Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Thursday, June 24, 2010

NAMNA YA KUPANGILIA MLO WAKO (DIETY) KWA MTU AMBAYE ANATAKA KUPUNGU BILA KUJA NENEPA HAPO BAADAE (2)

KAMA NILIVYOKUZUMZIA WAKATI ULOPITA KATIKA SOMO LETU HILI LA NAMNA YA KUPANGILIA CHAKULA CHAKO (DIETY) KILA SIKU YA MAISHA YAKO.
NILIZUNGUMZIA KWAMBA, INABIDI UPUNGUZE VITU VYA MAFUTA NA KUFANYA MAZOEZI.
LEO HII NAENDELEA KUZUNGUMZIA AINA GANI YA CHAKULA UNACHOTAKIWA KUPUNGUZA ILI IKUSAIDIE KATIKA KUPUNGUZA UZITO BILA KURUDIA PALE ULIKOTOKA.
JARIBU KUPUNGUZA VYAKULA VYA WANGA ILI UPUNGUZE UNENE ULONAO AMBAO UNAKUSUMBUA.
NIKISEMEA VYAKULA VYA WANGA NI KAMA VILE UGALI, CHAPATI, MAKARON HII IKIWA NI AINA YA VYAKULA CHA WANGA.

KUNA WENGINE HUWA WANASEMA HAWALI WANGA LAKINI ANATUMIA KINYWAJI
AINA YA BIA HALAFU ANASEMA HATUMII WANGA. NI MAKOSA KWA SABABU BIA INA WANGA TOSHA NIKIWA NA MAANA HUTENGENEZWA KWA KUTUMIA NGANO.

AINA NYINGINE YA CHAKULA AMBAYO PIA HUONGEZA UZITO BILA WEWE KUJUA NI
NYAMA NYEKUNDU KAMA VILE, NYAMA YA NG'OMBE NA YA MBUZI, UWE UNAKULA NYAMA NYEUPE KAMA KUKU NA SAMAKI KWA MARA NYINGI ZAIDI YA NYAMA NYEKUNDU

HII ITAKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO ULOKITHIRI NA KUKUSUMBUA KWA KIPINDI KIREFU, PIA USISAHAU KUFANYA MAZOEZI JAPO MARA TATU AU TANO KWA WIKI.

Thursday, June 17, 2010

MWALIMU MNUBI AKIWA COLOSSEM GYM DSM

IJUE GYM KISASA YA COLOSSEM ILIYOPO OYSTERBAY AMBAYO INA SEHEMU TOFAUTI ZA KUFANYIA MAZOEZI KAMA VILE AEROBICS, AQUA AEROBICS, GYM SPINER CLASS.

KWA KWELI NI GYM KUBWA HAPA DAR ES SALAAM NA YA KISASA KABISA


MWALIMU MNUBI WA MAZOEZI YA VIUNGOKATIKA GYM YA COLOSSEM

MWALIMU SALUM AKIWA KWENYE DARASA LA AEROBICS

KIJANA SALUM NI MWALIMU MAHIRI NA MZOEFU KATIKA KAZI YAKE YA KUFUNDISHA MAZOEZI YA VIUNGO.
MWALIMU SALUM MPAKA SASA ANA TAKRIBAN MIAKA 12 KATIKA KUFANYA HII KAZI YAKE.
KATIKA MAHOJIANO YETU YEYE HUPENDELEA KUJIENDELEZA NA PIA HUPENDA SANA KUDADISI MAMBO YANAYOHUSU MAZOEZI.
PAMOJA NA AEROBICS PIA HUFUNDISHA (GYM) YAANI KUTUMIA MASHINE ZA KISASA

KWENYE PICHA SALUM YUKO KATIKA DARASA LAKE AKIFUNDISHA STEP AEROBICS KATIKA COLOSSEM GYM

Tuesday, June 15, 2010

NAMNA YA KUFANYA MPANGILIO WA CHAKULA(DIETY) ILI USIJE UKANENEPA TENA BAADAE KAMA ZAMANI.

MARA NYIGI SANA UTAKUTA WATU WAKIDANGANYANA KUHUSU NAMNA YA KUFANYA DIETY.
HII NI KWA SABABU YA KUTOKUWA NA UELEWA WA NAMNA GANI MWILI WAKO UNATAKIWA KUWA AU KUUFANYIA PINDI UNAPONENEPA.

HAYA MATATIZO MARA NYINGI HUWAKUTA KINA MAMA NA AKINA DADA WALE AMBAO WAMEPANIA KUPUNGUZA MWILI, LABDA KAAMBIWA NA DAKTARI, AU AMEONA KWAMBA KILA AVAAPO NGUO HAIMPENDEZI, NDIPO HUAMUA KUJINYIMA KULA AU KULA VITU VYA AJABU BAADAE HUMLETEA MADHARA.

KWA MFANO MTU ANAKUAMBIA ETI UNYWE NDIMU GLASI MOJA KILA SIKU NDIYO INAYOKONDESHA AU UJINYIME KUTOKULA KAWAIDA KWA MUDA WA WIKI MBILI KWELI UNAJITAKIA MEMA, MAADA BAADA YA HAPO UNAPATA VIDONDA VYA TUMBO.
NA UZITO UNARUDI PALE PALE,PINDI UENDELEAPO KULA KAWAIDA.

KAMA UMEAMUA KUFANYA DAYATI NI KUPUNGUZA MLO UNAOKULA NA KAMA ULIKUWA UNAKULA MAFUTA MENGI KWENYE CHAKULA PUNGUZA PIA.
PIA UJITAHIDI KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU. MWILI HUNENEPA KUTOKANA NA KULA BILA MPANGILIO.

PINDI UFUATAPO HAYA MAELEKEZO UTAISHI BILA YA KUPEWA MASHRTI NA DAKTARI NA KUJISIKIA RAHA WAKATI WOTE.

Friday, June 11, 2010

GENESIS HEALTH CLUB NA MAMA MZUANDA

GENESIS HEALHT CLUB NI CLABU YA MAZOEZI YA VIUNGO YENYE KUENDESHA MAZOEZI YA AEROBICS, SAUNA,STEAMING BATH, KARATE NA PIA SEHEMU YA MASSAGE

Katika picha hapo ni mama Mzuanda
ambaye ni mmiliki wa gym hiyo
akipokea wadau wake na kuwakaribi
sha. pindi wafikapo hapo kwenye mazoezi.





GENESIS HEALTH CLUB NA WAALIMU MAAHIRI

KATIKA CLABU HII JINA LA MWALIM MOSES SIYO GENI YEYE AMEBOBEA KATIKA KUFUNDISHA MAZOEZI YA AEROBIC KATIKA CLABU YA GENESIS ILIYOPO K/NYAMA MAJI MACHAFU KWENYE KITUO CHA OIL COM.
PINDI UINGIAPO KWENYE DARASA LAKE HUWA NI MWALIMU MCHANGAMVU HUKU AKUFUNDISHA DARASA LAKE NA MIRUZI KIBAO UTAPENDA HIYO NDIYO STAILI YAKE.

NILIPOMUULIZA MATARAJIO YAKE NI NINI KUWA MWALIMU WA AEROBICS ALINAMBIA NDOTO YAKE NI KUFANYA KAZI UGHAIBUNI ILI AWE MWALIMU WA KIMATAIFA.

Malimu Moses akifundisha darasa




Picha ya chini ni mwalimu Salum akifundisha mdau wa genesis gym.

Tuesday, June 8, 2010

AINA YA MAZOEZI YA TUMBO KWENYE PICHA

MAZOEZI YA TUMBO NAMNA YANAVYOANZA NA KUMALIZIA UNATAKIWA UENDE KAMA MARA KUMI
NA KURUDIA HIVO KAMA INAVOONYESHA 10x 5 NA UKIMALIZIA UNAKUNJA MIGUU YAKO MIWILI NA KUIKUMBATIA KAMA PICHA YA MWISHO INAVOONYESHA HII NI KWA AJILI YA KUONDOA MAUMIVU YA MUSULI YA TUMBO.
FANYA MAZOEZI HAYA KULA SIKU UTAPATA MATOKEO.














MAZOEZI YA MAPAJA KWA WALE WENYEMAFUTA MENGI NA KUPUNGUZA

MAZOEZI YA VIUNGO HUWA YANAFANYWA KWA UTULIVU NA MAKINI KWA YULE ANAYEFANYA NA KUPATA MATOKEO MAZURI.
KWA SABABU UNAHITAJI KURUDIA ZOEZI HILO KAMA MAELEZO YANGU YANAVYOKWENDA.

-UNALALA KWA UBAVU MMOJA NA KUKUNJA MIGUU YAKO PAMOJA NA KUANZA KUNYANYUA PAJA MOJA LILILO JUU YA JINGINE NA KUURUDISHA CHINI LAKINI USIGUSE PAJA LA CHINI UNALIRUDISHA MPAKA MARA KUMI YAANI 10x3 HALAFU UNABADILISHA UPANDE MWINGINE KWA HESABU KAMA ZA MWANZO.

HII ITAKUSAIDIA KUPUNGUZA UKUBWA WA MAPAJA YAKO NA KUKUWEKA KATIKA HALI YA MVIRINGO WA KAWAIDA BILA KUWA NA MAFUTA.

FANYA HIVI KILA SIKU KWA MUDA WA WIKI TATU NA UTAONA MATOKEO YAKE.


HAPA CHINI KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA ZOEZI HILO LA MAPAJA NA MWALIMU SWAI






Thursday, June 3, 2010

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA MGONGO NA MWALIMU SWAI

MARA NYINGI HUWA KUNA MATATIZO YA KUUMWA MGONGO AU KUSIKIA UMECHOKA NA HATA KUSABABISHA MAUMIVU MAKALI, HII HUTOKANA LABDA KWA KUKAA KWA MUDA MREFU UKIWA OFISINI AU UNAENDESHA GARI KWA MUDA MREFU.

MAUMIVU HAYA YANAWEZA KUKUFANYA KUTOJISIKIA RAHA HATA PINDI ULALAPO KITANDANI NA KUWEKA HILA YA KUBADILI GODORO LAKO LA KULALIA MARA KWA MARA.

KABLA YA KUFIKIA HIVYO AU KAMA UNA TATIZO KAMA HILO. NI VEMA UFANYE MAZOEZI YA MGONGO KUFUATIALIA KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA NA MWALIMU SWAI.

NI VIZURI UFANYE MAZOEZI HAYA ASUBUHI PINDI UAMKAPO NA JIONI UKIRUDI NYUMBANI.



HAPO CHINI PICHA ZINONYESHA MAZOEZI AINA MBILI TOFAUTI NAMNA UNAVYOANZA NA KUMALIZIA ZOEZI















Wednesday, June 2, 2010

SUPER FITNESS GYM NA MWALIMU OTHMAN




WANACHAMA WA SUPER GYM KATIKA MAZOEZI






Super Gym siyo jina geni kwa wakazi wa maeneo ya kariakoo iliyoko katika mtaa wa GoGo, Sikukuu/Mchikichini tukizingatia ni sehemu ya biashara.
Mwalimu Othman ni mtaalam aliyebobea katika fani hii ya mazoezi ya viungo kwa takriban miaka 20 iliyopita.

Yeye amesomea hii kazi yake huko Canada na kuhitimu stashahada ya juu na pia aliwahi kufaya kazi huku ulaya kwa miaka kadhaa na ndipo alipoamua kuja nyumbani Tanzania Dar es salaam kufungua sehemu ya mazoezi ya kujenga mwili.



Pia mwalimu Othman hutengeneza mashine zake yeye mwenyewe pindi ziharibikapo mambo haya yote ni mafanyikio aliyopata huko ulaya.




















HAPA PICHA ZINAONYESHA MWALIMU OTHMAN AKITENGENEZA MASHINE YA KUKIMBILIA