Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, May 23, 2012

JINSI UNAVYOTAKIWA KUFANYA MAZOEZI NA MUDA WAKE

Kuna baaadhi ya watu ambao wanafanya mazoezi kwa kupita kiasi,kwa maana hiyo hufikiria kufanya mazoezi kwa muda unaozidi saa moja ndio utakuwa unapunguza uzito na wengine hudiriki kufanya mara saba kwa wiki tena sio chini ya saa mbili.

Hii  siyo sahihi kwa sababu mwili wa binadamu unahitaji muda wa kupumzika na kuupa nafasi ya kujenga misuli ya mwili kwa mpangilio ulosahihi kutokana na maumbile yake.

Muda maalum unaotakiwa kufanya mazoezi usizidi saa moja na ikwa imepungua ni dakika 30 kwa siku mara tano kwa wiki,hii inasaidia kupunguza kaloriz ambazo hazihitajiki  mwilini.Kwani binaadamu anatakiwa awe anapata kaloriz 1500 kwa siku kutokana na chakula anachokula hii humsaidi awe na afya njema na kutokuwa namaradhi yanayosababishwa na mafuta  kwa wingi mwilini.

Madhara wanayopata wale wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu bila ya kupumzika huwa yanawafanya kuonekana wamechoka muda wote huonekana kuzeeka hararaka haswa sehemu ya uso wake.
Epuka kuzidisha mazoezi na pata muda wa kuupumzisha mwili ili kujenga seli mpya za mwili.
















Katika picha inaonyesha baadhi ya mazoezi ya 
viungo  namna unavyoanza na kumalizia.
Je wewe waweza haya mazoezi.JARIBU LEO;

No comments: