KWANZA HAKIKISHA SEHEMU AMBAYO UNAYOFANYIA MAZOEZI YAKO KWA SIKU HIYO IWE NI HATUA NNE KUELEKEA UPANDE NA HATUA NNE NYUMA.
- UNAANZA NA KUPASHA MOTO MWILI WAKO UWE KAMA UNAKIMBIA LAKINI UMESIMAMA UNARUKA SEHEMU MOJA TU. KWA MUDA WA DAKIKA KUMI NDIPO UTASIKIA UMEPASHA MWILI MOTO VYA KUTOSHA.
BAADA YA HAPO UNASIMAMA SEHEMU MOJA NA MIGUU YAKO UKIWA UMEPANUA NA KUNYANYUA MIKONO YAKO YOTE MIWILI JUU, NA KUANZA KUKUNJA KUGUSA MABEGA YAKO NA KUNYOOSHA NA HUKU PIA UKIENDA SAMBAMBA NA MIGUU KAMA UNACHUCHUMAA NA KUNYANYUKA JUU KUFUATA MIKONO YAKO.
(unafanya hivyo mara kumi na kurudia hivyo kwa hesabu hiyo mara tatu 10x3=30)
HALAFU UNASHIKA KIUNO NA KUKUCHUMAA NA KUINUKA 10x3=30
BAADA YA HAPO UNANYANYUA MIGUU YAKO JUU KWA KUPOKEZANA KULIA KUSHOTO HADI UNAFIKIA IDADI YA HESABU KAMA YA KWANZA YAANI 10x3=30
KWA WALE AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA MAZOEZI HAYA ITAKUWA IMECHUKUA
MUDA WA DAKIKA 20 TUKIANZA NA HII UTAKUWA UMESHATOKWA NA JASHO NA KUJISIKIA UMEFANYA MAZOEZI.
USISAHU KUMALIZIA NA UNYOOSHA MWILI UKIWA UMELALA CHALI HUKU UKIPUMZIKA.
HEBU JARIBU HIVYO PINDI UTOKAPO KAZINI AU UNAPOAMKA ASUBUHI. UKIPENDA UTAFANYA ASUBUHI NA JIONI.
MWISHO WA ZOEZI LA KWANZA.
No comments:
Post a Comment