Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Thursday, November 27, 2014

MAMBO MUHIMU KWA ANAYEFANYA MAZOEZI YA KUJENGA MISULI(BODY BUILDING)


(Body building) Mjenga misuli ni muhimu sana awe na mwenzake wa kumsimamia wakati akiwa anafanya mazoezi(msaidizi) hii inasaidia kumlinda asije umia kwa uzito anaobeba kumshinda kunyanyua na kumrudia shingoni hii ni hatari inaweza kusababisha kupoteza maisha pao hapo.

Hii pia humsaidia yule mwana mazoezi kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito mkubwa akitegemea kuwa na msaidizi nyuma yake na kumsaidia kunyanyu hadi kufikia lengo lake, na kumpa moyo mnyanyuaji uzito.











               Mazoezi ya boby building hutegemea sana uwe na mtu wa kukusaidia
                hii hapa ni namna unavyoanza.










                  Jinsi ya kumalizia kwa kunyanyua uzito huku kukiwa na mwangalizi












                     Hapa inabidi kusaidia wakati uonapo inamshinda  ili kumwezesha
                      mwana mazoezi mwenzako.




   


















               





















Friday, November 21, 2014

AINA YA MAZOEZI YA KUONDOA MAFUTA NA KUJENGA MISULI YA TUMBO UKIWA NYUMBANI.

Mazoezi ya kuondoa  tumbo kama usemi unaotumika ni zoezi ambalo unatakiwa kuwa na moyo wa kufanya zoezi hilo na kupania kiukweli kwa kuwa na ari ikiwa inafuatiwa  na shauku kubwa ya kujenga misuli yake (six pax).
Yafuatayo ni baadhi ya mazoezi ambayo unashauriwa kuyafanya marakwa mara na kila siku katika picha.

Ikiwa kila zoezi unalofanya unatakiwa uwe na uwezo wa kufanya mara mia sita kwa mpangilio utakao jipangia mwenyewe.



                                Mazoezi haya aina tatu ni namna unavyoanza na kumalizia
                                 unapeleka mikono kama unakata panga



                               Aina ya pili ya mazoezi  inayojulikana kama side cranch
                          ikionysha unavyoanza na kumalizia unafanya mara hamsini
                          bila ya kupumzika.





                                   Zoezi hili pia ni la tumbo iukitumia mpira maalum kwa
                          kuunyanyuka nao na kurudi chini kama picha zinavyoonyesha

Thursday, November 20, 2014

MWALIMU SHWAHIBU (ANDUNJE) ALIYEBOBEA KATIKA KUFUNDISHA MAZOEZI YA AEROBICS.


Bila shaka nikimzungumzia mwalimu Andunje kwa wakazi wale wa Dar es salaam sio jina geni hususan kwa wale wanaofanya mazoezi ya aerobics kwenye club mbalimbali hapa jijini.
Mwalimu Andunje alianza kufanyisha mazoezi katika ukumbi wa vijana pale mango garden na baadae alijiendeleza alipokuwa  Kelken gym iliyopo chan'gombe na nyerere road.
Hapo alikutana na mkongwe wa mazoezi ya aerobic ambaye hivi sasa anafundisha  chuo kikuu mlimani na kufuzu.


                  Mwalimu Shwahibu  aliye maahiri  katika mzoezi ya aerobics
                  na pia hutegemea sana kwa kumuingizia kipato.

                        Hapo akionyesha mazoezi ya kunyoosha viungo kwenye
                        gym ya UDSM.


                             Mwalimu Andunje akiwa kwenye darasa lake akionyesha
                              mazoezi na kufuatilia kwa makini