Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa Chuo Kikuu Mlimani(School of Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.
Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.
Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa ni pamoja na Aerobics and Fitness.
Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka China ambao wako na furaha.
Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.
Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.
Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)
Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.
Kila mwanafunzi hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema
No comments:
Post a Comment