Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, December 23, 2011

HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA WADAU WA MAZOEZI YA VIUNGO POPOTE PALE MLIPO ULIMWENGUNI.

NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA SIKUKUU YA KRISMASI HII NA MWAKA MPYA KWA WAPENZI WANGU WOTE WA MAZOEZI YA VIUNGO YA AEROBICS POPOTE PALE MLIPO KATIKA ULUMWENGU WA MAZOEZI.

Wakati huu wa sikukuu mara nyingi watu hujiachia na kula bila kuzingatia wanakula nini hii ni kawaida lakini chunga unachokula naufurahishe moyo wako.

Wednesday, December 14, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA UDSM PESS WANAPOFAIDIKA NA KOZI YA AEROBICS

Katika kozi ya Aerobics sasa inapata umashuhuri mkubwa katika Chuo Kikuu cha Mlimani UDSM katika kitengo cha Elimu ya Sayansi ya michezo.
Hii ikiwa ni kozi ya tatu tangu chuo kikuu cha mlimani kilipoanza kufundisha rasmi,imeonekana kila mwaka wanafunzi wanaongezeka tu hii ni kwa sababu ni kozi ambayo waalimu wa aerobics wanahitajika na mtu hukosi ajira ya ufundishaji iwe kwenye gym za watu binafsi au uwe umejiajiri mwenyewe.


















Katika picha anaonekana mwalimu mwanafunzi
Lulu akiongoza darasa la h/l aerobics PESS DSM.

















Mwalimu mwanafunzi Janifa akiongoza
mazoezi ya step wanafunzi wenzake
UDSM PESS

















Mwalimu wa waalimu Omar Swai (menye kofia
nyekundu)
akiwa katika pozi ya picha na wanafunzi wanao-
somea kozi ya aerobicsPess Udsm.

Thursday, December 1, 2011

NI AINA GANI YA MAJI NA UMUHIMU WA KUNYWA KWA ANAYEFANYA MAZOEZI

Mara nyingi tunapofanya fanya mazoezi iwe ni mazoezi ya viungo au unapocheza mpira na hata unafanya mazoezi ya aina yoyote ile, jua unapunguza maji mwilini mwako kwa kutokwa na jasho unahitaji uongeze maji mwilini mwako.

Lakini kuna watu wengi walipata mafundisho ya kupotoshwa eti huruhusiwi kunywa maji wakati unapofanya mazoezi hadi umemaliza mazoezi na hata ikiwa ni muda wa saa moja au saa mbili hiyo siyo sahihi kabisa.

Mara nyingi unapofanya mazoezi kwanza mwili hupanda joto zaidi ya kawaida, hivyo unahitaji kupoozwa kwa kunywa maji na maji yenyewe yasiwe ya moto kama wengine wanavyojua.
Yawe ni maji ambayo yamepoa yaani yawe na ubaridi kiasi hii husaidia pindi maji yakifika tumboni kuzama mwilini kwa urahisi na kupooza mwili kwa kuteremsha joto lililozidi mwilini.

Pia isiwe baada ya mazoezi bali iwe hata wakati wa mazoezi lakini unywe kiasi cha fundo mbili au tatu kuepuka kichomi.

Kumbuka mwili wako unahitaji maji ya kutosha kwani pasenti 60% ya mwili wako inahitaji maji.
Kunywa maji zaidi ya glasi nane kwa siku.
















Wadau wakifanya mazoezi ya cardio na jasho
huwatoka pia.
















Mazoezi ya Aerobic hutoa jasho sana hivyo maji
ni muhimu wakati wa zoezi na baada ya zoezi.

Thursday, November 17, 2011

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA TUMBO KWA KUTUMIA MPIRA MAALUM.

Kwa kawida mazoezi ya kupunguza tumbo yako ya aina mbalimbali na staili nyingi hii yote ni kumsaidia mlengwa mwenye matatizo na kupungua kama sio kuondoka kabisa.
Mazoezi ya tumbo ni ya kufanya kwa muda mrefu na sio kwa msimu tu hivyo inatkiwa kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi hayo mara kwa mara.
















Namna ya kuanza zoezi la tumbo kwa kutumia
mpira maalum wa zoezi hilo.
unafanya hilo zoezi mara 25x4 halafu unapumzika
kila baada ya seti moja yaani mara 25. kama picha
inaonyesha juu unavyoanza















Picha ya chini inaonyesha namna ya kumalizia
hilo zoezi la tumbo kwa kutumia mpira maalum

Monday, November 7, 2011

MAZOEZI YA KUJENGA MGONGO KWA KUTUMIA MASHINE

Mazoezi mengi siku hizi yameboreshwa kwa kufanya kwa kutumia mashine kwa uhakika na bila ya kuumia sehemu nyingine ambayo haitakiwi kwa wakati muafaka wa mazoezi.
Kama picha zetu zikionyesha wadau wakifanya mazoezi ya kujenga mgongo.





















Katika picha ya juu inaonyesha namna
ya kuanza zoezi la kujenga mgongo hapo
ni mwana mazoezi Wolter akifanya zoezi.





















Hapa Wolter akimalizia zoezi la kujenga
mgongo huku patna wake wa mazoezi
Maiko akisubiria zamu lake

Thursday, October 27, 2011

NAMNA YA KUTUMIA MASHINE KWA MAZOEZI YA MGONGO

Huwa ni mazoea ya wadau wengi hufikiria mazoezi ya kutumia mashine ni kwa ajili ya wanaume tu hapana.
Mwanamke pia anahitaji kufanya mazoezi kwa kutumia mashine hii humsaidia kupunguza mafuta na kujenga misuli haswa sehemu ya mgongo yaani husaidia kuondoa matairi au manyama uzembe.















Hapa mdau wa mazoezi akifanya mazoezi ya
mgongo akiwa anaazia kama picha inavyoonyesha















Mdauwa mazoezi ya viungo akimalizia kuvuta
kama picha inavyoonyesha akiatimia mashine
nayoitwa rowing.

Tuesday, October 25, 2011

MAZOEZI YA AEROBICS KATIKA CHUO KIKUU CHA MLIMANI DAR ES SALAAM















Wadau wakiwa katika muvment ya mazoezi















Wadau wa mazoezi wa chuo kikuu wakiwa
na mwamko wa mazoezi kwa ajili ya afya
zao. wakiongozwa na mwalimu Swai






























Baadhi ya mazoezi wakifuatilia kwa makini
wadau wa mazoezi udsm mlimani

Sunday, October 16, 2011

KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA HAMSINI YA CHUO KIKUU NA BONANZA LA MAZOEZI YA AEROBICS.

KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA MIAKA HAMSINI YA CHUO KIKUU CHA MLIMANI WANAMICHEZO WOTE WALISHIRIKI KATIKA KUPASHA MISULI KWA MAZOEZI YA AEROBICS YA KIONGOZWA NA MWALIMU OMAR SWAI.















Washiriki wa bonanza wakianza na mazoezi ya
aerobics.
















Ilikuwa ni mambo ya cooldown hapa baada ya
aerobics.
















Mazoezi ya kunyoosha misuli kwa matayarisho
ya wanamichezo wa bonanza hilo lililofanyika
katika viwanja vya Chuo kikuu Mlimani.

Saturday, October 15, 2011

SIKU YA BONANZA CHUO KIKUU CHA DAR ESALAAM MLIMANI NA MIAKA HAMSINI

Katika kusherehekea miaka hamsini ya tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Dar es salaamMlimani enzi hizo mpaka hadi leo kulikuwa na sherehe mbali mbali za kushiriki kwenye michezo.



















Hapa akinamama wakijitayarisha kukimbia
mita mia moja siku ya bonanza jumamosi
kwenye viwanja vya chuo kikuu.
















Mbio zilianza hivyo kama inavyookana
hapo juu kwa akina mama.















Akina baba nao walikuwemo katika mashindano
hayo ya mita mia moja.

Friday, October 7, 2011

MIAKA HAMSINI YA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM CHA MLIMANI YAFANA KWA MAZOEZI YA VIUNGO.

Katika shamra shamra za kusherehekea miaka hamsini ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Mlimani mkuu wa chuo hicho Profesa Mkandala akifungua Gym ya mazoezi ya viungo akiwa anasindikizwa na mkuu wa shule kuu ya elimu Eustella Bhalalusesa ambaye pia kitengo hiko kiko chini yake.





















Profesa Ruwekeza Mkandala akikata utepe rasmi kufungua gym.
















Baada ya kukata utepe Profesa Mkandala alijiunga na mazoezi ya aerobic
pamoja na wadauwengine.















Ilikuwa ni siku ya mazoezi tu wadau wakifurahia
mazoezi ya viungo

Wednesday, September 28, 2011

UMUHIMU WA MATAYARISHO KABLA YA KUANZA MAZOEZI (WARM UP)

Wadau wa mazoezi ya viungo leo ngoja niwakumbushe umuhimu wa kufanya mazoezi ya kupasha mwili moto(warm up) kabla ya kuanza zoezi lolote.

Umuhimu wa kufanya hilo zoezi la kupasha mwili moto(WARM UP) ni kuutayarisha mwili kwa mazoezi. Pia husaidia kuongeza usambazaji wa damu katika viungo pamoja na misuli ya mwili pamoja na kuupa mwii joto kwa matayarisho ya mazoezi utakayofanya ambayo husaidia kulainisha viungo vyako vya mwili, hata hivyo husaidia kulainisha mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kusaidia kulinda misuli isipate madhara pamoja na mifupa.

Vilevile kupasha mwili moto(warm up) husaidia kuongezeka upatikainaji wa hewa ya oksijen kwenye misuli na mishipa ya fahamu kwa binaadamu anayefanya mazoezi.

Hivyo mdaua wa mazoezi huo ndio umuhimu wa kupasha mwili moto( warm up) kabla ya kufanya mazoezi.

Friday, September 23, 2011

MAZOEZI YA MGONGO NA UTI WA MGONGO

MAZOEZI YA MGONGO JINSI YANAVYOANZA NA KUMAZIA















Unaanza mazoezi kama picha inavyoonyesha juu















Unamalizia kama picha inavyoonyesha hapo
kwa kurudia 10x10





















Hapa chini ni mazoezi ya uti wa mgongo

Tuesday, September 6, 2011

MAZOEZI AMBAYO MTU YEYOTE ANAWEZA FANYA AKIWA NYUMBANI

Baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan nadhani kila mtu sasa anayofursa ya kufanya mazoezi ya viungo bila ya kuwa na kiwazo labda awe anaumwa. Lakini ukiwa mzima jaribu kufanya mazoezi kama hayo yanasaidia sana kwa kuzingatia maelekezo yake.

















Mazoezi unayoyaona kwenye picha hapo juu ni mazoezi ya sehemu ya mgongo unafanya hivyo na kulala huku mikono yako ikiwa umekita pembeni mwa kifua na kuhakikisha mapaja yanabaki chini kinacho inuka ni sehemu ya juu kama picha inavyoonyesha. Unafanya mara kumi unapumzika halafu unarudia tena kwa mara tatu yaani 10x3 jumla iwe ni mara 30


















Hapa ni mazoezi ya sehemu ya pembeni mwa mbavu(oblique) mazoezi haya yanasaidia kutoa manyama uzembe yaliyo pembeni mwa kiuno na kwenye maeneo ya mbavu kwa kutumia mkono mmoja kupita juu ya kichwa chako kama picha inavyoonyesha hapo juu unafanya 10x3 kila upande.















Mazoezi haya ni saw na yaliyotangulia lakini unatumia mikono yote kama picha inavyoonyesha.

Thursday, August 18, 2011

MAZOEZI KATIKA MFUNGO WA RAMADHANI NA DAYATI YAKE

Mara nyingi watu wengi ambao wanafunga mwezi mtukufu wa ramadhani huwa wanasimama kufanya mazoezi kwa sababu ya swaumu kali na wengine ule muda wa mazoezi ndio wakati wa yeye kwenda kufuturu kwa akina mama wao huwa wanawahi majumbani kutayarisha futari, kwa kweli jambo hilo haliepukiki.

Leo mimi nitajaribu kukupa kidokezo kidogo kuhusu ule namna gani. Katika hilo suala la kula huwa ni gumu kidogo kwa sababu hata aina ya vyakula hubadilika na kuwa wanakula vyakula vya wanga kwa wingi na mafuta ikiwa nazi samli na kadhalika na kwa muda wa futari na halikadhalika daku huliwa usiku wa manane. Kwa wakati huo hakuna msago wa chakula cha aina yoyote katika tumbo.

Kitu cha muhimu epuka kula kupita kipimo na jaribu kunywa maji ya kutosha na ukipata maziwa ya mgando yatakusaidia kuyeyusha kile chakula chenye mafuta mengi, na pia kupata mboga za majani kwa wingi.

NAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

RAMADHAN KARIM


Wednesday, August 3, 2011

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO NA KUPUNGUZA MAPAJA








Jinsi ya kuanza mazoezi ya tumbo na namna ya kumalizia





















Chini kabisa ni mazoezi ya mapaja
kuanza nz kumalizia

Tuesday, July 19, 2011

MAZOEZI YA KUFANYA KWENYE MAJI (AQUA AEROBICS)

Mazoezi ya aqua aerobics hayana tofauti kubwa na mazoezi ya aerobics ambayo unafanyia pasipo maji.
Tofauti ni kwamba aqua nimazoezi yenye usalama zaidi katika viungo kama ankal kuachia na kukufanya kujisikia huna msindilio wa viungo.







Mazoezi ya aqua aerobics huwa nimazuri na salama hapa wadau wakifuatilia kwa makini mwalimu swai akitoa maelekezo.















wadau wa mazoezi ya viungo wakianza kufuatiliana wakiwa wanafurahia

Monday, July 4, 2011

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA TUMBO NA MAZOEZI YA SEHEMU NYINGINE KATIKA MWILI NA KUPATA MATOKEO MAZURI.

Mazoezi kama haya ya sehemu ya chini ikiwa ni kama tumbo na mapaja huwa yanasaidia sana kupunguza kama utarudia kama seti nne hadi tano kwa hesabu ya kumi(4x10) kwa matokeo ya haraka ni kufanya haya mazoezi mfulululizo.







KATIKA PICHA NIMAZOEZI MBALIMBALI YA MWILI.

Monday, June 13, 2011

NAMNA MAZOEZI YANAYOSAIDIA KATIKA AFYA YA KILA BINADAMU



Katika maisha ya kila siku kila binaadamu anakula na hiyo ndiyo kawaida ya mzunguko wa maisha ya kila siku.

Je tunakumbuka kufanya mazoezi ili kuwa na afya bora, jibu linaweza kuwa ndio au hapana hii na kutokana na hulka ya maisha ya mtu ya kila siku.

Kwa kuwa tunanakula kila siku tunahitaji kukitumia chakula ulichokula kwa kufanya mazoezi ili kuepuka maradhi kama ya moyo, kisukari na kuwa na uzito ulokithiri, huna budi kufanya mazoezi katika maisha yako bila kujali umri na jinsia.

Friday, June 3, 2011

CHUO KIKUU CHA UDSM CHAFUNGULIWA GYM NA MKUU WA CHUO HICHO

Mkuu wa chuo kikuu cha mlimani Profesa Mkandala akiwa na anakata utepe wa gym ya mlimani huku mkuu wa shule kuu ya elimu profesa Bhalalusesa akiangalia kwa kuadhimisha miaka hamsini ya tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu hicho
















Katika picha Mwalimu Omar Swai akitoa maelezo
jinsi ya kufanya mazoezi kwenye mashine.















Wadau wa Aerobics siku ya ufunguzi.

Wednesday, May 11, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA CLEMSON CHA AMERIKA WAKIFANYA MAZOEZI YA AEROBICS KATIKA GYM YA UDSM.





Mwalimu Swai akitoa mazoezi ya chini akiwa na wanfunzi wa Chuo Kikuu cha Clemson cha Amerika.
Wanfunzi hao wamekuja kutembelea Chuo kikuu cha Mlimani Dar es salaam katika kitengo cha michezo PESS. kama picha zinavyoonyesha.


katika picha ya pamoja na mwalimu swai