Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, February 25, 2012

ZOEZI LA AEROBICS LINAVYOSAIDIA KUDHIBITI UZITO WAKO

Mara nyingi tunaongezeka uzito uliokithiri kwa sababu ya kula kupita kiasi virutubisho ambavyo vinatakiwa uwe navyo mwilini mwako na kutumika kwa wakati muafaka.
Hivyo basi ni vema ule vyakula vyenye virutubisho bora na kufanya mazoezi, hii pia hukusaidia mwili wako kupunguza uzito ulokithiri na kuwa na nguvu kwenye misuli yako.

Mazoezi ya Aerobics yanasaidia sana kupunguza mafuta yaliyokithiri kwenye mwili wako kwa wakati muafaka.
Kwamfano ukuwa unafaya mazoezi ya kutembea unaweza kuchoma mpaka kaloriz 210 kwa saa,
halafu ukifanya mazoezi ya mpira wa mikono(hand ball) unachoma kaloriz 600 na unapofanya mazoezi ya Aerobics unachoma kaloriz 700 hadi 860 kwa saa.
Kwa hiyo basi unaona jinsi mazoezi ya Aerobics yalivyo na matokeo mazuri katika kupunguza uzito wa mwili wako, hivyo chaguo ni lako ufanye mazoezi yapi kati ya hayo ambayo nimeyachambua.

















Wadau wa Aerobics wakifaya mazoezi hayo huku
wakifuatilia kwa makini kwa mwalimu wao.

Friday, February 17, 2012

KWA NINI SUKARI NI MUHIMU MWILINI MWAKO

Tukizungumzia sukari ni muhimu kwa binadamu yeyote yule nina maama sukari pia ni uhai au ni moja wapo ya kiungo kinachoupa nguvu misili yako.

Hii ni pamoja nakukupa nguvu na uhai kwenye misuli ya moyo wako.Pamoja na hayo kwa wale wanaofanya mazoezi kila siku ni muhimu kutumia sukari ya kawaida nikuwa na maana kuwa mchujo wa sukari kwenye mwili wake ni wa haraka sana na wa kuaminika kuliko wale wasiofanya mazoezi kabisa.

Sababu ni kwamba anayefanya mazoezi hutokwa na jasho na pia hutumia nguvu katika misuli yake ya mwili hivyo sukari huhitajika mara dufu ya yule asiyefanaya mazoezi ya aina yoyote ile.

Dalili unazosikia kama hauna sukari ya kutosha mwilini hujisikia kuwa na mchoko usioisha kwenye mwili hata kama utajipumzisha kwa siku kadhaa.

Halikadhalika ukiwa unafanya mazoezi utajikuta unakosa nguvu za kuendelea na mazoezi kwa muda mfupi hata wakati huo moyo unakwenda mbio na jasho kukutoka huku ukijisikia vibaya sana na mwili kukosa nguvu.mpaka upate huduma ya kwanza kwa kupatiwa glucose(sukari) ndipo unajisikia vema.

Hii ni tahadhari kwa wale wanaoanza kufanya zoezi la aina yoyote.

Friday, February 10, 2012

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA KUJENGA KIFUA KWA KUTUMIA BENCHI PRESS.

Mara nyingi watu ambao hufanya mazoezi, huwa wanatamani kuwa na kifua kilichojengeka na hii ikiwa ni kwa ajili ya kuwa na muonekano mzuri na pindi uvaapo nguo huonekana nadhifu.















Mazoezi ya kujenga kifua wadau wakiwa
wanasimamiana picha ikionyesha namna
ya kuanza zoezi hilo.
















Hapa zoezi la kujenga kifua namna ya kumaliza
ikiwa wamebeba uzito ambao unaumudu.

Monday, February 6, 2012

MAZOEZI YA TUMBO KWA KUTUMIA MPIRA

Katika picha inaonyesha namna ya kuanza zoezi la kupunguza tumbo na namna ya kumlizia
















Katika picha ya kwanza inavyoonyesha jinsi ya
kuanza mazoezi ya kuondoa tumbo unafaya hivyo
kwa kunyanyua mikono yako juu kuvuta pumzi
ndani.















Hapa ni namana ya kumalizia zoezi hilo la tumbo
kwa kutumia mpira.unafanaya hivyo kabadili
mkono na mguu unazungishia chini ya paja lako
mara kwa seti 5x10 halafu unapumziku kwa sekunde
15 na kuanza tena.

















Mdau wa mazoezi ya viungo akifanya mazoezi
ya tumbo picha inaonyesha anavyoanza

















Hapa mazoezi yanavyoishia kwa kupitisha mikono
yako miwili katikati mwa mapaja na mabega ukiwa
umenyanyua unafanya set 3x10