OK BODY SHAPE
Hii ni blog mahususi kwa mazoezi ya viungo ambayo ni muhimu kwa afya zetu
Friday, May 24, 2019
Friday, February 2, 2018
MAZOEZI MBALI MBALI BAADA YA UKARABATI UDSM GYM
Baada ya ukarabati mubwa wa gym hall ya udsm mazoezi yameanza kama kawaida.
Mara nyingi nasisitiza mazoezi ni muhimu kwa kila mtu ambaye anauwezo huo wa kufanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki ili kuondoa mafuta yalozidia mwilini mwako ambayo husababisha maradhi usotarajia.
Mashine ya kukimbilia treadmillMazoezi ya miguu unavyoanza na kumaliza
Step cardio ya style mbalimbali
Mazoezi mbali mbali yakiwemo kukimbia na Aerobics
Wednesday, December 13, 2017
UMUHIMU WA KUNYWA MAJI WAKATI WA MAZOEZI NA MWISHO WA MAZOEZI
Maji ni muhimu sana pindi ufanyapo mazoezi na baada ya mazoezi kwa sababu ya kupooza joto la mwili wako na kurudisha katika joto lako la kawaida.Nikisemea hivyo wako watu wengi wanaogopa kunywa maji wakati wanapofanya mazoezi, kwa kuzingatia hivyo maji yenyewe yawe baridi na sio ya moto. Kwa hiyo pasenti 60 ya mwili wako ni maji. Pia unatakiwa kunywa maji yasiyopungua lita mbili kwa siku.
Tuesday, October 10, 2017
MAZOEZI MBALIMBALI YA KUONDOA TUMBO
Mara nyingi tatizo la tumbo huwa ni changamoto kubwa kwa watu wengi kukimbilia kufanya mazoezi ili kuondoa hilo tatizo la kuwa na tumbo kumbwa.
Hapa nakupatia namna ya kufanya zoezi ukiwa nyumbani au sehemu yoyote utaweza kufanya haya mazoezi.
Mazoezi ya tumbo namna inavyoanza na kumalizi
unanyoosha mikono nyuma kichwa chini na
ukinnyanyuka unagusa magoti ulokunja
Hili zoezi linalingana kama la kwanza lakini unakuwa
umenyoosha mguu na mikono ukinyanyuka unagusa goti.
Zoezi hili linaonyesha unavyoanza na kumalizia
Zoezi la upande wa mbavu picha zikionyesha namna ya
kufanya zoezi hilo
Wednesday, August 2, 2017
NINI MAANA YA DAYATI NA FAIDA ZAKE KWA ANAYEFANYA NA ASIYEFANYA MAZOEZI
Mara nyingi watu hudhani kuwa kufanya dayati ni kutokula kabisa, la hasha hizo ni fikra potofu kwa mwana mazoezi ambazo zimerithiwa na wale ambao hawajui namna au maana ya dayati, Dayati maana yake ni kubadili mfumo wako wa kula kula bila ya mpangilio.
Kubadilisha tabia ya kula bila mpangilio na kula kiasi kidogo cha chakula haswa wakati wa usiku ili kuepuka uzito maana nyakati za usiku unakuwa hufanyi shughuli yoyote ile ya kutumia chakula ambacho ulichokula kwa usiku ule hivyo basi kile chakula hubadililika na kuwa mafuta na kwenda kujikusanya sehemu mbalimbali ya mwili wako. Kwa wale ambao hawafanyi mazoezi hupata shida ya kuongezeka uzito mara kwa mara.Kama unataka kupungua uzito punguza chakula unachokula na kula mboga za majani kwa wingi na mtunda kwa ajiliya kuepuka vyakula venye mafuta mengi. Fanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki.
