Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, April 30, 2013

GYM YA CHUO KIKUU MLIMANI (UDSM) PESS YAFANA KATIKA MAZOEZI YA AEROBICS

Gym maarufu ambayo inaongoza kwa kutoa mafunzo ya waalimu wa aerobics hapa Tanzania na ambayo ina mwalimu aliyebobea katika mazoezi haya hapa Tanzania mwalimu O.Swai inafana kila kukicha kwenye mazoezi haya.Hivyo akitoa wito kwa wanamazoezi kujiunga katika gym hiyo iliyopo chuo kikuu na kupata mazoezi yaliyokwenda shule kama usemi wetu usemavyo Elimu Kwanza.






                              Mwalimu O.Swai akiwa kwenye darasa lake la step aerobics
                                 chuo kikuu cha mlimani




                              Wadau  wa aeobics wakifuatilia bila kukosea mazoezi ya step






                                  Likiwa ni darasa lililoja wadau wa mataifa mbali mbali
                                  wakifuatilia kwa makini mazoezi.






                         Kushoto mwanzo ni mdau wa mazoezi Isabellah akifuatilia kwa makini






                            Mwalimu Swai akiwa kwenye mwendo mdundo katika mazoezi.

Wednesday, April 24, 2013

CLUB YA MAZOEZI YA AEROBICS YA VETA (DSMRVTSC) SASA YAVUMA



 Ni kwa nadra sana kusikia wafanyakazi  kuamua kufanya mazoezi na kwa moyo kama club ya VETA ambayo inavuma kwa sasa kwa ajili ya kufanya mazoezi, hii ni kwa sababu hata viongozi wao wanapenda mazoezi na kuwathamini wafanya kazi wenzao.
Klabu hii hufanya mazoezi mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu,Jumatano na Ijumaa wakifundishwa na mwalimu  O.Swai akishirikiana na msaidizi wake mwalimu Sukamba.






                                  Mwalimu Sukamba akiwa kwenye darasa lake la aerobics.


                                 Wanawake wafanyakazi wa veta pia wanashiriki ipasavyo



                              Wafanyakazi wa veta wakiwa na kiongozi wao baser wa chiuo
                                  aliyevaa tishet  njano msitari wa kwanza.




                              Wafanyakazi wengi hufurahia mazoezi  na kupata matokeo
                                 mazuri na kuwa na afya njema.

Tuesday, April 23, 2013

MWALIMU WA AEROBICS ABDALA HERRI ANAVYOWIKA ABUDHABI KATIKA KUTOA AINA MBALI MBALI YA MAZOEZI YA VIUNGO



Mwalimu Abdala Herri ni kijana aliyebobea  sana katika mazoezi haya ya aerobics, hata katika mazoezi ya spin yaani kuendesha darasa la  baskeli maalum kwa mazoezi ya mwili yaitwayo spin bike.
Siyo hayo tu pia huendesha darasa la NRG ambalo unatumia barbell na uzito kwa ajili ya kuondoa manyama uzembe.
Pia hutoa ushauri kwa wateja wake ambao wana matatizo mbali mbali ya afya zao.
Hivi sasa  Abdala yukoAbudhabi akifundisha kwenye Gym ya jeshi la  huko na anatarajia kufungua gym hapa Tanzania na huko Mombasa Kenya.




Mwalimu Abdala yuko mbele  kavaa tisheti nyekundu akiwa anafundisha darasa la spin





                    Hili ni darasa la NRG ambalo Abdala anafanyisha mazoezi yake ya mapaja.
                     (squat)kwa ajili ya kujenga misuli wa mbele ya paja





Abdala Herri akionyesha mazoezi kwa ajili ya kujenga misuli ya mgongo





                           Zoezi likiwa limepamba moto yakiongozwa na mwalimu Abdala. Herri.


Friday, April 12, 2013

KOZI YA AEROBICS INAYOFANYIKA CHUO KIKUU MLIMANI YAFANA SANA MWAKA HUU 2013


Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa  Chuo Kikuu Mlimani(School of  Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball  na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.

Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.

Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu  wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo  kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa  ni pamoja na Aerobics and Fitness.





              Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka  China ambao wako na furaha.

 


                 Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.




                         Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.



       Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)




  Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.





Kila mwanafunzi  hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema