Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Monday, December 16, 2013

JINSI UNAVYOTAKIWA KULA UKIWA UNAFANYA MAZOEZI YA KUJENGA MISULI

Mara nyingi kwa  wale ambao wanataka kujenga misuli hawakumbuki au kuwa na uhakika wa mlo ambao anatakiwa kula.
Kwa sababu ninapata maswali mengi kuhusu aina ya chakula anatakiwa kutumia wakati afanyapo haya mazoezi ya kujenga misuli.

AINA YA VYAKULA 
1.Awe anapata chakula cha wanga kwa ajili ya kuupata nguvu.(kama makaroni,chapati,ugali na wali)
2.Chakula cha protini kwa ajili yakujenga misuli kwa haraka(kama kuku,samaki,figo,na nyama)
3.Apate aina mbali mbali ya matunda.
Kula  zaidi ya miilo 3 iwe mara tano na mazoezi ya kutosha kwa kuongeza uzito kila baada ya seti.

Friday, November 1, 2013

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA MBOGA MBOGA INAYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

 Hebu leo tuangalia faida ya kutumia juisi ambayo ni mchanganyiko wa matunda na mboga mboga ambayo husaidia kupunguza uzito. Juisi yenyewe inamchanganyiko wa mboga na matunda, ikiwa na virutubisho vyote vinanyohitajika mwilini.
Hii hapa ni jinsi ya kutayarisha aina ya vitu vinavyohitajika
1.Uwe na mashine ya kutengezea hiyo juisi(Juice maker)
2.Karrot
3.Matango mawili
5.Cornflower ya kijani
6.Apple 2
7.Spinach


                                                    Karoti za kutosha


               Mashine ya kutengenezea juisi yenyewe pamoja na mchanganyiko wa mboga




                                                     Mboga za spinach



                        Muonekano ya juisi yenyewe ukisha tengeneza tayari kutumia

Friday, October 4, 2013

MWANA MAZOEZI MHADHIRI WA CHUO KIKUU MLIMANI AWA MFANO KWA WENZAKE

Katika maisha ya siku hizi ni nadra  sana kukuta mhadhiri wa chuo kikuu kupenda mazoezi na kuhudhuria mara tano kwa wiki bila kukosa.
Leo hii nampongeza sana Dr. Ngoma ambaye yuko na umri lakini amekuwa hodari sana katika kufanya mazoezi akiwa yeye na mke wake hata watoto wake wanahuduria mazoezi.
Hii ikimaanisha kwamba mazoezi ni kwa kila mtu kutojali umri au jinsia.



                                                                                 
                         Dr.Ngoma akiwa katika mazoezi ya step aerobics katika gym ya UDSM
                          (aiyevaa tishet nyekundu hapo mbele kulia)


                        Akiwa katika umaahiri wake wa kupanda step bila ya kukosea Dr.Ngoma


                       Hakuna staili inayompita Dr.Ngoma  kutokana na uelewa wake wa mazoezi

Monday, September 2, 2013

FAIDA ZA KUTUMIA JUICE YA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI


Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali.
Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
Mangenisium
Mangnese
Potasium
Copper
Vitamini B6
Hii ikiwa katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa wataalamu kutengeneza tangawizi ni  tiba tosha kwa magonjwa ya ngozi

Hili hapa kwenye picha ni zao la tangawizi kama linavyoonyesha likiwa bado kusagwa.

Faida  za kutumia tangawizi:
-.Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wnawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
-Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
-Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
-Tangawizi husaidia kupunguz maumivu mwilini
-Husaidia kutoganda kwa damu mwilini
-Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.
Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama

 

Monday, August 12, 2013

MAZOEZI YA MASHINE YA ROWING NA FAIDA ZAKE


Katika dunia ya sasa kuna aina nyingi sana za mazoezi mbali na mazoezi ya Aerobics, ambayo husaidia kupunguza uzito kwa muda fulani.
Mazoezi mengine ambayo hushabihiana na mazoezi ya aerobics ni yale mazoezi ya kutumia aina ya mashine aina ya Rowing mashine.
Faida ya  kufanya mazoezi ya rowing: Husaidia kupunguza uzito kwa kipindi kifupi kwa kuzingatia mzoezi yake.Hupunguza tumbo na kujenga misuli yake.Hupunguza mapaja yalokithiri.
Pia husaidia katika kuujenga moyo  na kuwa mdhubuti. Pia hukupa uwezo wa pumzi yako kuwa ya uhakika.

                Malaika akionyesha  kutumia mashine ya Rowing kuanza zoezi hilo hapo juu.
               (Unakunja miguu yako kwa kwenda mbele)


                        Mazoezi ya Rowing katika kumalizia zoezi hilo ambapo unajivuta nyuma
                         kama mwana mazoezi Mery(Malaika) akionyesha.

Monday, July 15, 2013

NAMNA YA KWENDA NA DAYATI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Awali ya yote nawatkia mfungo mwema kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani wale waislamu popote walipo.
Kuna maswali ambayo mtu unaweza kujiuliza katika mambo yanayohusu ulaji wa mwezi huu mtukufu wa ramadhani ewe mwanamazoezi na namna gani utafanya mazoezi ukiwa  umefunga.
Je utaweza kufanya mazoezi huku umefunga.
Je kuhusu aina gani ya chakula unatakiwa kula.
Katika mwezi huu wa mfungo mtu huwa unachoka ule mda wa jioni ambao unatakiwa kufanya mazoezi inakuwa ni vigumu maana unasikia njaa, kwa hiyo hata mazoezi huwezi kuenda.
Nakupa usauri  wangu katika ulaji wako uchunge sana vitu vya mafuta mengi.
Ukisha maliza kufuturu unywe maji ya kutosha na upunguze kiasi cha chakula ambacho hukuongezea uzito kwa urahisi.
Baada ya kula futari  utembee kwa muda wa dakika 20 baada ya hapo uendelee na mambo yako mengine, hii itakusaidia kusaga kile chakula na kukufanya kuwa mchangamfu.
Upate kahawa baada ya kupata futari hii pia itakusaidia kuondoa yale mafuta yaliyobaki kwenye mishipa yako ya mwili na kuifanya ipanuke na pia huondoa shibe.
Huu ni baadhi ya ushauri kwa wadau wa mazoezi ni muhimu kuzingatia.

Monday, June 24, 2013

MWALIMU WA AEROBICS ALFA SIMWANZA AMALIZA CHUO KIKUU UDSM NA KUANZA KUFUNDISHA


Mwalimu chipukizi katika fani ya aerobics Alfa Simwanza ambaye amemaliza mafunzo yake ya miaka mitatu akiwania cheti cha digirii katika ualimu wa michezo kutoka chuo kikuu cha mlimani(UDSM).
Akiwa ameshiriki katika michezo yote, isipokuwa yeye amejikita katika ufundishaji wa mazoezi ya Aerobics.


Katika picha mwalimu Alfa (bukta buluu) akiwa katika darasa lake kwenye gym ya UDSM




      Mwalimu A.Simwanza akifuatilia kwa makini wanafunzi wakifanya mazoezi





          Mwalimu Alfa akibadili mwelekeo wa mazoezi huku wadau wakufurahia

Friday, June 21, 2013

FAIDA YA MATUMIZI YA KUTUMIA KINYWAJI CHA KAHAWA


Watu wengi hufikiria kahawa ni kwa ajili ya wale watu ambao  hawahitaji kulala, huwa  ndio faida yake tu lakini kahawa ina faida nyigi.
Huwasaidia kukuchangamsha na kuamsha akili na kuondoa uchovu.
Husaidia msago wa chakula kwa urahisi zaidi
Husaidia kupanua mishipa ya damu
Husaidia misuli ya moyo kuwa madhubuti katika msukumo wa damu mwilini.
Husaidia kuondoa mafuta kwenye damu.
Hii  ikiwa ni baadhi ya faida za matumizi ya kahawa kwa binaadamu, na pia imefanyiwa majaribio na kuonekana inasaidia sana katika maisha ya mwanadamu kumfanya kuwa na afya bora na furaha.

Monday, May 20, 2013

WANAFUNZI WAALIMU WA AEROBICS CHUO KIKUU MLIMANI WAMALIZIA KOZI KWA FURAHA.


Waalimu wa kufundisha mazoezi ya aerobics wakiwa wanafikia ukingoni mwa hiyo kozi wakiwemo wametokea sehemu mbali mbali duniani wakisomea mazoezi ya aerobics Chuo Kikuu Mlimani.


Hapa wanafunzi wakiwa darasani kwa vitendo kwenye kozi ya 
high and low aerobics







                             Wakiwa wanapokezana kufaya mazoezi ya kufundisha aerobics






                  Wanafunzi wa mataifa mbali mbali wakifurahia wenzao kuendesha
                    mazoezi




                                Hapa ni mwanafunzi wa mazoezi ya ualimu wa aerobics katika
                                  step aerobics








                     Waalimu wa aerobics  wakiwa kwenye pozi baaada ya mafunzo UDSM
                         PESS





                        Wanafunzi wa aerobics wakiwa na mwalimu Swai aliyevaa kofia






















































Tuesday, April 30, 2013

GYM YA CHUO KIKUU MLIMANI (UDSM) PESS YAFANA KATIKA MAZOEZI YA AEROBICS

Gym maarufu ambayo inaongoza kwa kutoa mafunzo ya waalimu wa aerobics hapa Tanzania na ambayo ina mwalimu aliyebobea katika mazoezi haya hapa Tanzania mwalimu O.Swai inafana kila kukicha kwenye mazoezi haya.Hivyo akitoa wito kwa wanamazoezi kujiunga katika gym hiyo iliyopo chuo kikuu na kupata mazoezi yaliyokwenda shule kama usemi wetu usemavyo Elimu Kwanza.






                              Mwalimu O.Swai akiwa kwenye darasa lake la step aerobics
                                 chuo kikuu cha mlimani




                              Wadau  wa aeobics wakifuatilia bila kukosea mazoezi ya step






                                  Likiwa ni darasa lililoja wadau wa mataifa mbali mbali
                                  wakifuatilia kwa makini mazoezi.






                         Kushoto mwanzo ni mdau wa mazoezi Isabellah akifuatilia kwa makini






                            Mwalimu Swai akiwa kwenye mwendo mdundo katika mazoezi.

Wednesday, April 24, 2013

CLUB YA MAZOEZI YA AEROBICS YA VETA (DSMRVTSC) SASA YAVUMA



 Ni kwa nadra sana kusikia wafanyakazi  kuamua kufanya mazoezi na kwa moyo kama club ya VETA ambayo inavuma kwa sasa kwa ajili ya kufanya mazoezi, hii ni kwa sababu hata viongozi wao wanapenda mazoezi na kuwathamini wafanya kazi wenzao.
Klabu hii hufanya mazoezi mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu,Jumatano na Ijumaa wakifundishwa na mwalimu  O.Swai akishirikiana na msaidizi wake mwalimu Sukamba.






                                  Mwalimu Sukamba akiwa kwenye darasa lake la aerobics.


                                 Wanawake wafanyakazi wa veta pia wanashiriki ipasavyo



                              Wafanyakazi wa veta wakiwa na kiongozi wao baser wa chiuo
                                  aliyevaa tishet  njano msitari wa kwanza.




                              Wafanyakazi wengi hufurahia mazoezi  na kupata matokeo
                                 mazuri na kuwa na afya njema.

Tuesday, April 23, 2013

MWALIMU WA AEROBICS ABDALA HERRI ANAVYOWIKA ABUDHABI KATIKA KUTOA AINA MBALI MBALI YA MAZOEZI YA VIUNGO



Mwalimu Abdala Herri ni kijana aliyebobea  sana katika mazoezi haya ya aerobics, hata katika mazoezi ya spin yaani kuendesha darasa la  baskeli maalum kwa mazoezi ya mwili yaitwayo spin bike.
Siyo hayo tu pia huendesha darasa la NRG ambalo unatumia barbell na uzito kwa ajili ya kuondoa manyama uzembe.
Pia hutoa ushauri kwa wateja wake ambao wana matatizo mbali mbali ya afya zao.
Hivi sasa  Abdala yukoAbudhabi akifundisha kwenye Gym ya jeshi la  huko na anatarajia kufungua gym hapa Tanzania na huko Mombasa Kenya.




Mwalimu Abdala yuko mbele  kavaa tisheti nyekundu akiwa anafundisha darasa la spin





                    Hili ni darasa la NRG ambalo Abdala anafanyisha mazoezi yake ya mapaja.
                     (squat)kwa ajili ya kujenga misuli wa mbele ya paja





Abdala Herri akionyesha mazoezi kwa ajili ya kujenga misuli ya mgongo





                           Zoezi likiwa limepamba moto yakiongozwa na mwalimu Abdala. Herri.


Friday, April 12, 2013

KOZI YA AEROBICS INAYOFANYIKA CHUO KIKUU MLIMANI YAFANA SANA MWAKA HUU 2013


Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa  Chuo Kikuu Mlimani(School of  Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball  na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.

Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.

Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu  wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo  kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa  ni pamoja na Aerobics and Fitness.





              Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka  China ambao wako na furaha.

 


                 Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.




                         Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.



       Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)




  Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.





Kila mwanafunzi  hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema









Thursday, March 14, 2013

MAZOEZI YA AEROBICS YAFANA MJINI MOROGORO






Wakazi wa Morogoro mji uliozungukwa na milima ya uluguru na hali ya hewa nzuri,wakiwa na hamasa kubwa kufanya mazoezi ya viungo kwa afya yao, huku wakiongozwa na mwalimu Musiba  Manyama ambaye ni mwalimu wa siku nyingi katika fani hii.
Gym hii ya mazoezi inaitwa SIMBA OIL GYM iliyopo katika majengo hayo ya Simba oil kituo cha petroli cha mjini Morogoro.


                       Mwalimu Musiba akiwa  katikati  ya wanafunzi akitoa mazoezi ya
                          kunyoosha viungo baada ya zoezi kuisha.




                          Hapa ni mwalimu  mwalikwa   Payas (mwenye kofia) kutoka Dar
                          ambaye ni mkurugenzi wa gym ya Fitness for Life akitoa mazoezi




                                      Kina dada wa Moro nao hawapo nyuma kwa kufanya
                                        mazoezi kwa afya zao




                                  Mwalimu musiba akifanya mazoezi na wadau wake wa
                                       Morogoro .Simba Oili Gym

Friday, February 22, 2013

NAMNA YA KULA MLO WAKATI UNAPOTAKA KUPUNGUA UZITO ULIOZIDI NA MAZOEZI


Kupunguza uzito ulokithiri huchukua muda mpaka kupata matokeo yake,ukiwa unazingatia kufanya mazoezi kama vile kutembea, kuendesha baiskeli na kufanya mazoezi ya aerobics ambayo hukupa matokeo haraka zaidi kuliko mazoezi yoyote yale.

Nikizungumzia mazoezi ya aerobics huwa nina maana kila sehemu ya kiungo cha mwili wako hufanyishwa mazoezi.
Ukizingatia kuanzia mwanzo wa zoezi hilo unaanza na kupasha mwili moto halafu ndio unaendelea na mazoezi mengine huku ukifuatilia ikienda  sambamba na   muziki maalumu kwa mazoezi  tofauti.
Hii hukupa wewe mwanamazoezi kufanya  na kufurahia,baada ya hapo ikifuatiwa na mazoezi kuunnyoosha mwili na kuondoa uchovu kwa kipindi  chote cha mazoezi.
Na kumalizia na zoezi la kuondoa tumbo.

Lakini mazoezi  yanatakiwa uende sambamba na kupunguza chakula kwa mfano ulikuwa unakula sahani iliyojaa unakula nusu yake. Hata hivyo uwe umepata kifungua kinywa cha kutosha itakisaidia kutokula hovyo hovyo.Mchana  utakula kiasi tu  ukipata matunda kwa wingi.
Wakati wa usiku ujitahidi upate chakula chepesi kwani maranyingi chakula cha jioni huongeza uzito kwa sababu ukishakula unaenda kulala na msago wa chakula huwa umesimama hadi kesho yake saa 12 asubuhi.
Pia jitahidi kupunguza mafuta kwenye  chakula hata sukari iwe kiasi na chumvi pia itakusaidia kupunguza uzito.








                     Aina ya mazoezi  ambayo unatakiwa kufanya kama picha  inavyoonyesha

                                 







          Kuna aina nyingi ya mazoezi ambayo husaidia kukupunguza kwa kutumia mashine
                       






















Thursday, February 7, 2013

AINA MBALI MBALI YA MAZEOZI YA VIUNGO(AEROBICS)




Katika kufanya mazoezi ya viungo unaweza pia kufanya mazoezi  kwa kucheza utakavyo ili mradi unaendana na midundo.
Hivi sasa waalimu wa mazoezi haya ya viungo wamegundua namna ya kuwavutia wadau wa mazoezi haya kwa kuwapa mtindo na aina ya muziki







                                             Hapa ni namna  ya kuanza zoezi la kick box






                                         Namna ya kutupa ngumi pamoja kufuatilia mdundo






                                     Jinsi  ya kutumia mateke au kutumia goti uku ukienda na muziki









Mwalimu  Swai akitoa mafunzo namnkukunja na kutupa ngumi



Monday, January 21, 2013

MBAGALA JOGGING CLUB WAKARIBISHWA VETA CLUB KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA

                                             
Klabu ya mazoezi ya viungo ya  VETA    chuo cha ufundi stadi  Dar es salaam ikiwa imewakaribisha wanamazoezi wenzao kutoka klabu ya Mbagala Joging ikiongozwa na mwalimu wao Adam Gwao ambaye pia ni muasisi wa club hiyo. Mazoezi hayo yalifana sana ambayo yalianza  majira ya  saa 12 hadi saa moja asubuhi  yakiwa yamehudhuriwa na wakuu wa chuo hicho cha  Veta.
                                                                                                                        











    Mwalimu Swai  akikakaribisha wanamazoezi  wenzake kutoka  Mbagala  Jogging  club
    akiwa mbele ya wanamazoezi na mwalimu  Adam Gwao tayari kuanza zoezi la Aerobics

                                                                               

                                                                                           



   Mazoezi yameanza pamoja na mkuu wa chuo cha Veta (mwenye fulana ya bluu ) akiwa
   mstari wa mbele.
                     





               Zoezi lilipamba moto kila mtu akiwa  mwenye furaha  asubuhi hiyo ya mazoezi





        Kila mtu alikuwa na usongo wa kufanya zoezi siku hiyo bila kushindwa au kuchoka







               Mkuu  wa chuo cha Veta  Mr. Samwel Ng'andu  akizungumza na wanamazoezi
              na kuwakaribisha wanamazoezi wa Mbagala club  wote wakimsikiliza kwa makini.



                                                                               



     Mwalimu O.Swai akitoa mafunzo ya lishe bora baada ya kumaliza mazoezi ya siku hiyo
     Akisema "Kufanya mazoezi peke yake hayasaidi ila ni pamoja na kujaribu kubadili tabia
       ya  kula mlo".