Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, December 28, 2010

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU UDSM WAPATA HAMASA YA KUFANYA MAZOEZIYA KUJENGA MISULI

Katika picha hapo chini inaonyesha wadau wanafunzi wa UDSM wakijifua katika mazoezi ya kujenga misuli.



Friday, December 24, 2010

RAISI WA UDSM AKIWA KWENYE GYM NA WADAU WA MAZOEZI

Hivi ndivyo wadau wa gym ya Mlimani UDSM wakifurahia mazoezi katika mashine wakiwa na raisi wa wanafunzi wa Udsm.




Thursday, December 23, 2010

CHUO KIKUU DAR ES SALAAM YAFUNGUA GYM YA KISASA YA MAZOEZI

KATIKA PICHA HAPO CHINI NI WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS WAKIONGOZWA NA MWALIMU OMAR SWAI AMBAE NI MTAALAMU WA MAMBO YA GYM KATIKA KITENGO CHA ELIMU YA MICHEZO NA SAYANSI(PESS)



Wednesday, December 22, 2010

MWALIMU ADAM KATIKA AEROBICS

Katika picha mwalimu Adam Gwao akiwa kwenye mazoezi ya chini Lamada Hotel




Saturday, December 4, 2010

LIKIZO YA KRISMAS NA NAMNA YA KUCHUNGA USIZIDI UZITO

Mara nyingi kipindi hiki cha mwezi wa Desemba wadau wengi wa mazoezi huwa ni wakati wa kupumzika na kukaa na familia zao, ambao kwa muda mrefu watoto wao walikuwa mashuleni.

Hata hivyo wengine ni wakati muafaka kwa wao kuchukua likizo na kusafiri kuelekea makwao.

Kwa makusudi ninazungumzia kipindi cha skukuu ya krismas ambacho mtu huenda kula bila ya mpangilio na hata kusababisha maradhi ambayo hapo awali aliweza kuyamudu kwa kufanya mazoezi.

Jambo la muhimu ni kujaribu kuchunga usirudi pale ulikotoka na kujiweka katika afya madhubuti uliyonayo hapo mwanzoni kipindi ufanyapo mazoezi.

Kuwe na umuhimu wa kujichunga na uzito ulokithiri kwa kufuata mpangilio wako wa kila siku. Yaani usizidishe chakula kupita ili kuchunga kuongezeka uzito usio na mpangilio maana baada ya siku unaanza palepale kama zamani.

Nini cha kufanya ni wewe kujaribu kutokula wanga kwa wingi na wakati wa usiku upate chakula chepesi.

Nakutakieni KRISMASI NJEMA NA AFYA NJEMA.

Tuesday, November 23, 2010

WAKILI NYANGE MDAU ANAEPENDA MAZOEZI

Mara nyingi watu wanaojishughulisha na sheria huwa hawana muda wa mazoezi, lakini wakili Nyange yeye hakosi mazoezi na anajua kuyafanya na kwa bidii.

Siku hii ya leo nachukua fursa hii kumzungumzia mdau wa mazoezi Wakili Nyange, amefanya mazoezi kwa miaka mingi na anajua faida ya mazoezi,pia amehakikisha familia yake nao wanafanya mazoezi.

Kwa kweli nampongeza sana na kumfagilia na namombea aendelee na bidii yake huwa an jina lake analolipenda wakati wa mazoezi na pia ni staili inaitwa ding dong huipenda sana ambayo mimi nili
buni.


Katika picha hapo chini advocate Nyange amevaa fulana nyekundu na bukta nyeusi anafya mazoezi ya ding dong step kulia nyuma.

Sunday, November 7, 2010

WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS KATIKA HOTEL YA LAMADA

Mara nyigi mazoezi kama haya husaidia kuondoa matairi au mikunjo iliyopo pembeni mwa mbavu.

Hakikisha unafanya mazoezi hayo mara kwa mara husaidia kuondoa mikunjo ambayo imegeuka kuwa mafuta pembeni mwa mbavu kwa muda mfupi,ukizingatia dayati.

Katika picha hapo chini wadau wakifanya mazoezi ya (oblique) yaani kuondoa mafuta pembeni mwa mbavu.

Tuesday, November 2, 2010

KUTANA NA MDAU WA AEROBICS WA SIKU NYINGI MR MGENI

Anajulikana kwa jina la Mgeni lakini siyo mgeni wa mazoezi bali nia mdau aliyebobea katika mazoezi ya aerobics tangu enzi ya uwanja wa taifa hadi leo hii.

Katika picha hapo chini Mgeni yuko na wadau wa kike akiwapa moyo wa mazoezi kulia kwake ni zahra na kushoto erika katika club ya ok body shape iliyopo Lamada hoteli

Thursday, October 28, 2010

MDAU ANAYEPENDA MAZOEZI YA AEROBICS MAJID

Majid ni madau mkuu katika mazoezi ya aerobics amevaa tishet nyekundu na chini nyeupe na raba za nyano ni mmojawapo wa wadau wenye mapenzi kwenye mazoezi ya aerobics kwa hali na mali.

Majid ni Mkurugenzi kampuni ya kubadilisha fedha za kigeni kuuza na kununua hapa Dar es salaam.

Nikisema hivyo sina maana hakuna mdau kama yeye bali yeye huwa amepangia katika maisha yake yote bila kukosa hivyo ni mfano bora wa wiki hii.

Big up Majid

MAZOEZI YA AEROBICS KWENYE MAJI AQUA AEROBICS

Picha chini wadau wa aerobics wakifurahia mazoezi ya aqua aerobics


Monday, October 18, 2010

MAZOEZI NA NAMNA YA KUFANYA DAYATI

Mara nyingi watu hukosea kufuatilia namna ya kufanya dayati, hii hutokea kutopata maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam au walimu wa mazoezi. Mara nyingi mazoezi yanakwenda na dayati yaani kupunguza mlo unaokula, na mwili huja kwa kula bila mpangilio.Lakini ukijitahidi kupunguza mlo na uzito ulokithiri utapungua, pia chakula kinachonenepesha ni kile unachokula wakati wa usiku. Jaribu kula mapema kabla ya kwenda lala na upate mlo ulokuwa mwepesi. Kwa maswali niandikie kupitia omaryswai@gmail.com

Saturday, October 16, 2010

MWALIMU OMAR SWAI KATIKA CLUB YAKE MPYA ILIYOPO LAMADA HOTEL NA WADAU WA AEROBICS

Katika picha ni wiki ya ufunguzi wa darasa la aerobics likiongozwa na mwalimu Swai ilikuwa ni furaha tupu.Clabu hii huwa ni ya mazoezi ya aerobics tu kwa kila rika mnakaribishwa Lamada hotel kwa mazoezi.









High Impact Aerobics hapo juu
Wadau wa aerobics wakiwa wanafanya mazoezi ya tumbo kwa bidii hapo chini huku wakisimamiwa na mwalimu Swai Master class katika hoteli ya Lamada ni siku za mwanzo tangu club hiyo ifunguliwe




























stratching baada ya mazoezi ya viungo ni muhimu,hii husaidia kuondoa maumivu kwenye misuli ya mwili wako.

Wednesday, October 13, 2010

MWALIMU PETRO WA TANZANED GYM AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUFUNDISHA

Mwalimu Petro ni mwalimu mahiri katika ufundishaji wa mazoezi ya gym pamoja na spiner yaani mazoezi ya baiskeli hapo katika gym ya Tanzaned .

Ni mwalimu mwenye bidii na hodari katika kazi yake.

Matarjio yake ni kujiendeleza zaidi katika hii fani ya ufundishaji mazoezi na kuwa wa kimataifa


Mwalim Pertro kushoto akitoa maelekezo ya mazoezi kwa wadau wa mazoezi na wengine wakiwa kwenye mashine za kukumbilia.

Thursday, October 7, 2010

MASTER CLASS OMAR SWAI AFUNGUA CLUB YA AEROBICS

Master class Omar Swai amefunga club ya mazoezi ya aerobics katika hoteli ya Lamada iliyopo barabara ya kawawa karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Wadau wa Aerobics mnawakaribisha mje mpate mazoezi ya aerobics kutoka kwa mtaalam wa mazoezi, mkaribishe na rafiki yako. Mazoezi yanaanza saa kumi na mbili jioni hadi saa moja usiku kila siku ya jumatatu hadi ijumaa mnakaribishwa.

Pia kwa ushauri wa namna ya kuthibiti uzito ulokithiri ambao ulikusumbua kwa muda mrefu na kujiweka katika afya njema.



Master class akiwa kwenye moja ya darasa lake ni burudani tosha

Saturday, September 25, 2010

MWALIMU YASINI AKIWA KATIKA DARASA LA MAZOEZI YA TUMBO KATIKA GYM YA TANZANED

Mwalimu Yasini ni mwalimu aliye makini katika kufundisha mazoezi yaviungo, akiwa amebobea kwa muda mrefu. Wadau wa mazoezi ya viungo wamefaidika naye kujaribu kuwasaidia kuondoa matatizo ya uzito akiwa katika gym ya Tanzaned na gym nyingine anazofundisha jijini Dar es salaam.

Katika picha mwalimu Yasin akitoa maelekezo nakuangalia kama wadau wanafanya vyema mazoezi mbalimbali ya tumbo.







Thursday, September 23, 2010

MWALIMU FRANCIS KATIKA DARASA LA SPINNER

Mazoezi ya spinner yametokea kupendwa na wadau wengi wa mazoezi japo siyo siku nyingi kuanzia hapa bongo.
Mwalimu Francis ni mmoja wa waalimu anayefundisha mazoezi ya spinner katika gym ya Gymkhana club ya Dar es salaam




MWALIMU FRANCIS akiwa kwenye darasa lake la spinner (baiskeli za mazoezi)


















Wadau wa mazoezi wakifuatilia kwa makini master class O.Swai nae alikuwepo.













Monday, September 20, 2010

BONANZA LA AEROBICS PAMOJA NA FAMILIA

Aquar Aerobics vilevile ilikuwepo ili mradi kupata burudani isiyo kifani pamoja na familia katika hoteli ya South beach iliyopo Kigamboni.
AQUA AEROBICS


























Pamoja na michezo mingine hapa ni volleyball
Ni muhimu kuchanganya mazoezi ili usichukie mazoezi na kukutana na familia.