Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, December 23, 2011

HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA WADAU WA MAZOEZI YA VIUNGO POPOTE PALE MLIPO ULIMWENGUNI.

NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA SIKUKUU YA KRISMASI HII NA MWAKA MPYA KWA WAPENZI WANGU WOTE WA MAZOEZI YA VIUNGO YA AEROBICS POPOTE PALE MLIPO KATIKA ULUMWENGU WA MAZOEZI.

Wakati huu wa sikukuu mara nyingi watu hujiachia na kula bila kuzingatia wanakula nini hii ni kawaida lakini chunga unachokula naufurahishe moyo wako.

Wednesday, December 14, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA UDSM PESS WANAPOFAIDIKA NA KOZI YA AEROBICS

Katika kozi ya Aerobics sasa inapata umashuhuri mkubwa katika Chuo Kikuu cha Mlimani UDSM katika kitengo cha Elimu ya Sayansi ya michezo.
Hii ikiwa ni kozi ya tatu tangu chuo kikuu cha mlimani kilipoanza kufundisha rasmi,imeonekana kila mwaka wanafunzi wanaongezeka tu hii ni kwa sababu ni kozi ambayo waalimu wa aerobics wanahitajika na mtu hukosi ajira ya ufundishaji iwe kwenye gym za watu binafsi au uwe umejiajiri mwenyewe.


















Katika picha anaonekana mwalimu mwanafunzi
Lulu akiongoza darasa la h/l aerobics PESS DSM.

















Mwalimu mwanafunzi Janifa akiongoza
mazoezi ya step wanafunzi wenzake
UDSM PESS

















Mwalimu wa waalimu Omar Swai (menye kofia
nyekundu)
akiwa katika pozi ya picha na wanafunzi wanao-
somea kozi ya aerobicsPess Udsm.

Thursday, December 1, 2011

NI AINA GANI YA MAJI NA UMUHIMU WA KUNYWA KWA ANAYEFANYA MAZOEZI

Mara nyingi tunapofanya fanya mazoezi iwe ni mazoezi ya viungo au unapocheza mpira na hata unafanya mazoezi ya aina yoyote ile, jua unapunguza maji mwilini mwako kwa kutokwa na jasho unahitaji uongeze maji mwilini mwako.

Lakini kuna watu wengi walipata mafundisho ya kupotoshwa eti huruhusiwi kunywa maji wakati unapofanya mazoezi hadi umemaliza mazoezi na hata ikiwa ni muda wa saa moja au saa mbili hiyo siyo sahihi kabisa.

Mara nyingi unapofanya mazoezi kwanza mwili hupanda joto zaidi ya kawaida, hivyo unahitaji kupoozwa kwa kunywa maji na maji yenyewe yasiwe ya moto kama wengine wanavyojua.
Yawe ni maji ambayo yamepoa yaani yawe na ubaridi kiasi hii husaidia pindi maji yakifika tumboni kuzama mwilini kwa urahisi na kupooza mwili kwa kuteremsha joto lililozidi mwilini.

Pia isiwe baada ya mazoezi bali iwe hata wakati wa mazoezi lakini unywe kiasi cha fundo mbili au tatu kuepuka kichomi.

Kumbuka mwili wako unahitaji maji ya kutosha kwani pasenti 60% ya mwili wako inahitaji maji.
Kunywa maji zaidi ya glasi nane kwa siku.
















Wadau wakifanya mazoezi ya cardio na jasho
huwatoka pia.
















Mazoezi ya Aerobic hutoa jasho sana hivyo maji
ni muhimu wakati wa zoezi na baada ya zoezi.