Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, May 24, 2019

KWA NINI UNAFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU

Mara nyingi katika maisha ya binaadamu yeyote anatakiwa kufanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki. Hii ikiwa ni hali ya kawaida kabisa  kwaajili ya kuondoa mafuta yalozidi mwilini mwako na pia hukusaidia kujenga kuta za misuli ya moyo wako kwa kutembea haraka au kukimbia pia hukusaidia kutumika sukari ya mwili wako kuepukana na maradhi yatokanayo kutofanya mazoezi.

Ni muhimu sana kufanya mazoezi katika maisha yako kuepukana na maradhi mbalimbali.

Friday, February 2, 2018

MAZOEZI MBALI MBALI BAADA YA UKARABATI UDSM GYM

Baada ya ukarabati mubwa wa gym hall ya udsm mazoezi yameanza kama kawaida.

Mara nyingi nasisitiza mazoezi ni muhimu kwa kila mtu ambaye anauwezo huo wa kufanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki ili kuondoa mafuta yalozidia mwilini mwako ambayo husababisha maradhi usotarajia.

                                                         Mashine ya kukimbilia treadmill

                                                Mazoezi ya  miguu unavyoanza na kumaliza
                                       Step cardio ya style mbalimbali

                                     Mazoezi mbali mbali yakiwemo kukimbia na Aerobics

Wednesday, December 13, 2017

UMUHIMU WA KUNYWA MAJI WAKATI WA MAZOEZI NA MWISHO WA MAZOEZI

Maji ni muhimu sana pindi ufanyapo mazoezi na baada ya mazoezi kwa sababu ya kupooza joto la mwili wako na kurudisha katika joto lako la kawaida.Nikisemea hivyo wako watu wengi wanaogopa kunywa maji wakati wanapofanya mazoezi, kwa kuzingatia hivyo maji yenyewe yawe baridi na sio ya moto. Kwa hiyo pasenti 60 ya mwili wako ni maji. Pia unatakiwa kunywa maji yasiyopungua lita mbili kwa siku.

Tuesday, October 10, 2017

MAZOEZI MBALIMBALI YA KUONDOA TUMBO

Mara nyingi tatizo la tumbo huwa ni changamoto kubwa kwa watu wengi kukimbilia kufanya mazoezi ili kuondoa hilo tatizo la kuwa na tumbo kumbwa.

Hapa nakupatia namna ya kufanya zoezi ukiwa nyumbani au sehemu yoyote utaweza kufanya haya mazoezi.

             


                                      Mazoezi ya tumbo namna inavyoanza na kumalizi
                                       unanyoosha mikono nyuma kichwa chini na
                                       ukinnyanyuka unagusa magoti ulokunja

                                        Hili zoezi linalingana kama la kwanza lakini unakuwa
                                     umenyoosha mguu na mikono ukinyanyuka unagusa goti.


                                          Zoezi hili linaonyesha unavyoanza na kumalizia


                                 Zoezi  la upande wa mbavu picha zikionyesha namna ya 
                                  kufanya zoezi hilo


Wednesday, August 2, 2017

NINI MAANA YA DAYATI NA FAIDA ZAKE KWA ANAYEFANYA NA ASIYEFANYA MAZOEZI

Mara nyingi watu hudhani kuwa kufanya dayati ni kutokula kabisa, la hasha hizo ni fikra potofu kwa mwana mazoezi ambazo zimerithiwa na wale ambao hawajui namna au maana ya dayati, Dayati maana yake ni kubadili  mfumo wako wa kula kula bila ya mpangilio.

Kubadilisha tabia ya kula bila mpangilio na kula kiasi kidogo cha chakula haswa wakati wa usiku ili kuepuka uzito maana nyakati za usiku unakuwa hufanyi shughuli yoyote ile ya kutumia chakula ambacho ulichokula kwa usiku ule hivyo basi kile chakula hubadililika na kuwa mafuta na kwenda kujikusanya sehemu mbalimbali ya mwili wako. Kwa wale ambao hawafanyi mazoezi hupata shida ya kuongezeka uzito mara kwa mara.Kama unataka kupungua uzito punguza chakula unachokula na kula mboga za majani kwa wingi na mtunda kwa ajiliya kuepuka vyakula venye  mafuta mengi. Fanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki.

MAZOEZI AINA MBALI MBALI KWA KUJIWEKA NA AFYA NZURI  YA MWILI WAKO

                                                               Mazoezi ya tumbo kuondoa mfuta
                                                   Zoezi la kunyoosha  misuli ya mgongo
                                   Kufanya mazoezi ya Aerobics kwa ajili ya kupunguza uzito
                                 Mazoezi ya kutengeneza misuli yako na kuonekana nadhifu

Wednesday, May 24, 2017

MAZOEZI YA KICK BOXING NAMNA YA KUFANYA


Kuna aina nyingi ya mazoezi  kwa ajili ya kukufanya uwe na afya bora na kukupa nguvu mwili wote. Mazoezi haya ya kick boxing ni mazoezi ya kutumia nguvu zako wakati wote ukiwa unafanya mazoezi haya.

Pia hukufanya uwe na nguvu zisizoishia pamoja na pumzi yako.







                                   Mwalimu Swai akionyesha wanamazoezi hilo

                                      zoezi la kick boxing namna ya kuanza kwa 

                                        kurusha jab kama picha inavyo  hapo juu


                                        Wana mazoezi wakifuatilia na kufanya zoezi



                                   Mwalimu  Swai akipita na kuwarekebisha wana

                                    mazoezi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam 

                            Mwalimu akionyesha namna ya kupiga jap moja ya zoezi

                               Zoezi likiwa linaendelea ni la upper cut ambalo 

                                       husaidia kuwa na nguvu ya mikono 





Saturday, April 8, 2017

KOZI YA WAALIMU WA AEROIBICS YAANZA CHUO KIKUU UDSM 2017

                               Wanafunzi wa mwaka wa tatu wakiwa katika mafunzo ya awali
                                ya aerobics
                                 Wanafunzi wakifurahia mafunzo ya awali ya kozi ya aerobics
                                   Mkufunzi  O.Swai(akiwa kulia mwenye kapero nyeusi)katika
                                     picha ya pamoja na   wanafunzi wake wa aerobics 2017.
                               

Saturday, February 25, 2017

MAZOEZI TOFAUTI YA KISAIDIA SANA KUFANYA UKIWA NYUMBANI PEKE YAKO


Mazoezi  ya tumbo huwa ni muhimu sana kufanya katika maisha ya kila siku, hii ikiwa na maana unakula chakula kila siku na ni muhimu kutumia chakula ulacho kwa kufanya mazoezi. 



                                     Zoezi la tumbo namna unavyoanza hilo zoezi
                                   Jinsi unavyomaliza mazoezi ya tumbo kwa kuinuka
                                   upande mmoja hadi mwingine kushika sakafu kama
                                   picha zinavyoonyesha hakikisha unakaza tumbo pindi
                                   ufanyapo zoezi hilo.


                                        Zoezi la mgongo jinsi unavyoanza kwa mbele


                                  Zoezi la mgongo kwa upande ukiwa unanyoosha mkono
                                  na mguu mmoja ukiwa kwenye floor. kama picha ilivyo
















Thursday, January 19, 2017

MAZOEZI BAADA YA MAPUMZIKO YA MWISHO WA MWAKA

Baada ya mapumziko na kuingia mwaka mpya leo nakuletea mazoezi mchanganyiko baad ya mapumziko kama picha tofauti zikionyesha mazoezi mbali mbali





                                        Karibuni tena katika mazoezi yetu kama kawaida

Thursday, December 29, 2016

MAPUMZIKO YA KUFANYA MAZOEZI NI JAMBO LA MUHIMU


Kuna umuhimu wa kuwa na muda wa mapumziko ya kutosha katika kufanya mazoezi, hii ikiwa ni  kipindi cha mwisho wa mwaka.

Sababu za kupumzika ni  kuipa misuli ya mwili kujipanga vizuri na kukuwa. Pia hii husaidia kuuondoa maumivu mwilini na kusaidia mwili kujipanga na kupungua.

Sababu ingine nikukufanya uwe na hamu ya kurudi mazoezini baada ya mapumziko ya muda wa wiki mbili. Pia husaidia kujua mwili wako ulivyo  kubali kupungua au kujengeka kimazoezi.

JAMBO LA MUHIMU NI KUJITAMBUA UNATAKA NINI UNAPOAMUA KUFANYA MAZOEZI AMBAYO HUENDA SAMBAMBA NA MPANGILIO  WA  CHAKULA.


Thursday, November 24, 2016

MLO WA SIKU NI KIFUNGUA KINYWA (A MEAL OF A DAY IS BREAKFAST)


Kwa nini nazungunzia Mlo wa siku ni kifungua kinywa' Nikimaanisha kwa wale ambao wanahitaji kujenga  miili yao hawana budi kupata chai nzito ikiwa imeshehena matunda,protini ikiwa ni kama nyama kiasi cha nusu kilo asubuhi hii ni kwa ajili ya wale wenye kujenga misuli kwani wanahitaji protini ya kutosha kwa ajili ya kupata virutubisho vya kujenaga misuli.

Halikadhalika awe anapata miilo zaidi ya mitatu nikimaanisha mara tano kwa siku awe anakula .Kila baada ya zoezi unatakiwa kupata aina ya chakula cha wanga, hii ikiwa ni mahitaji ya mjenga misuli anahitajika kula kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kurudishia viambatanino vilivyotumika wakati wa mazoezi.



                           Mwili uliojengwa  kwa mazoezi na kula ipasavyo.(Body Builder)

Wednesday, October 12, 2016

MAZOEZI YA KUJENGA MKONO BICEPS CURL KWA KUTUMIA CABLE MACHINE

Kuna aina  nyingi za kufanya mazoezi ya kujenga mikono kwa wakati mwingine unafanya kwa kutumia free weight, kama vile dumbell au barbell.

Kwa leo tunaanza na mazoezi ya mkono kwa kutumia cable mashine namna unavyoanza na kumaliza.Mazoezi haya unafanya seti tatu kwa hesabu ya kumi na tano kila mkono



                                          Jinsi ya kuanza zoezi la (mkono) biseps curl na
                                           kumalizia kama picha zikionyesha juu na chini                      
                                            Baada ya kubadilisha mkono wako nakufanya 
                                            zoezi hilo hilo la biceps curl seti 4x15..

Tuesday, September 13, 2016

MAZOEZI AMBAYO WAWEZAFANYA HATA UKIWA NYUMBANI HASWA KAMA HUJAWAHI KUFANYA MAZOEZI


Mara nyingi watu hufikiria kuanza kufanya mazoezi pindi akiwa na tatizo la uzito au daktari  kamshauri aanze kufanya mazoezi.

Mimi nashauri isifikie hapo maana mazoezi ni jambo la muhimu  mtu yeyote yule anayekula vizuri na pia ni dawa, hukufanya kuwa mchangamfu wakati wote wa maisha yako.


                                        Zoezi hili hapa linaitwa jumping lunge unakuwa
                                       kama unaruka ukirudi chini unakunja goti lako na
                                       unafanya kwa sekunde 30 halafu unabadili miguu.
                                            Zoezi la jumping lunge kumalizia mguu mwingine




                        Picha hizi mbili zikionyesha namna ya kufanya zoezi la tumbo
                         ukiwa umesimama kwa kuanza mguu wako nyuma na kupandisha
                         juu huku goti lako limejikunja na mikono yako kwenda nyuma
                         kama picha ya juu ikionyesha unavyoanza na ya chini ukimaliza
                         unafanya kwa muda wa sekunde  45 halafu unapumzika na kurudia
                            tena.
                                   Zoezi hili linaitwa  Side bridge ukiwa umelala upande na 
                                    kunyanyuka juu kwa kutumia mkono mmoja unakaa kwa 
                                    sekunde 30 kama picha inavyoonyesha na kubadilisha upande
                                    mwingine 

Monday, August 8, 2016

AINA YA MAZOEZI YA TUMBO NA FAIDA ZAKE KWA MUDA WA DAKIKA 20 TU.

Yapo aina mbalimbali ya mazoezi ya kuondoa tumbo ambalo limekuwa likisumbua kutopungua.

Yafuatayo ni aina mbalimbali ya mazoezi ambayo yanasaidia kwa  kufanya kwa muda wa dakika 20 tu.




                                         Zoezi la Bicycle crunh ambalo unafanya kwa muda
                                         wa sekunde 60 kama zoezi linavyoonyesha hapo juu,



                               Zezi hili la Glute bridge leg rise unafanya zoezi hili kwa sekunde
                               30 na kubadili mguu mwingine kwa muda huo.


 
 Zoezi hili linaitwa Dorsal rise unafanya kwa muda wa 
             sekunde30 halafu unapumzika kwa sekunde15 na kuanza tena,