Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, April 12, 2013

KOZI YA AEROBICS INAYOFANYIKA CHUO KIKUU MLIMANI YAFANA SANA MWAKA HUU 2013


Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa  Chuo Kikuu Mlimani(School of  Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball  na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.

Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.

Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu  wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo  kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa  ni pamoja na Aerobics and Fitness.





              Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka  China ambao wako na furaha.

 


                 Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.




                         Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.



       Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)




  Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.





Kila mwanafunzi  hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema









No comments: