















Wadau wa mazoezi wakifuatilia kwa mkini zoezi hilo.
















Baada ya zoezi la kwenye maji sasa ni nje ya maji.















Wadau wakimalizia  mazoezi ya kunyoosha viungo
baada  ya  zoezi husika.

Wednesday, May 23, 2012

JINSI UNAVYOTAKIWA KUFANYA MAZOEZI NA MUDA WAKE

Kuna baaadhi ya watu ambao wanafanya mazoezi kwa kupita kiasi,kwa maana hiyo hufikiria kufanya mazoezi kwa muda unaozidi saa moja ndio utakuwa unapunguza uzito na wengine hudiriki kufanya mara saba kwa wiki tena sio chini ya saa mbili.

Hii  siyo sahihi kwa sababu mwili wa binadamu unahitaji muda wa kupumzika na kuupa nafasi ya kujenga misuli ya mwili kwa mpangilio ulosahihi kutokana na maumbile yake.

Muda maalum unaotakiwa kufanya mazoezi usizidi saa moja na ikwa imepungua ni dakika 30 kwa siku mara tano kwa wiki,hii inasaidia kupunguza kaloriz ambazo hazihitajiki  mwilini.Kwani binaadamu anatakiwa awe anapata kaloriz 1500 kwa siku kutokana na chakula anachokula hii humsaidi awe na afya njema na kutokuwa namaradhi yanayosababishwa na mafuta  kwa wingi mwilini.

Madhara wanayopata wale wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu bila ya kupumzika huwa yanawafanya kuonekana wamechoka muda wote huonekana kuzeeka hararaka haswa sehemu ya uso wake.
Epuka kuzidisha mazoezi na pata muda wa kuupumzisha mwili ili kujenga seli mpya za mwili.
















Katika picha inaonyesha baadhi ya mazoezi ya 
viungo  namna unavyoanza na kumalizia.
Je wewe waweza haya mazoezi.JARIBU LEO;

Monday, May 14, 2012

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUWA NAYO KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU

Mambo matatu  unayopaswa uyazingatie katika maisha yako ya kila siku ili kuepukana na uzito  uliokithiri.

1. USIWE UNALALA  WAKATI UNAWEZA KUKAA KITAKO

2.USIKAE WAKATI UNAWEZA KUSIMAMA.


3.USISIMAME SEHEMU MOJA WAKATI UNAWEZA KUSOGEA

Hii nikiwa na maana unapokuwa kazini uwe unazingatia hayo mambo matatu,utakuwa umeokoa maisha yako katika ogezeko la uzito wa mwili usiohitajika na kuwa na afya njema wakati wote wa maisha yako.
Mara nyigi ukiwa ofisini jitahidi  kufanya mambo mengi bila ya kutegemea msaada kwa msaidizi, kama vile kunyanyuka na kwenda kuchukua faili kwenye shelfu, kunyanyua kitu au kuzungumza na simu kwa muda mrefu umekaa kwenye kwenye kiti jitahidi uwe  unasimama na kutembea huku unazungumza..
Pia wakati wa kwenda kupata chakula cha mchana jitahidi uende mwendo kidogo ili uupe mwili mazoezi ya kutembea , hii itakusaidia katika usagaji wa chakula kwa wepesi zaidi na kujisikia mchangamfu wakati wote wa maisha yako.


Wednesday, May 9, 2012

SULEIMAN KIULA MWANA MAZOEZI WA WIKI















Katika picha mwisho kulia mwana mazoezi aliyevaa tisheti
nyekundu na bukta ya rangi nyeupe yenye mistari pembeni
ndiye Mwana Mazoezi wa wiki anaitwa Suleiman Kiula
ambaye anafanya kazi SUMAJKT  na Meneja wa fedha.


















 Suleiman akionekana na wanamazoezi wenzake
katika darasa la Aerobics yuko mwisho kulia.

Wednesday, April 25, 2012

WADAU WA MAZOEZI WAPAGAWA NA MAZOEZI YA TAE BO GYM YA UDSM

                                              
Wadau wa mazoezi yaviungo wakiwa katika mazoezi ya Tae Bo mazoezi ambayo yametokea kupendwa sana na yenye matokeo ya haraka katika mwili. Mazoezi  ya Tae Bo hukufanya uwe na nguvu na pumzi ya kutosha hata katika kukabiliana tatizo la aina yoyote ile.                                           






