Mwalimu Mango wa gym ya Home Gym siyo jina geni kwa wale wadau wa luninga ya ITV. Monday, May 17, 2010
MWALIMU HENRY MANGO WA HOME GYM
Mwalimu Mango wa gym ya Home Gym siyo jina geni kwa wale wadau wa luninga ya ITV. Kijana Henry Mango alianzisha sehemu yake ya mazoezi katika mwaka wa 2004.ambapo alifungua sehemu ya kunyanyua vyuma kwa ajili ya kujenga misuli huko mwenge Dar.
Baada ya miaka michache alianzisha sehemu ya kufanyisha mazoezi ya aerobics, ambayo anaendelea na kwa sasa ana wadau ambao wengi wao wanatokea sehemu za mwenge.
Nilipomuuliza kiwango cha elimu yake alinambia amefikia darasa la saba lakini amesema atajiendeleza zaidi kielimu, ili apate mafanikio katika kazi hii ya mwalimu wa aerobics .
WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS
WAKIONGOZWA NA MWALIMU FREDY LAUWO AMBAYE YEYE PIA AMEJULIA MAZOEZI KUTOKA KWA MWALIMU MANGO HAPO HOME GYM.
Saturday, May 15, 2010
MWALIMU WA KWANZA MTANZANIA ABDALAH KWENDA KUFUNDISHA AEROBICS DUBAI
Abdalah a.k.a DULLA ni mwalimu wa kwanza kwenda kufundisha aerobics Dubai. Nikisema hivyo nina maana hapo awali hapakuwa na Mtanzania aliyewahi kwenda kuishi huko na kufundisha aerobics.
KAMA UONAVVYO KATIKA PICHA NI MSWAHILI PEKEE.

KAMA UONAVVYO KATIKA PICHA NI MSWAHILI PEKEE.Dulla alianza kufundisha pale Dubai, halafu alichukuliwa na shirika ndege la Etihad na kwenda kuishi Abudhabi, pale alifanya kazi yake kwa mkataba baada ya kumaliza huko sasa ameajiriwa na chuo cha jeshi la huko anafundisha mazoezi ya aerobics huko.
Mwalimu Dulla ni kijana mwenye bidii na upendo na pia hupenda kushirikiana na waalimu wenzake japo ni kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Kwa keli najivunia kijana huyu kwa mafanyikio yake ambayo yana zaa matunda. Alipokuwa kwenye mafunzo alikuwa ni msikilivu na mwelewa ndio maana amefanikiwa katika mambo yake ya kikazi huko ughaibuni.
Mwalimu Dulla ameshawatafutia wabongo wenzake kazi huko Dubai na bado ana bidii ya kupeleka wengine zaidi, hii ni kwa ajili ya bidii yake ya kujituma ndio akaaminiwa na kuleta sifa kwa waalimu wa aerobics Tanzania.
Mwaka jana nilifika Abudhabi huko nikapata hizo sifa zote kwa kujituma kazini na hupenda kujiendeleza kwa kusomea zaidi. mie nampa big up nikiwa kama mwalimu wake wa kwanza.
Thursday, May 13, 2010
TANZANED FITNESS CENTRE(gymkhana club)
Mazoezi ya mapaja
kwa kutumia mashine iitwayo Leg extention
namna ya kuanza na kumalizia.
namna ya kuanza na kumalizia.
MAZOEZI YA KUJENGA MISULI KATIKA GYM YA TANZANED FITNESS CENTRE
ILIYOPO JIJINI DAR ES SALAAM. PICHA NI MWALIMU SWAI AKIFANYA MAZOEZI YA MISULI YA MIKONO KWA KUTUMIA MASHINE INAYOITWA BICEPS CURL
Watu wengi siku hizi hupendelea sana kufanya mazoezi ya kujenga misuli, hii ni kwa sababu kumfanya aonekane amejazia na kupendeza wakati anapovaa nguo zake. Halikadhalika kwa ajili ya afya yake.
Wengine hufanya mazoezi haya kwa kupunguza mafuta kwenye mwili, kama vile wanawake ambao wamejikuta wana mikono minene kuliko miili yao hufanya mazoezi haya kwa ajili ya kuondoa mafuta na kujenga misuli, lakini kwa mwana mke siyo rahisi kujenga misuli ikaonekana kama mwanaume, kwa sababu mwanamke hana homon zinazofanana na za kiume.
Lakini usijisahau ukafanya mazoezi ya juu tu pia kuna mazoezi ya miguu kama picha inavyoonyesha hapo juu
Hivyo basi anza leo mazoezi ili nawe uonekane umependeza kama wale ambao waliokwisha jiunga kenye gym za mazoezi haya.
Tuesday, May 11, 2010
BONANZA LA AEROBICS NA MICHEZO
MAZOEZI YA AEROBICS HIGH IMPACT
Monday, May 10, 2010
MAZOEZI YA TUMBO NA OMAR SWAI

MAZOEZI YA TUMBO KATIKA PICHA NA O. SWAI.
Mazoezi ya kuondoa tumbo huchukua muda kwa sababu ukumbuke tumbo halikuja siku moja ila lilichukua muda mpaka ukashituka limekuwa kubwa.
Wakati wa kulitoa ndio unaona sasa ni matatizo na kuchukua hata miezi miwili au mitatu, ndio uone linaanza kupungua tena kwa taratibu. Hii ni kwa sababu umejenga mafuta mengi tumboni kwa muda mrefu.
Unachotakiwa kufanya ni mazoezi ya kila siku ili uondoe hilo tumbo ambalo hukunyima raha wakati wote.
Kwa kweli ukiwa na tumbo kubwa hupendezi hata ukivaa nguo nzuri utaonekana hujapendeza.
Kama una tatizo hilo anza leo mazoezi ya tumbo na kupunguza mlo unaokula.Kila kitu yataka moyo .
Saturday, May 8, 2010
MWALIMU SWAI AKIWA NA DARASA LA MAZOEZI YA STEP AEROBICS UDSM
Mara nyingi ukuiwa unaanza mazoezi haya utasema ni mazingaumbwe, kwa sababu utakuwa huelewi wanafanya vipi lakini ukelewa kufanya, huwa unachanganyikiwa muda wa mazoezi ukufika hujahudhuria darasa la mwalimu Swai. Ni mazoezi yanayopunguza mafuta kwenye mwili na uzito kwa haraka sana. Pia unakuwa mchangamufu siku zote za maisha yako.
Musa Kisoky Mwanamazoezi wa siku nyingi


Musa Kisoky mkurugenzi wa Sofia Record akiwa katika mazoezi ya kujenga misuli katika gym ya Kilimaniaro DSM.
Musa Kisoki siyo jina jipya kwa wale wadau wa michezo hata burudani katika jiji la Dar es salaam hata nje ya Dar.
Brother Kisoky ni mwana mazoezi wa kweli sababu yeye amekuwa ni mtu wa mazoezi maishani mwake kwa kuwa yeye ni miraba minne.
Tokea miaka ya nyuma yuko mstari wa mbele haswa kwenye mazoezi ya aerobics, na ni mtu anayejichanganya na kila rika na nilipokutana nae siku hiyo alinambia kuwa siri ya kuonekana kijana kila siku ni kufanya mazoezi katika maisha yako ya kawaida kama vile unavyokula chakula na kukitumia ipasavyo kwa kufanya mazoezi.
Alisema kwamba mambo ya kuugua mara kwa mara kwake yeye hayapo, pia alisisitiza kila mtu afanye mazoezi kwa afya ili kuondoa uzee na kurefusha maisha.
Friday, May 7, 2010
MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO KWA KUTUMIA BODI


Mkurugenzi wa BIGY RESPECT akifanya mazoezi ya tumbo na mwalimu Swai akimsimamia picha hapo juu.
MAZOEZI YA TUMBO
Kwa kusema kweli kila kitu inabidi mtu ujitahidi,maana mazoezi ya tumbo unatakiwa ufanye mengi ya kutosha kama kuhesabu ifike angalau mara 300 hapo utakuwa umeafanya kidogo.
Maana msuli wa tumbo huchukua muda kujengeka na kuondoa mafuta, hivyo kihaswa unatakuwa uende kama hesabu ya 600.
Wakati una matatizo ya kuwa na tumbo kubwa unatakiwa kufanya mazoezi haya ya tumbo kila siku, kuizingatia kupunguza vitu vya mafuta.
Kumbuka ukizingatia haya utafanikiwa.Pia usisiste kuniuliza maswali kupitia tofuti hii.
MAZOEZI YA MWILI KWA KUTUMIA MASHINE
Wednesday, May 5, 2010
MAZOEZI YA KUNYOOSHA VIUNGO BAADA YA ZOEZI NA MWALIMU SWAI
Tuesday, May 4, 2010
Monday, May 3, 2010
MAZOEZI YA AEROBICS UKIWA NYUMBANI KWA AFYA YAKO.
KWANZA HAKIKISHA SEHEMU AMBAYO UNAYOFANYIA MAZOEZI YAKO KWA SIKU HIYO IWE NI HATUA NNE KUELEKEA UPANDE NA HATUA NNE NYUMA.
- UNAANZA NA KUPASHA MOTO MWILI WAKO UWE KAMA UNAKIMBIA LAKINI UMESIMAMA UNARUKA SEHEMU MOJA TU. KWA MUDA WA DAKIKA KUMI NDIPO UTASIKIA UMEPASHA MWILI MOTO VYA KUTOSHA.
BAADA YA HAPO UNASIMAMA SEHEMU MOJA NA MIGUU YAKO UKIWA UMEPANUA NA KUNYANYUA MIKONO YAKO YOTE MIWILI JUU, NA KUANZA KUKUNJA KUGUSA MABEGA YAKO NA KUNYOOSHA NA HUKU PIA UKIENDA SAMBAMBA NA MIGUU KAMA UNACHUCHUMAA NA KUNYANYUKA JUU KUFUATA MIKONO YAKO.
(unafanya hivyo mara kumi na kurudia hivyo kwa hesabu hiyo mara tatu 10x3=30)
HALAFU UNASHIKA KIUNO NA KUKUCHUMAA NA KUINUKA 10x3=30
BAADA YA HAPO UNANYANYUA MIGUU YAKO JUU KWA KUPOKEZANA KULIA KUSHOTO HADI UNAFIKIA IDADI YA HESABU KAMA YA KWANZA YAANI 10x3=30
KWA WALE AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA MAZOEZI HAYA ITAKUWA IMECHUKUA
MUDA WA DAKIKA 20 TUKIANZA NA HII UTAKUWA UMESHATOKWA NA JASHO NA KUJISIKIA UMEFANYA MAZOEZI.
USISAHU KUMALIZIA NA UNYOOSHA MWILI UKIWA UMELALA CHALI HUKU UKIPUMZIKA.
HEBU JARIBU HIVYO PINDI UTOKAPO KAZINI AU UNAPOAMKA ASUBUHI. UKIPENDA UTAFANYA ASUBUHI NA JIONI.
MWISHO WA ZOEZI LA KWANZA.
- UNAANZA NA KUPASHA MOTO MWILI WAKO UWE KAMA UNAKIMBIA LAKINI UMESIMAMA UNARUKA SEHEMU MOJA TU. KWA MUDA WA DAKIKA KUMI NDIPO UTASIKIA UMEPASHA MWILI MOTO VYA KUTOSHA.
BAADA YA HAPO UNASIMAMA SEHEMU MOJA NA MIGUU YAKO UKIWA UMEPANUA NA KUNYANYUA MIKONO YAKO YOTE MIWILI JUU, NA KUANZA KUKUNJA KUGUSA MABEGA YAKO NA KUNYOOSHA NA HUKU PIA UKIENDA SAMBAMBA NA MIGUU KAMA UNACHUCHUMAA NA KUNYANYUKA JUU KUFUATA MIKONO YAKO.
(unafanya hivyo mara kumi na kurudia hivyo kwa hesabu hiyo mara tatu 10x3=30)
HALAFU UNASHIKA KIUNO NA KUKUCHUMAA NA KUINUKA 10x3=30
BAADA YA HAPO UNANYANYUA MIGUU YAKO JUU KWA KUPOKEZANA KULIA KUSHOTO HADI UNAFIKIA IDADI YA HESABU KAMA YA KWANZA YAANI 10x3=30
KWA WALE AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA MAZOEZI HAYA ITAKUWA IMECHUKUA
MUDA WA DAKIKA 20 TUKIANZA NA HII UTAKUWA UMESHATOKWA NA JASHO NA KUJISIKIA UMEFANYA MAZOEZI.
USISAHU KUMALIZIA NA UNYOOSHA MWILI UKIWA UMELALA CHALI HUKU UKIPUMZIKA.
HEBU JARIBU HIVYO PINDI UTOKAPO KAZINI AU UNAPOAMKA ASUBUHI. UKIPENDA UTAFANYA ASUBUHI NA JIONI.
MWISHO WA ZOEZI LA KWANZA.
Saturday, May 1, 2010
MAZOEZI YA STEP AEROBICS
WANA MAZOEZI CHUO KIKUU MLIMANI(UDSM)
MAZOEZI YA AEROBIC BALL
Subscribe to:
Posts (Atom)



























