Mara nyingi kwa wale ambao wanataka kujenga misuli hawakumbuki au kuwa na uhakika wa mlo ambao anatakiwa kula.
Kwa sababu ninapata maswali mengi kuhusu aina ya chakula anatakiwa kutumia wakati afanyapo haya mazoezi ya kujenga misuli.
AINA YA VYAKULA
1.Awe anapata chakula cha wanga kwa ajili ya kuupata nguvu.(kama makaroni,chapati,ugali na wali)
2.Chakula cha protini kwa ajili yakujenga misuli kwa haraka(kama kuku,samaki,figo,na nyama)
3.Apate aina mbali mbali ya matunda.
Kula zaidi ya miilo 3 iwe mara tano na mazoezi ya kutosha kwa kuongeza uzito kila baada ya seti.
Monday, December 16, 2013
Friday, November 1, 2013
NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA MBOGA MBOGA INAYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
Hebu leo tuangalia faida ya kutumia juisi ambayo ni mchanganyiko wa matunda na mboga mboga ambayo husaidia kupunguza uzito. Juisi yenyewe inamchanganyiko wa mboga na matunda, ikiwa na virutubisho vyote vinanyohitajika mwilini.
Hii hapa ni jinsi ya kutayarisha aina ya vitu vinavyohitajika
1.Uwe na mashine ya kutengezea hiyo juisi(Juice maker)
2.Karrot
3.Matango mawili
5.Cornflower ya kijani
6.Apple 2
7.Spinach
Karoti za kutosha
Mashine ya kutengenezea juisi yenyewe pamoja na mchanganyiko wa mboga
Mboga za spinach
Muonekano ya juisi yenyewe ukisha tengeneza tayari kutumia
Hii hapa ni jinsi ya kutayarisha aina ya vitu vinavyohitajika
1.Uwe na mashine ya kutengezea hiyo juisi(Juice maker)
2.Karrot
3.Matango mawili
5.Cornflower ya kijani
6.Apple 2
7.Spinach
Karoti za kutosha
Mashine ya kutengenezea juisi yenyewe pamoja na mchanganyiko wa mboga
Mboga za spinach
Muonekano ya juisi yenyewe ukisha tengeneza tayari kutumia
Friday, October 4, 2013
MWANA MAZOEZI MHADHIRI WA CHUO KIKUU MLIMANI AWA MFANO KWA WENZAKE
Katika maisha ya siku hizi ni nadra sana kukuta mhadhiri wa chuo kikuu kupenda mazoezi na kuhudhuria mara tano kwa wiki bila kukosa.
Leo hii nampongeza sana Dr. Ngoma ambaye yuko na umri lakini amekuwa hodari sana katika kufanya mazoezi akiwa yeye na mke wake hata watoto wake wanahuduria mazoezi.
Hii ikimaanisha kwamba mazoezi ni kwa kila mtu kutojali umri au jinsia.
Dr.Ngoma akiwa katika mazoezi ya step aerobics katika gym ya UDSM
(aiyevaa tishet nyekundu hapo mbele kulia)
Akiwa katika umaahiri wake wa kupanda step bila ya kukosea Dr.Ngoma
Hakuna staili inayompita Dr.Ngoma kutokana na uelewa wake wa mazoezi
Leo hii nampongeza sana Dr. Ngoma ambaye yuko na umri lakini amekuwa hodari sana katika kufanya mazoezi akiwa yeye na mke wake hata watoto wake wanahuduria mazoezi.
Hii ikimaanisha kwamba mazoezi ni kwa kila mtu kutojali umri au jinsia.
Dr.Ngoma akiwa katika mazoezi ya step aerobics katika gym ya UDSM
(aiyevaa tishet nyekundu hapo mbele kulia)
Akiwa katika umaahiri wake wa kupanda step bila ya kukosea Dr.Ngoma
Hakuna staili inayompita Dr.Ngoma kutokana na uelewa wake wa mazoezi
Monday, September 2, 2013
FAIDA ZA KUTUMIA JUICE YA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI
Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali.
Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
Mangenisium
Mangnese
Potasium
Copper
Vitamini B6
Hii ikiwa katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa wataalamu kutengeneza tangawizi ni tiba tosha kwa magonjwa ya ngozi
Hili hapa kwenye picha ni zao la tangawizi kama linavyoonyesha likiwa bado kusagwa.
