MARA NYIGI SANA UTAKUTA WATU WAKIDANGANYANA KUHUSU NAMNA YA KUFANYA DIETY.
HII NI KWA SABABU YA KUTOKUWA NA UELEWA WA NAMNA GANI MWILI WAKO UNATAKIWA KUWA AU KUUFANYIA PINDI UNAPONENEPA.
HAYA MATATIZO MARA NYINGI HUWAKUTA KINA MAMA NA AKINA DADA WALE AMBAO WAMEPANIA KUPUNGUZA MWILI, LABDA KAAMBIWA NA DAKTARI, AU AMEONA KWAMBA KILA AVAAPO NGUO HAIMPENDEZI, NDIPO HUAMUA KUJINYIMA KULA AU KULA VITU VYA AJABU BAADAE HUMLETEA MADHARA.
KWA MFANO MTU ANAKUAMBIA ETI UNYWE NDIMU GLASI MOJA KILA SIKU NDIYO INAYOKONDESHA AU UJINYIME KUTOKULA KAWAIDA KWA MUDA WA WIKI MBILI KWELI UNAJITAKIA MEMA, MAADA BAADA YA HAPO UNAPATA VIDONDA VYA TUMBO.
NA UZITO UNARUDI PALE PALE,PINDI UENDELEAPO KULA KAWAIDA.
KAMA UMEAMUA KUFANYA DAYATI NI KUPUNGUZA MLO UNAOKULA NA KAMA ULIKUWA UNAKULA MAFUTA MENGI KWENYE CHAKULA PUNGUZA PIA.
PIA UJITAHIDI KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU. MWILI HUNENEPA KUTOKANA NA KULA BILA MPANGILIO.
PINDI UFUATAPO HAYA MAELEKEZO UTAISHI BILA YA KUPEWA MASHRTI NA DAKTARI NA KUJISIKIA RAHA WAKATI WOTE.
No comments:
Post a Comment