Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Monday, May 14, 2012

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUWA NAYO KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU

Mambo matatu  unayopaswa uyazingatie katika maisha yako ya kila siku ili kuepukana na uzito  uliokithiri.

1. USIWE UNALALA  WAKATI UNAWEZA KUKAA KITAKO

2.USIKAE WAKATI UNAWEZA KUSIMAMA.


3.USISIMAME SEHEMU MOJA WAKATI UNAWEZA KUSOGEA

Hii nikiwa na maana unapokuwa kazini uwe unazingatia hayo mambo matatu,utakuwa umeokoa maisha yako katika ogezeko la uzito wa mwili usiohitajika na kuwa na afya njema wakati wote wa maisha yako.
Mara nyigi ukiwa ofisini jitahidi  kufanya mambo mengi bila ya kutegemea msaada kwa msaidizi, kama vile kunyanyuka na kwenda kuchukua faili kwenye shelfu, kunyanyua kitu au kuzungumza na simu kwa muda mrefu umekaa kwenye kwenye kiti jitahidi uwe  unasimama na kutembea huku unazungumza..
Pia wakati wa kwenda kupata chakula cha mchana jitahidi uende mwendo kidogo ili uupe mwili mazoezi ya kutembea , hii itakusaidia katika usagaji wa chakula kwa wepesi zaidi na kujisikia mchangamfu wakati wote wa maisha yako.


No comments: