Mwalimu Abdala Herri ni kijana aliyebobea sana katika mazoezi haya ya aerobics, hata katika mazoezi ya spin yaani kuendesha darasa la baskeli maalum kwa mazoezi ya mwili yaitwayo spin bike.
Siyo hayo tu pia huendesha darasa la NRG ambalo unatumia barbell na uzito kwa ajili ya kuondoa manyama uzembe.
Pia hutoa ushauri kwa wateja wake ambao wana matatizo mbali mbali ya afya zao.
Hivi sasa Abdala yukoAbudhabi akifundisha kwenye Gym ya jeshi la huko na anatarajia kufungua gym hapa Tanzania na huko Mombasa Kenya.
Mwalimu Abdala yuko mbele kavaa tisheti nyekundu akiwa anafundisha darasa la spin
Hili ni darasa la NRG ambalo Abdala anafanyisha mazoezi yake ya mapaja.
(squat)kwa ajili ya kujenga misuli wa mbele ya paja
Abdala Herri akionyesha mazoezi kwa ajili ya kujenga misuli ya mgongo
Zoezi likiwa limepamba moto yakiongozwa na mwalimu Abdala. Herri.
No comments:
Post a Comment