Faida za kutumia tangawizi:
-.Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wnawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
-Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
-Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
-Tangawizi husaidia kupunguz maumivu mwilini
-Husaidia kutoganda kwa damu mwilini
-Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.
Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama
Monday, August 12, 2013
MAZOEZI YA MASHINE YA ROWING NA FAIDA ZAKE
Katika dunia ya sasa kuna aina nyingi sana za mazoezi mbali na mazoezi ya Aerobics, ambayo husaidia kupunguza uzito kwa muda fulani.
Mazoezi mengine ambayo hushabihiana na mazoezi ya aerobics ni yale mazoezi ya kutumia aina ya mashine aina ya Rowing mashine.
Faida ya kufanya mazoezi ya rowing: Husaidia kupunguza uzito kwa kipindi kifupi kwa kuzingatia mzoezi yake.Hupunguza tumbo na kujenga misuli yake.Hupunguza mapaja yalokithiri.
Pia husaidia katika kuujenga moyo na kuwa mdhubuti. Pia hukupa uwezo wa pumzi yako kuwa ya uhakika.
Malaika akionyesha kutumia mashine ya Rowing kuanza zoezi hilo hapo juu.
(Unakunja miguu yako kwa kwenda mbele)
Mazoezi ya Rowing katika kumalizia zoezi hilo ambapo unajivuta nyuma
kama mwana mazoezi Mery(Malaika) akionyesha.
Monday, July 15, 2013
NAMNA YA KWENDA NA DAYATI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
Awali ya yote nawatkia mfungo mwema kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani wale waislamu popote walipo.
Kuna maswali ambayo mtu unaweza kujiuliza katika mambo yanayohusu ulaji wa mwezi huu mtukufu wa ramadhani ewe mwanamazoezi na namna gani utafanya mazoezi ukiwa umefunga.
Je utaweza kufanya mazoezi huku umefunga.
Je kuhusu aina gani ya chakula unatakiwa kula.
Katika mwezi huu wa mfungo mtu huwa unachoka ule mda wa jioni ambao unatakiwa kufanya mazoezi inakuwa ni vigumu maana unasikia njaa, kwa hiyo hata mazoezi huwezi kuenda.
Nakupa usauri wangu katika ulaji wako uchunge sana vitu vya mafuta mengi.
Ukisha maliza kufuturu unywe maji ya kutosha na upunguze kiasi cha chakula ambacho hukuongezea uzito kwa urahisi.
Baada ya kula futari utembee kwa muda wa dakika 20 baada ya hapo uendelee na mambo yako mengine, hii itakusaidia kusaga kile chakula na kukufanya kuwa mchangamfu.
Upate kahawa baada ya kupata futari hii pia itakusaidia kuondoa yale mafuta yaliyobaki kwenye mishipa yako ya mwili na kuifanya ipanuke na pia huondoa shibe.
Huu ni baadhi ya ushauri kwa wadau wa mazoezi ni muhimu kuzingatia.
Kuna maswali ambayo mtu unaweza kujiuliza katika mambo yanayohusu ulaji wa mwezi huu mtukufu wa ramadhani ewe mwanamazoezi na namna gani utafanya mazoezi ukiwa umefunga.
Je utaweza kufanya mazoezi huku umefunga.
Je kuhusu aina gani ya chakula unatakiwa kula.
Katika mwezi huu wa mfungo mtu huwa unachoka ule mda wa jioni ambao unatakiwa kufanya mazoezi inakuwa ni vigumu maana unasikia njaa, kwa hiyo hata mazoezi huwezi kuenda.
Nakupa usauri wangu katika ulaji wako uchunge sana vitu vya mafuta mengi.
Ukisha maliza kufuturu unywe maji ya kutosha na upunguze kiasi cha chakula ambacho hukuongezea uzito kwa urahisi.
Baada ya kula futari utembee kwa muda wa dakika 20 baada ya hapo uendelee na mambo yako mengine, hii itakusaidia kusaga kile chakula na kukufanya kuwa mchangamfu.
Upate kahawa baada ya kupata futari hii pia itakusaidia kuondoa yale mafuta yaliyobaki kwenye mishipa yako ya mwili na kuifanya ipanuke na pia huondoa shibe.
Huu ni baadhi ya ushauri kwa wadau wa mazoezi ni muhimu kuzingatia.
Monday, June 24, 2013
MWALIMU WA AEROBICS ALFA SIMWANZA AMALIZA CHUO KIKUU UDSM NA KUANZA KUFUNDISHA
Mwalimu chipukizi katika fani ya aerobics Alfa Simwanza ambaye amemaliza mafunzo yake ya miaka mitatu akiwania cheti cha digirii katika ualimu wa michezo kutoka chuo kikuu cha mlimani(UDSM).
Akiwa ameshiriki katika michezo yote, isipokuwa yeye amejikita katika ufundishaji wa mazoezi ya Aerobics.
Katika picha mwalimu Alfa (bukta buluu) akiwa katika darasa lake kwenye gym ya UDSM
Mwalimu A.Simwanza akifuatilia kwa makini wanafunzi wakifanya mazoezi
Mwalimu Alfa akibadili mwelekeo wa mazoezi huku wadau wakufurahia
Friday, June 21, 2013
FAIDA YA MATUMIZI YA KUTUMIA KINYWAJI CHA KAHAWA
Watu wengi hufikiria kahawa ni kwa ajili ya wale watu ambao hawahitaji kulala, huwa ndio faida yake tu lakini kahawa ina faida nyigi.
Huwasaidia kukuchangamsha na kuamsha akili na kuondoa uchovu.
Husaidia msago wa chakula kwa urahisi zaidi
Husaidia kupanua mishipa ya damu
Husaidia misuli ya moyo kuwa madhubuti katika msukumo wa damu mwilini.
Husaidia kuondoa mafuta kwenye damu.
Hii ikiwa ni baadhi ya faida za matumizi ya kahawa kwa binaadamu, na pia imefanyiwa majaribio na kuonekana inasaidia sana katika maisha ya mwanadamu kumfanya kuwa na afya bora na furaha.
Monday, May 20, 2013
WANAFUNZI WAALIMU WA AEROBICS CHUO KIKUU MLIMANI WAMALIZIA KOZI KWA FURAHA.
Waalimu wa kufundisha mazoezi ya aerobics wakiwa wanafikia ukingoni mwa hiyo kozi wakiwemo wametokea sehemu mbali mbali duniani wakisomea mazoezi ya aerobics Chuo Kikuu Mlimani.
Hapa wanafunzi wakiwa darasani kwa vitendo kwenye kozi ya
high and low aerobics
Wakiwa wanapokezana kufaya mazoezi ya kufundisha aerobics
Wanafunzi wa mataifa mbali mbali wakifurahia wenzao kuendesha
mazoezi
Hapa ni mwanafunzi wa mazoezi ya ualimu wa aerobics katika
step aerobics
Waalimu wa aerobics wakiwa kwenye pozi baaada ya mafunzo UDSM
PESS
Wanafunzi wa aerobics wakiwa na mwalimu Swai aliyevaa kofia
Tuesday, April 30, 2013
GYM YA CHUO KIKUU MLIMANI (UDSM) PESS YAFANA KATIKA MAZOEZI YA AEROBICS
Gym maarufu ambayo inaongoza kwa kutoa mafunzo ya waalimu wa aerobics hapa Tanzania na ambayo ina mwalimu aliyebobea katika mazoezi haya hapa Tanzania mwalimu O.Swai inafana kila kukicha kwenye mazoezi haya.Hivyo akitoa wito kwa wanamazoezi kujiunga katika gym hiyo iliyopo chuo kikuu na kupata mazoezi yaliyokwenda shule kama usemi wetu usemavyo Elimu Kwanza.
Mwalimu O.Swai akiwa kwenye darasa lake la step aerobics
chuo kikuu cha mlimani
Wadau wa aeobics wakifuatilia bila kukosea mazoezi ya step
Likiwa ni darasa lililoja wadau wa mataifa mbali mbali
wakifuatilia kwa makini mazoezi.
Kushoto mwanzo ni mdau wa mazoezi Isabellah akifuatilia kwa makini
Mwalimu Swai akiwa kwenye mwendo mdundo katika mazoezi.
Mwalimu O.Swai akiwa kwenye darasa lake la step aerobics
chuo kikuu cha mlimani
Wadau wa aeobics wakifuatilia bila kukosea mazoezi ya step
Likiwa ni darasa lililoja wadau wa mataifa mbali mbali
wakifuatilia kwa makini mazoezi.
Kushoto mwanzo ni mdau wa mazoezi Isabellah akifuatilia kwa makini
Mwalimu Swai akiwa kwenye mwendo mdundo katika mazoezi.
Wednesday, April 24, 2013
CLUB YA MAZOEZI YA AEROBICS YA VETA (DSMRVTSC) SASA YAVUMA
Ni kwa nadra sana kusikia wafanyakazi kuamua kufanya mazoezi na kwa moyo kama club ya VETA ambayo inavuma kwa sasa kwa ajili ya kufanya mazoezi, hii ni kwa sababu hata viongozi wao wanapenda mazoezi na kuwathamini wafanya kazi wenzao.
Klabu hii hufanya mazoezi mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu,Jumatano na Ijumaa wakifundishwa na mwalimu O.Swai akishirikiana na msaidizi wake mwalimu Sukamba.
Mwalimu Sukamba akiwa kwenye darasa lake la aerobics.
Wanawake wafanyakazi wa veta pia wanashiriki ipasavyo
Wafanyakazi wa veta wakiwa na kiongozi wao baser wa chiuo
aliyevaa tishet njano msitari wa kwanza.
Wafanyakazi wengi hufurahia mazoezi na kupata matokeo
mazuri na kuwa na afya njema.
Tuesday, April 23, 2013
MWALIMU WA AEROBICS ABDALA HERRI ANAVYOWIKA ABUDHABI KATIKA KUTOA AINA MBALI MBALI YA MAZOEZI YA VIUNGO
Mwalimu Abdala Herri ni kijana aliyebobea sana katika mazoezi haya ya aerobics, hata katika mazoezi ya spin yaani kuendesha darasa la baskeli maalum kwa mazoezi ya mwili yaitwayo spin bike.
Siyo hayo tu pia huendesha darasa la NRG ambalo unatumia barbell na uzito kwa ajili ya kuondoa manyama uzembe.
Pia hutoa ushauri kwa wateja wake ambao wana matatizo mbali mbali ya afya zao.
Hivi sasa Abdala yukoAbudhabi akifundisha kwenye Gym ya jeshi la huko na anatarajia kufungua gym hapa Tanzania na huko Mombasa Kenya.
Mwalimu Abdala yuko mbele kavaa tisheti nyekundu akiwa anafundisha darasa la spin
Hili ni darasa la NRG ambalo Abdala anafanyisha mazoezi yake ya mapaja.
(squat)kwa ajili ya kujenga misuli wa mbele ya paja
Abdala Herri akionyesha mazoezi kwa ajili ya kujenga misuli ya mgongo
Zoezi likiwa limepamba moto yakiongozwa na mwalimu Abdala. Herri.
Friday, April 12, 2013
KOZI YA AEROBICS INAYOFANYIKA CHUO KIKUU MLIMANI YAFANA SANA MWAKA HUU 2013
Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa Chuo Kikuu Mlimani(School of Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.
Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.
Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa ni pamoja na Aerobics and Fitness.
Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka China ambao wako na furaha.
Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.
Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.
Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)
Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.
Kila mwanafunzi hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema
Thursday, March 14, 2013
MAZOEZI YA AEROBICS YAFANA MJINI MOROGORO
Wakazi wa Morogoro mji uliozungukwa na milima ya uluguru na hali ya hewa nzuri,wakiwa na hamasa kubwa kufanya mazoezi ya viungo kwa afya yao, huku wakiongozwa na mwalimu Musiba Manyama ambaye ni mwalimu wa siku nyingi katika fani hii.
Gym hii ya mazoezi inaitwa SIMBA OIL GYM iliyopo katika majengo hayo ya Simba oil kituo cha petroli cha mjini Morogoro.
Mwalimu Musiba akiwa katikati ya wanafunzi akitoa mazoezi ya
kunyoosha viungo baada ya zoezi kuisha.
Hapa ni mwalimu mwalikwa Payas (mwenye kofia) kutoka Dar
ambaye ni mkurugenzi wa gym ya Fitness for Life akitoa mazoezi
Kina dada wa Moro nao hawapo nyuma kwa kufanya
mazoezi kwa afya zao
Mwalimu musiba akifanya mazoezi na wadau wake wa
Morogoro .Simba Oili Gym
Friday, February 22, 2013
NAMNA YA KULA MLO WAKATI UNAPOTAKA KUPUNGUA UZITO ULIOZIDI NA MAZOEZI
Kupunguza uzito ulokithiri huchukua muda mpaka kupata matokeo yake,ukiwa unazingatia kufanya mazoezi kama vile kutembea, kuendesha baiskeli na kufanya mazoezi ya aerobics ambayo hukupa matokeo haraka zaidi kuliko mazoezi yoyote yale.
Nikizungumzia mazoezi ya aerobics huwa nina maana kila sehemu ya kiungo cha mwili wako hufanyishwa mazoezi.
Ukizingatia kuanzia mwanzo wa zoezi hilo unaanza na kupasha mwili moto halafu ndio unaendelea na mazoezi mengine huku ukifuatilia ikienda sambamba na muziki maalumu kwa mazoezi tofauti.
Hii hukupa wewe mwanamazoezi kufanya na kufurahia,baada ya hapo ikifuatiwa na mazoezi kuunnyoosha mwili na kuondoa uchovu kwa kipindi chote cha mazoezi.
Na kumalizia na zoezi la kuondoa tumbo.
Lakini mazoezi yanatakiwa uende sambamba na kupunguza chakula kwa mfano ulikuwa unakula sahani iliyojaa unakula nusu yake. Hata hivyo uwe umepata kifungua kinywa cha kutosha itakisaidia kutokula hovyo hovyo.Mchana utakula kiasi tu ukipata matunda kwa wingi.
Wakati wa usiku ujitahidi upate chakula chepesi kwani maranyingi chakula cha jioni huongeza uzito kwa sababu ukishakula unaenda kulala na msago wa chakula huwa umesimama hadi kesho yake saa 12 asubuhi.
Pia jitahidi kupunguza mafuta kwenye chakula hata sukari iwe kiasi na chumvi pia itakusaidia kupunguza uzito.
Aina ya mazoezi ambayo unatakiwa kufanya kama picha inavyoonyesha
Kuna aina nyingi ya mazoezi ambayo husaidia kukupunguza kwa kutumia mashine
Thursday, February 7, 2013
AINA MBALI MBALI YA MAZEOZI YA VIUNGO(AEROBICS)
Katika kufanya mazoezi ya viungo unaweza pia kufanya mazoezi kwa kucheza utakavyo ili mradi unaendana na midundo.
Hivi sasa waalimu wa mazoezi haya ya viungo wamegundua namna ya kuwavutia wadau wa mazoezi haya kwa kuwapa mtindo na aina ya muziki
Hapa ni namna ya kuanza zoezi la kick box
Namna ya kutupa ngumi pamoja kufuatilia mdundo
Jinsi ya kutumia mateke au kutumia goti uku ukienda na muziki
Mwalimu Swai akitoa mafunzo namnkukunja na kutupa ngumi
Monday, January 21, 2013
MBAGALA JOGGING CLUB WAKARIBISHWA VETA CLUB KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA
Klabu ya mazoezi ya viungo ya VETA chuo cha ufundi stadi Dar es salaam ikiwa imewakaribisha wanamazoezi wenzao kutoka klabu ya Mbagala Joging ikiongozwa na mwalimu wao Adam Gwao ambaye pia ni muasisi wa club hiyo. Mazoezi hayo yalifana sana ambayo yalianza majira ya saa 12 hadi saa moja asubuhi yakiwa yamehudhuriwa na wakuu wa chuo hicho cha Veta.
akiwa mbele ya wanamazoezi na mwalimu Adam Gwao tayari kuanza zoezi la Aerobics
Mazoezi yameanza pamoja na mkuu wa chuo cha Veta (mwenye fulana ya bluu ) akiwa
mstari wa mbele.
Zoezi lilipamba moto kila mtu akiwa mwenye furaha asubuhi hiyo ya mazoezi
Kila mtu alikuwa na usongo wa kufanya zoezi siku hiyo bila kushindwa au kuchoka
Mkuu wa chuo cha Veta Mr. Samwel Ng'andu akizungumza na wanamazoezi
na kuwakaribisha wanamazoezi wa Mbagala club wote wakimsikiliza kwa makini.
Mwalimu O.Swai akitoa mafunzo ya lishe bora baada ya kumaliza mazoezi ya siku hiyo
Akisema "Kufanya mazoezi peke yake hayasaidi ila ni pamoja na kujaribu kubadili tabia
ya kula mlo".
Subscribe to:
Posts (Atom)