MAZOEZI AINA MBALI MBALI KWA KUJIWEKA NA AFYA NZURI YA MWILI WAKO
Mazoezi ya tumbo kuondoa mfutaZoezi la kunyoosha misuli ya mgongo
Kufanya mazoezi ya Aerobics kwa ajili ya kupunguza uzito
Mazoezi ya kutengeneza misuli yako na kuonekana nadhifu
Wednesday, May 24, 2017
MAZOEZI YA KICK BOXING NAMNA YA KUFANYA
Kuna aina nyingi ya mazoezi kwa ajili ya kukufanya uwe na afya bora na kukupa nguvu mwili wote. Mazoezi haya ya kick boxing ni mazoezi ya kutumia nguvu zako wakati wote ukiwa unafanya mazoezi haya.
Pia hukufanya uwe na nguvu zisizoishia pamoja na pumzi yako.
Mwalimu Swai akionyesha wanamazoezi hilo
zoezi la kick boxing namna ya kuanza kwa
kurusha jab kama picha inavyo hapo juu
Wana mazoezi wakifuatilia na kufanya zoezi
Mwalimu Swai akipita na kuwarekebisha wana
mazoezi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam
Mwalimu akionyesha namna ya kupiga jap moja ya zoezi
Zoezi likiwa linaendelea ni la upper cut ambalo
husaidia kuwa na nguvu ya mikono
Saturday, April 8, 2017
KOZI YA WAALIMU WA AEROIBICS YAANZA CHUO KIKUU UDSM 2017
Wanafunzi wa mwaka wa tatu wakiwa katika mafunzo ya awali
ya aerobics
Wanafunzi wakifurahia mafunzo ya awali ya kozi ya aerobics
Mkufunzi O.Swai(akiwa kulia mwenye kapero nyeusi)katika
picha ya pamoja na wanafunzi wake wa aerobics 2017.
ya aerobics
Wanafunzi wakifurahia mafunzo ya awali ya kozi ya aerobics
Mkufunzi O.Swai(akiwa kulia mwenye kapero nyeusi)katika
picha ya pamoja na wanafunzi wake wa aerobics 2017.
Saturday, February 25, 2017
MAZOEZI TOFAUTI YA KISAIDIA SANA KUFANYA UKIWA NYUMBANI PEKE YAKO
Mazoezi ya tumbo huwa ni muhimu sana kufanya katika maisha ya kila siku, hii ikiwa na maana unakula chakula kila siku na ni muhimu kutumia chakula ulacho kwa kufanya mazoezi.
Jinsi unavyomaliza mazoezi ya tumbo kwa kuinuka
upande mmoja hadi mwingine kushika sakafu kama
picha zinavyoonyesha hakikisha unakaza tumbo pindi
ufanyapo zoezi hilo.
Zoezi la mgongo jinsi unavyoanza kwa mbele
Zoezi la mgongo kwa upande ukiwa unanyoosha mkono
na mguu mmoja ukiwa kwenye floor. kama picha ilivyo
Thursday, January 19, 2017
MAZOEZI BAADA YA MAPUMZIKO YA MWISHO WA MWAKA
Baada ya mapumziko na kuingia mwaka mpya leo nakuletea mazoezi mchanganyiko baad ya mapumziko kama picha tofauti zikionyesha mazoezi mbali mbali
Karibuni tena katika mazoezi yetu kama kawaida
Thursday, December 29, 2016
MAPUMZIKO YA KUFANYA MAZOEZI NI JAMBO LA MUHIMU
Kuna umuhimu wa kuwa na muda wa mapumziko ya kutosha katika kufanya mazoezi, hii ikiwa ni kipindi cha mwisho wa mwaka.
Sababu za kupumzika ni kuipa misuli ya mwili kujipanga vizuri na kukuwa. Pia hii husaidia kuuondoa maumivu mwilini na kusaidia mwili kujipanga na kupungua.
Sababu ingine nikukufanya uwe na hamu ya kurudi mazoezini baada ya mapumziko ya muda wa wiki mbili. Pia husaidia kujua mwili wako ulivyo kubali kupungua au kujengeka kimazoezi.
JAMBO LA MUHIMU NI KUJITAMBUA UNATAKA NINI UNAPOAMUA KUFANYA MAZOEZI AMBAYO HUENDA SAMBAMBA NA MPANGILIO WA CHAKULA.
Thursday, November 24, 2016
MLO WA SIKU NI KIFUNGUA KINYWA (A MEAL OF A DAY IS BREAKFAST)
Kwa nini nazungunzia Mlo wa siku ni kifungua kinywa' Nikimaanisha kwa wale ambao wanahitaji kujenga miili yao hawana budi kupata chai nzito ikiwa imeshehena matunda,protini ikiwa ni kama nyama kiasi cha nusu kilo asubuhi hii ni kwa ajili ya wale wenye kujenga misuli kwani wanahitaji protini ya kutosha kwa ajili ya kupata virutubisho vya kujenaga misuli.
Halikadhalika awe anapata miilo zaidi ya mitatu nikimaanisha mara tano kwa siku awe anakula .Kila baada ya zoezi unatakiwa kupata aina ya chakula cha wanga, hii ikiwa ni mahitaji ya mjenga misuli anahitajika kula kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kurudishia viambatanino vilivyotumika wakati wa mazoezi.
Mwili uliojengwa kwa mazoezi na kula ipasavyo.(Body Builder)
Wednesday, October 12, 2016
MAZOEZI YA KUJENGA MKONO BICEPS CURL KWA KUTUMIA CABLE MACHINE
Kuna aina nyingi za kufanya mazoezi ya kujenga mikono kwa wakati mwingine unafanya kwa kutumia free weight, kama vile dumbell au barbell.
Kwa leo tunaanza na mazoezi ya mkono kwa kutumia cable mashine namna unavyoanza na kumaliza.Mazoezi haya unafanya seti tatu kwa hesabu ya kumi na tano kila mkono
kumalizia kama picha zikionyesha juu na chini
Baada ya kubadilisha mkono wako nakufanya
zoezi hilo hilo la biceps curl seti 4x15..
Tuesday, September 13, 2016
MAZOEZI AMBAYO WAWEZAFANYA HATA UKIWA NYUMBANI HASWA KAMA HUJAWAHI KUFANYA MAZOEZI
Mara nyingi watu hufikiria kuanza kufanya mazoezi pindi akiwa na tatizo la uzito au daktari kamshauri aanze kufanya mazoezi.
Mimi nashauri isifikie hapo maana mazoezi ni jambo la muhimu mtu yeyote yule anayekula vizuri na pia ni dawa, hukufanya kuwa mchangamfu wakati wote wa maisha yako.
kama unaruka ukirudi chini unakunja goti lako na
unafanya kwa sekunde 30 halafu unabadili miguu.
Zoezi la jumping lunge kumalizia mguu mwingine
Picha hizi mbili zikionyesha namna ya kufanya zoezi la tumbo
ukiwa umesimama kwa kuanza mguu wako nyuma na kupandisha
juu huku goti lako limejikunja na mikono yako kwenda nyuma
kama picha ya juu ikionyesha unavyoanza na ya chini ukimaliza
unafanya kwa muda wa sekunde 45 halafu unapumzika na kurudia
tena.
Zoezi hili linaitwa Side bridge ukiwa umelala upande na
kunyanyuka juu kwa kutumia mkono mmoja unakaa kwa
sekunde 30 kama picha inavyoonyesha na kubadilisha upande
mwingine
Monday, August 8, 2016
AINA YA MAZOEZI YA TUMBO NA FAIDA ZAKE KWA MUDA WA DAKIKA 20 TU.
Yapo aina mbalimbali ya mazoezi ya kuondoa tumbo ambalo limekuwa likisumbua kutopungua.
Yafuatayo ni aina mbalimbali ya mazoezi ambayo yanasaidia kwa kufanya kwa muda wa dakika 20 tu.
Zoezi la Bicycle crunh ambalo unafanya kwa muda
wa sekunde 60 kama zoezi linavyoonyesha hapo juu,
Zezi hili la Glute bridge leg rise unafanya zoezi hili kwa sekunde
30 na kubadili mguu mwingine kwa muda huo.
Zoezi hili linaitwa Dorsal rise unafanya kwa muda wa
sekunde30 halafu unapumzika kwa sekunde15 na kuanza tena,
Subscribe to:
Posts (Atom)