Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, May 15, 2010

MWALIMU WA KWANZA MTANZANIA ABDALAH KWENDA KUFUNDISHA AEROBICS DUBAI

Abdalah a.k.a DULLA ni mwalimu wa kwanza kwenda kufundisha aerobics Dubai. Nikisema hivyo nina maana hapo awali hapakuwa na Mtanzania aliyewahi kwenda kuishi huko na kufundisha aerobics.KAMA UONAVVYO KATIKA PICHA NI MSWAHILI PEKEE.
Dulla alianza kufundisha pale Dubai, halafu alichukuliwa na shirika ndege la Etihad na kwenda kuishi Abudhabi, pale alifanya kazi yake kwa mkataba baada ya kumaliza huko sasa ameajiriwa na chuo cha jeshi la huko anafundisha mazoezi ya aerobics huko.
Mwalimu Dulla ni kijana mwenye bidii na upendo na pia hupenda kushirikiana na waalimu wenzake japo ni kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Kwa keli najivunia kijana huyu kwa mafanyikio yake ambayo yana zaa matunda. Alipokuwa kwenye mafunzo alikuwa ni msikilivu na mwelewa ndio maana amefanikiwa katika mambo yake ya kikazi huko ughaibuni.
Mwalimu Dulla ameshawatafutia wabongo wenzake kazi huko Dubai na bado ana bidii ya kupeleka wengine zaidi, hii ni kwa ajili ya bidii yake ya kujituma ndio akaaminiwa na kuleta sifa kwa waalimu wa aerobics Tanzania.
Mwaka jana nilifika Abudhabi huko nikapata hizo sifa zote kwa kujituma kazini na hupenda kujiendeleza kwa kusomea zaidi. mie nampa big up nikiwa kama mwalimu wake wa kwanza.

No comments: