Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Sunday, June 21, 2015

MADHARA NA HASARA YA KUWA NA KITAMBI KWA AFYA YAKO


Wako baadhi ya watu ambao wanaona fahari ya kuwa na kitambi tena hujisifu na kusema kama huna kitambi hutopata heshima na kuonekana mchovu yaani huna pesa.

Mimi sikubaliani nao abani  nawaonea huruma kwani tayari wameshakuwa ni wagonjwa japo wao hujiona ni afya.

Kuwa na kitambi ni maradhi ambayo unatembea nayo lakini baada ya siku unakuja kugundua kumbe ulikuwa mgojwa, kwa sabababu kuwa na kitambi  ni mkusanyiko wa mafuta yaliyokithiri mwilini ambayo hutakiwi kuwa nayo.

Mwanadamu kwa kawaida akizidiwa na mafuta mwilini huwa anakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya presha na tena isitoshe ni rahisi pia kupata ugonjwa wa kisukari.

Nawashauri wale wenye vitambi kuondoa mawazo potofu ya kuonekana na kitambi ni heshima, fanya mazoezi kwa ajili ya afya yako, punguza uzito ulokithiri hapo ndipo utafanya mambo yako ya kila siku na kujisikia mwepesi na kuonekana na mvuto hata ukivaa nguo zako. 

Monday, June 8, 2015

MAZOEZI YA AEROBICS YANAVYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO KATIKA GYM YA UDSM



MAZOEZI YA AEROBICS YANAVYOWANUFAISHA WADAU WA MAZOEZI KATIKA GYM YA UNIVERSITY MLIMANI KATIKA PICHA MBALI MBALI .