WADAU WA MAZOEZI WAKIWA KWENYE
DARASA LA TAE BO LIKIONGOZWA NA
MWALIMU OMAR SWAI  UDSM











































Friday, April 20, 2012

FAIDA YA KUFANYA MAZOEZI YA AEROBICS


Faida ambazo unapata ukifanya mazoeziya Aerobics mara tatu hadi tano kwawiki ni:
-Kuonngeza uwezo wa kupumua kwa ufasaha na uhakika.
-Kuuweka moyo wako madhubuti na uhakika katika msukumo wa damu mwilini.
-Kupunguza mapigo ya moyo ambayo siyo ya kawaida.
-Kuongeza uwezo wa kusukuma damu mwilini na kuchuja mafuta yaliyomo kwenye damu kwa uhakika zaidi.
-Kusaidia kupunguza mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa.
-Kusaidia kupunguza uzito ulokithiri.
-Kuongeza mtiririko w hewa ya oksijen kwenye damu.
-Kusaidia mwili katika kulainisha misuli ya mwili.
-Kusaidia kujikinga na maradhi ya mara kwa mara na kuongeza seli nyekundu za mwili.
















Wadau wa aerobics wakifanya mazoezi kwa
ajili ya afya njema.

Wednesday, April 11, 2012

ZOEZI YA KUONDOA TUMBO KWA KUTUMIA MASHINE IITWAYO (TOTAL MOTION MACHINE)

Mdau wa mazoezi Elasi Njenga ambaye amepata amepata mafanyikio ya mtokeo mazuri kwenye kufanya mazoezi kwa bidii na kupunguza kilo nne kwa mwezi moja tangu alipoanza mazoezi.
Kwa wale wanaomjua wameona mafanikio makubwa na hata mwili wake kwa sasa unapendeza na kujisikia raha na afya, ikiwa pamoja na mazoezi ya aerobics ndio huleta mafanyikio ya haraka.















Mdau wa mazoezi Elias akiwa kwenye moja ya
mashine ambayo husaidia kuondoa tumbo na
kujenga misuli ya mwili ili kuondoa mafuta yale
yasiyohitajika .
Picha inaonyesha namna ya kuanza zoezi hilo.
















Hapa ni namna ya kumalizia zoezi hilo.















Hapa mdau Elias akimalizia zoezi hilo picha hiyo
ikionyesha upande wa nyuma.

Wednesday, April 4, 2012

UMUHIMU WA KUPASHA MWILI JOTO KABLA YA KUANZA ZOEZI(warm up) NA KUNYOOSHA BAADA YA ZOEZI(stretching)

Umuhimu wa kupasha moto misili kabla ya kuanza mazoezi kwa sababu ya kuutayarisha mwili kwa zoezi unalotaka kufanya.
Faida yake ni kuepuka maumivu ya misuli yasiyokwisha baada ya mazoezi.Hivyo ni muhimu sana kufanya mazezi kwa kupasha mwili joto(warm up) kwa kutumia baiskeli za mazoezi ukiwa gym
Pia kuna umuhimu wa kufanya azoezi yakunyoosha mwili baada ya mazoez(stretching), kwa ajili ya kuondoa maumivu na uchovu kwenye misuli.


















Hapa ni dada Nailia UDOM akianza mazoezi kwa
kupasha joto mwili kwa kuendelea na zoezi.






















Mama kidogo akipasha moto misuli
kwenye mashine aina ya crosse training
yeye ni hair dresser anapenda mazoezi.






















Mazoezi ya kunyoosha misuli baada
ya zoezi.





















Abigal akimalizia zoezi kwa kufanya
zoezi kunyoosha mwili baada ya zoezi
(stretching)

Friday, March 16, 2012

GYM YA UDSM YASHAMIRI NA ARI YA KUFANYA MAZOEZI YA AEROBICS

Sasa hivi hata Maprofesa wa chuo kikuu cha mlimani wako na ari ya kufanya mazoezi ya viungo
ili kuwa fit katika afya zao pamoja na wale walio karibu na chuo huwa wanajiunga na mazoezi.
















Wadau wa aerobic wakiwa katika mazoezi.















Hapa wadau wakionyesha umaaahiri wao wa
kufanya step aerobics.















Mwalimu O.Swai akitoa dozi ya mazoezi
Chuo kikuu mlimani Dar es salaam.

Friday, March 9, 2012

KUTANA NA MWANA MAZOEZI JAY JAY ALIYEBOBEA NA KUPENDA AEROBICS

JayJay mwenye asili ya Kiasia ni mwanamazoezi wa siku nyingi katika mazoezi Aerobics hapa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla.

Ni mtu ambaye yeye hajibagui kujichanganya na watanzania wenzake bila kujali yeye ana asili ya Kiasia. Pia Jay Jay ameamua kumshirikisha mkewe pia kufanya mazoezi na kuwa na afya bora.











Katika picha wa kwanza ni Jay Jay akiwa katika darasa la step Aerobics katika gym ya UDSM.