Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, September 6, 2011

MAZOEZI AMBAYO MTU YEYOTE ANAWEZA FANYA AKIWA NYUMBANI

Baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan nadhani kila mtu sasa anayofursa ya kufanya mazoezi ya viungo bila ya kuwa na kiwazo labda awe anaumwa. Lakini ukiwa mzima jaribu kufanya mazoezi kama hayo yanasaidia sana kwa kuzingatia maelekezo yake.

















Mazoezi unayoyaona kwenye picha hapo juu ni mazoezi ya sehemu ya mgongo unafanya hivyo na kulala huku mikono yako ikiwa umekita pembeni mwa kifua na kuhakikisha mapaja yanabaki chini kinacho inuka ni sehemu ya juu kama picha inavyoonyesha. Unafanya mara kumi unapumzika halafu unarudia tena kwa mara tatu yaani 10x3 jumla iwe ni mara 30


















Hapa ni mazoezi ya sehemu ya pembeni mwa mbavu(oblique) mazoezi haya yanasaidia kutoa manyama uzembe yaliyo pembeni mwa kiuno na kwenye maeneo ya mbavu kwa kutumia mkono mmoja kupita juu ya kichwa chako kama picha inavyoonyesha hapo juu unafanya 10x3 kila upande.















Mazoezi haya ni saw na yaliyotangulia lakini unatumia mikono yote kama picha inavyoonyesha.

No comments: