Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Thursday, November 29, 2012

FAIDA YA KUFANYA MAZOEZI YA AEROBICS KWA WALE WENYE KIFUA CHA PUMU.

Leo nimeona umuhimu wa kuzungumzia kuhusu wale ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa kifua cha pumu.
Mazoezi ni muhimu sana haswa  kwa wale ambao wanasumbuliwa na kifua cha pumu, hii nimesemea kwa sababu kuna watu ambao husumbuliwa na pumu muda mrefu maana wengine huzaliwa nayo hata pia kwa wale wnaosumbuliwa na maradhi ya kisukari mazoezi  huwasaidia sana katika kuugua mara kwa mara.
Kwa uthibitisho wa utafiti wangu nimeona wengi waliofanya mazoezi hupata nafuu ya hali ya juu na kupunguza matumizi ya dawa za pumu kwa sababu mazoezi humsaidia kumuwezesha kupumua na kufanaya mapafu yake kufanaya kazi ipasavyo. Hivyo nawashauri wale wenye matatizo haya kujiunga  na club za mazoezi na kufanya mazoezi ya Aerobics yatasaidia kama kupunguza na kutibika kabisa.


                     Mazoezi  ya kutembea  au kukimbia kwa kutumia mashine ya treadmill


                  Mazoezi ya aerobics ambayo pia ni njia muhimu katika kukusaidia kupunguza
                       na kutibu ugonjwa wa kifua cha pumu.

Tuesday, November 20, 2012

WAFANYA KAZI WA VETA(DSMRVTSC) WAFUNGUA CLUB YA MAZOEZI HAPO VETA KWA WAFANYAKAZI WOTE.


 Katika mazungumzo na wakuu wa hapo DSMRVTSC VETA walisema wameamua kuanzisha club yao ya mazoezi hii ni kutokana na kutokuwa na muda wa kufanya mazoezi siku za wiki na kuamua kufanya mazoezi angalau siku ya Jumamosi na jumapili hapo baadae.Kwa sasa wanafanya mazoezi kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa moja.






Wanamazoezi wa  Veta wakifanya mazoezi ya viungo kwenye  gym yao wakiwa na mwalimu  O.Swai



Hapa ni mkuu wa chuo hicho Samwel Ng'andu  akiongoza wafanyakazi wenzake katika  zoezi kila asubuhi ya Jumamosi alifungua rasmi.



                                      Mazoezi yakiwa yamepamba moto katika club hiyo Veta


                                 Mwalimu Swai akirekebisha wana mazoezi na kuwapa moyo












Friday, November 16, 2012

MAZOEZI YA KUJENGA MAPAJA KWA KUTUMIA BARBELL(free weight)

                                                                                                     

Mara nyingi wanamazoezi wa kujenga misuli husahau kufanya mazoezi ya kujenga misuli ya miguu, hii ni tatizo haswa kwa wale ambao wanaanza zoezi hili la kujenga misuli.
Nikisema hivyo nina maana wao huanza kujenga sehemu ya mikono na kifua ikiwa sehemu hiyo inaonekana aidha kwa kuvaa tisheti lakini  hii ikiwa ni staili ya vijana.
Kumbuka mazoezi ya miguu ni uhimu sana kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga misuli ili uonekane nadhifu zaidi





                                           Hapa katika picha inaonyesha  kijana Jonathan
                                              akianza zoezi la kujenga miguu kwenye gym ya
                                                Chuo  Kikuu cha Mlimani UDSM.





                                            Hapa Jonathan akimaliza zoezi hilo kwa hesabu
                                               ya 10x4 na kuongeza uzito kila seti. 


Wednesday, November 7, 2012

MAZOEZI YA KUJENGA SEHEMU YA MSULI WA NYUMA WA MKONO(TRICEPS)


Ukiwa unafanya mazoezi ya triceps kwa kutumia cable mashine mara nyingi huwa ni mazoezi ambayo yana matokeo mazuri na uhakika.
Mazoezi haya unafanya kwa marudio ya seti 4 x 12 na unapoongeza uzito ndipo unapo punguza hesabu ya kufanya.





                                    Mwalimu wa mazoezi  akionyesha  namna ya kuanza zoezi hilo




                                    Mwalimu Swai akionyesha jinsi ya kumalizia zoezi la triceps