Lakini kuna watu wengi walipata mafundisho ya kupotoshwa eti huruhusiwi kunywa maji wakati unapofanya mazoezi hadi umemaliza mazoezi na hata ikiwa ni muda wa saa moja au saa mbili hiyo siyo sahihi kabisa.
Mara nyingi unapofanya mazoezi kwanza mwili hupanda joto zaidi ya kawaida, hivyo unahitaji kupoozwa kwa kunywa maji na maji yenyewe yasiwe ya moto kama wengine wanavyojua.
Yawe ni maji ambayo yamepoa yaani yawe na ubaridi kiasi hii husaidia pindi maji yakifika tumboni kuzama mwilini kwa urahisi na kupooza mwili kwa kuteremsha joto lililozidi mwilini.
Pia isiwe baada ya mazoezi bali iwe hata wakati wa mazoezi lakini unywe kiasi cha fundo mbili au tatu kuepuka kichomi.
Kumbuka mwili wako unahitaji maji ya kutosha kwani pasenti 60% ya mwili wako inahitaji maji.
Kunywa maji zaidi ya glasi nane kwa siku.
Wadau wakifanya mazoezi ya cardio na jasho
huwatoka pia.
Mazoezi ya Aerobic hutoa jasho sana hivyo maji
ni muhimu wakati wa zoezi na baada ya zoezi.
No comments:
Post a Comment