KAMA PICHA ZINAVYO ONYESHA UNATUMIA MIKONO YAKO YOTE MIWILI KUGUSA CHINI NA KUGUKIA UPANDE WA KULIA NA KUSHOTO HII HUSAIDIA KUONDOA MAFUTA YALIYO PEMBENI MWA MBAVU WENGINE HUITA SPEA TAIRI. UNAFANYA HIVYO MARA KUMI KILA PEMBE.
Thursday, May 27, 2010
MAZOEZI YA KUPUNGUZA MAPAJA NA KUKUWEKA KUWA NA NYONGA KUWA MADHUBUTI
MAZOEZI YA KUPUNGUZA KITAMBI MWALIMU SWAI AKIONYESHA
MAZOEZI YA TUMBO KAMA PICHA ZINAVYO ONYESHA
Picha mbili za chini zikionyesha jinsi ya kuanza na kumalizia zoezi la tumbo.
Picha mbili za chini zikionyesha jinsi ya kuanza na kumalizia zoezi la tumbo.
HAPA NI MAZOEZI YA TUMBO UKIWA UMENYOOSHA MIKONO YOTE MIWILI UNANYANYUA MABEGA NA MGONGO NA KURUDI KWA KUHESABU HADI KUMI NA UNARUDIA HIVYO MARA TANO YAANI 10x5=50 UNAFANYA HIVYO ASUBUHI NA JIONI NI MAZOEZI TOSHA KWA TUMBO KAMA UKIYAFANYA KILA SIKU.
Wednesday, May 26, 2010
MAZOEZI YAKUFANYA UWAPO NYUMBANI AU SAFARINI NA MWALIMU SWAI
PICHA ZINAONYESHA MAZOEZI YATUMBO KUANZIA MWANZO HADI MWISHO WA ZOEZI .
Kwanza kabisa unakunja mguu wako mmoja juu ya mwaingine na unahakikisha mgongo wako umegusa kwenye sakafu unayofanyia kama picha inavyoonyesha.
Halafu unanyanyua kichwa mabega na mguu mmoja na kurudi chini pamoja kwa kuhesabu mara kumi na kurudia hivyo hadi ishirini na kupumzika muda wa sekunde sitini, huku umekumbatia miguu yako kwa kuondoa maumivu ya misuli ya tumbo.
Unarudia tena hadi kufikia idadi ya mara miamoja. Hiki ni kiwango cha mwanzo kabisa kwa wale wanoanza mazoezi haya kwa mara ya kwanza kabisa.
Ukiwa ni mzoefu katika mazoezi ufanye mara nyingi zaidi hata kufikia mia tatu au mia nnne, kwa hesabu ya hamsini ndio upumzike. Kwa sababu mazoezi ya kupunguza yanahitaji uwe makini na mvumilivu
Saturday, May 22, 2010
BONAZA LA AEROBICS KATIKA PICHA NA WAALIMU WA GYM MBILIMBALI DAR.
SIYO MAMBO YA AEROBICS TU HATA JACUZI PIA HUCHANGAMSHA MWILI NA KUKUFANYA UWE MCHANGAMFU
AQUA AEROBICS
NI FURAHA TUPU KUWA PAMOJA NAMNA HII.
KATIKA BONANZA LA KILA BAADA YA MIEZI MITATU WADAU WANAFURAHIA MAZOEZI KWENYE HOTELI YA SOUTH BEACH
Siku hii huwa ni siku ya kuhadithia katika maisha yako ya kufanya mazoezi, pia hukuweka karibu na wadau wenzako.
Halikadhalika kujuana kwa ukaribu zaidi maana hapa kwenye bonanza hili huchukua takriban siku nzima maana huanza asubuhi saa nne na kumalizika jioni saa kumi na moja jioni, huwa ni muda wa kutosha kukutana na kujuana zaidi kuliko ukiwa gym unachukua muda wa saa moja tu tena ukimaliza mazoezi ni kuwahi nyumbani.
Hivyo basi bonanza la aerobics lina manufaa makubwa ndio maana wadau wameamua kulifanya kila baada ya miezi mitatu.
Mimi mwenyewe binafsi nimepania kuwaalika wadau wote wa aerobics wa kila gym hapa Dar es salaam na pia nje ya dar, kwa kutegemea wadhamini ambao niko mbioni kuwasaka.
MWALIMU WA AEROBICS WA KIKE MTANZANIA MARIA ALIYEAMINIKA KUFUNDISHA UGHAIBUNI
Mwalimu Maria amewahi kufundisha katika gym mbali mbali jijini Dar es salaam ikiwemo Genessis gym, Kel Ken gym, na Tanzaned gym hizi zote ni gym za jijini Dar.
Mimi binafsi nimefundisha nae kwenye gym moja
na hata nilikuwa namwalika katika aerobics bonanza tofauti tunazofanya.
Kwa kweli alikuwa anakubalika kwa kufundisha wadau pia alikuwa ni dada anayependa kujua mambo mengi kutoka kwangu, kitu ambacho hakijuia alipenda kukijua kwa kumuonyesha ndio maana amepata mafanyikio katika kazi hii ya ualimu wa aerobics.
Hivi sasa mwana dada huyu yuko Duabai anfanya kazi ya mwalimu wa aerobics, na anaendelea vema na kazi hiyo kwa taarifa kutoka kwa kaka yao Dulla.
Picha inaonyesha akiwa kwenye bonanza la kelken na picha ya pamoja na mwalimu Omar Swai
Friday, May 21, 2010
NI KWANINI MTU ANANENEPA BILA YA YEYE KUJUA
KWENYE PICHA HAPO JUU MDAU WA MAZOEZI AMEPANIA KUPUNGUZA UZITO NA KUWA NA MPANGILIO WA MLO.
Sisi binaadam mara nyingi huwa tunajisahau katika kula chakula bila ya mpangilio.
Haswa katika jamii ya kibongo, huwa tunajisahau pindi tuwapo nakipato kikubwa huwa tunasema ponda mali kufa kwaja.
Hii inamaana pindi upatapo ndio kipindicha kukufuru kula chochote kile na kuzidi kupimo. Hivyo unajikuta uko katika wimbi la matatizo ya moyo.
Katika utafiti wangu niloufanya muda mrefu utakuta wale wenye matatiozo ya ugonjwa wa moyo ni wengi.Hii inatokea katika jamii yetu ya waafrika ambao mwisho wa siku anapokwenda kumuona daktari hugundua maradhi hayo alopata yalitokana na kula bila mpangilio.
Hivyo nawashauri wale ambao wanamatatizo kama haya wajitahidi kufanya mazoezi na kupunguza mlo unaokula pia kula kwa mpangilio.
Monday, May 17, 2010
OK.BODY SHAPE WADAU WA CLABU HIYO MWAKA 2000 NA MWALIMU SWAI
MWALIMU SWAI(a.k.a MASTER CLASS) ENZI YA GOGO HOTEL ILIKUWA NI MAZOEZI YA HIGH IMPACT AEROBICS ENZI HIZO YA
AKINA David Mrema, Kissy,Lukumai,Rehema,
Vivian,Shami,Mtagwa Fundikira,Maria,Nara na wengineo wengi.Ikiwa imepita miaka kumi.
SWALI: JE HAWA WADAU WANAFANYA MAZOEZI YA AEROBICS?
JIBU: Ni wachache sana kwa mujibu wa utafiti wangu.
MWALIMU HENRY MANGO WA HOME GYM
Mwalimu Mango wa gym ya Home Gym siyo jina geni kwa wale wadau wa luninga ya ITV.
Kijana Henry Mango alianzisha sehemu yake ya mazoezi katika mwaka wa 2004.ambapo alifungua sehemu ya kunyanyua vyuma kwa ajili ya kujenga misuli huko mwenge Dar.
Baada ya miaka michache alianzisha sehemu ya kufanyisha mazoezi ya aerobics, ambayo anaendelea na kwa sasa ana wadau ambao wengi wao wanatokea sehemu za mwenge.
Nilipomuuliza kiwango cha elimu yake alinambia amefikia darasa la saba lakini amesema atajiendeleza zaidi kielimu, ili apate mafanikio katika kazi hii ya mwalimu wa aerobics .
WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS
WAKIONGOZWA NA MWALIMU FREDY LAUWO AMBAYE YEYE PIA AMEJULIA MAZOEZI KUTOKA KWA MWALIMU MANGO HAPO HOME GYM.
Saturday, May 15, 2010
MWALIMU WA KWANZA MTANZANIA ABDALAH KWENDA KUFUNDISHA AEROBICS DUBAI
Abdalah a.k.a DULLA ni mwalimu wa kwanza kwenda kufundisha aerobics Dubai. Nikisema hivyo nina maana hapo awali hapakuwa na Mtanzania aliyewahi kwenda kuishi huko na kufundisha aerobics.KAMA UONAVVYO KATIKA PICHA NI MSWAHILI PEKEE.
Dulla alianza kufundisha pale Dubai, halafu alichukuliwa na shirika ndege la Etihad na kwenda kuishi Abudhabi, pale alifanya kazi yake kwa mkataba baada ya kumaliza huko sasa ameajiriwa na chuo cha jeshi la huko anafundisha mazoezi ya aerobics huko.
Mwalimu Dulla ni kijana mwenye bidii na upendo na pia hupenda kushirikiana na waalimu wenzake japo ni kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Kwa keli najivunia kijana huyu kwa mafanyikio yake ambayo yana zaa matunda. Alipokuwa kwenye mafunzo alikuwa ni msikilivu na mwelewa ndio maana amefanikiwa katika mambo yake ya kikazi huko ughaibuni.
Mwalimu Dulla ameshawatafutia wabongo wenzake kazi huko Dubai na bado ana bidii ya kupeleka wengine zaidi, hii ni kwa ajili ya bidii yake ya kujituma ndio akaaminiwa na kuleta sifa kwa waalimu wa aerobics Tanzania.
Mwaka jana nilifika Abudhabi huko nikapata hizo sifa zote kwa kujituma kazini na hupenda kujiendeleza kwa kusomea zaidi. mie nampa big up nikiwa kama mwalimu wake wa kwanza.
Thursday, May 13, 2010
TANZANED FITNESS CENTRE(gymkhana club)
Mazoezi ya mapaja
kwa kutumia mashine iitwayo Leg extention
namna ya kuanza na kumalizia.
namna ya kuanza na kumalizia.
MAZOEZI YA KUJENGA MISULI KATIKA GYM YA TANZANED FITNESS CENTRE
ILIYOPO JIJINI DAR ES SALAAM. PICHA NI MWALIMU SWAI AKIFANYA MAZOEZI YA MISULI YA MIKONO KWA KUTUMIA MASHINE INAYOITWA BICEPS CURL
Watu wengi siku hizi hupendelea sana kufanya mazoezi ya kujenga misuli, hii ni kwa sababu kumfanya aonekane amejazia na kupendeza wakati anapovaa nguo zake. Halikadhalika kwa ajili ya afya yake.
Wengine hufanya mazoezi haya kwa kupunguza mafuta kwenye mwili, kama vile wanawake ambao wamejikuta wana mikono minene kuliko miili yao hufanya mazoezi haya kwa ajili ya kuondoa mafuta na kujenga misuli, lakini kwa mwana mke siyo rahisi kujenga misuli ikaonekana kama mwanaume, kwa sababu mwanamke hana homon zinazofanana na za kiume.
Lakini usijisahau ukafanya mazoezi ya juu tu pia kuna mazoezi ya miguu kama picha inavyoonyesha hapo juu
Hivyo basi anza leo mazoezi ili nawe uonekane umependeza kama wale ambao waliokwisha jiunga kenye gym za mazoezi haya.
Tuesday, May 11, 2010
BONANZA LA AEROBICS NA MICHEZO
MAZOEZI YA AEROBICS HIGH IMPACT
Monday, May 10, 2010
MAZOEZI YA TUMBO NA OMAR SWAI
MAZOEZI YA TUMBO KATIKA PICHA NA O. SWAI.
Mazoezi ya kuondoa tumbo huchukua muda kwa sababu ukumbuke tumbo halikuja siku moja ila lilichukua muda mpaka ukashituka limekuwa kubwa.
Wakati wa kulitoa ndio unaona sasa ni matatizo na kuchukua hata miezi miwili au mitatu, ndio uone linaanza kupungua tena kwa taratibu. Hii ni kwa sababu umejenga mafuta mengi tumboni kwa muda mrefu.
Unachotakiwa kufanya ni mazoezi ya kila siku ili uondoe hilo tumbo ambalo hukunyima raha wakati wote.
Kwa kweli ukiwa na tumbo kubwa hupendezi hata ukivaa nguo nzuri utaonekana hujapendeza.
Kama una tatizo hilo anza leo mazoezi ya tumbo na kupunguza mlo unaokula.Kila kitu yataka moyo .
Saturday, May 8, 2010
MWALIMU SWAI AKIWA NA DARASA LA MAZOEZI YA STEP AEROBICS UDSM
Mara nyingi ukuiwa unaanza mazoezi haya utasema ni mazingaumbwe, kwa sababu utakuwa huelewi wanafanya vipi lakini ukelewa kufanya, huwa unachanganyikiwa muda wa mazoezi ukufika hujahudhuria darasa la mwalimu Swai. Ni mazoezi yanayopunguza mafuta kwenye mwili na uzito kwa haraka sana. Pia unakuwa mchangamufu siku zote za maisha yako.
Musa Kisoky Mwanamazoezi wa siku nyingi
Musa Kisoky mkurugenzi wa Sofia Record akiwa katika mazoezi ya kujenga misuli katika gym ya Kilimaniaro DSM.
Musa Kisoki siyo jina jipya kwa wale wadau wa michezo hata burudani katika jiji la Dar es salaam hata nje ya Dar.
Brother Kisoky ni mwana mazoezi wa kweli sababu yeye amekuwa ni mtu wa mazoezi maishani mwake kwa kuwa yeye ni miraba minne.
Tokea miaka ya nyuma yuko mstari wa mbele haswa kwenye mazoezi ya aerobics, na ni mtu anayejichanganya na kila rika na nilipokutana nae siku hiyo alinambia kuwa siri ya kuonekana kijana kila siku ni kufanya mazoezi katika maisha yako ya kawaida kama vile unavyokula chakula na kukitumia ipasavyo kwa kufanya mazoezi.
Alisema kwamba mambo ya kuugua mara kwa mara kwake yeye hayapo, pia alisisitiza kila mtu afanye mazoezi kwa afya ili kuondoa uzee na kurefusha maisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)