Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, May 26, 2010

MAZOEZI YAKUFANYA UWAPO NYUMBANI AU SAFARINI NA MWALIMU SWAI

PICHA ZINAONYESHA MAZOEZI YATUMBO KUANZIA MWANZO HADI MWISHO WA ZOEZI .


Kwanza kabisa unakunja mguu wako mmoja juu ya mwaingine na unahakikisha mgongo wako umegusa kwenye sakafu unayofanyia kama picha inavyoonyesha.
Halafu unanyanyua kichwa mabega na mguu mmoja na kurudi chini pamoja kwa kuhesabu mara kumi na kurudia hivyo hadi ishirini na kupumzika muda wa sekunde sitini, huku umekumbatia miguu yako kwa kuondoa maumivu ya misuli ya tumbo.
Unarudia tena hadi kufikia idadi ya mara miamoja. Hiki ni kiwango cha mwanzo kabisa kwa wale wanoanza mazoezi haya kwa mara ya kwanza kabisa.
Ukiwa ni mzoefu katika mazoezi ufanye mara nyingi zaidi hata kufikia mia tatu au mia nnne, kwa hesabu ya hamsini ndio upumzike. Kwa sababu mazoezi ya kupunguza yanahitaji uwe makini na mvumilivu





No comments: