Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, May 8, 2010

Musa Kisoky Mwanamazoezi wa siku nyingi













Musa Kisoky mkurugenzi wa Sofia Record akiwa katika mazoezi ya kujenga misuli katika gym ya Kilimaniaro DSM.

Musa Kisoki siyo jina jipya kwa wale wadau wa michezo hata burudani katika jiji la Dar es salaam hata nje ya Dar.


Brother Kisoky ni mwana mazoezi wa kweli sababu yeye amekuwa ni mtu wa mazoezi maishani mwake kwa kuwa yeye ni miraba minne.

Tokea miaka ya nyuma yuko mstari wa mbele haswa kwenye mazoezi ya aerobics, na ni mtu anayejichanganya na kila rika na nilipokutana nae siku hiyo alinambia kuwa siri ya kuonekana kijana kila siku ni kufanya mazoezi katika maisha yako ya kawaida kama vile unavyokula chakula na kukitumia ipasavyo kwa kufanya mazoezi.

Alisema kwamba mambo ya kuugua mara kwa mara kwake yeye hayapo, pia alisisitiza kila mtu afanye mazoezi kwa afya ili kuondoa uzee na kurefusha maisha.















No comments: