Thursday, December 29, 2016
Thursday, November 24, 2016
MLO WA SIKU NI KIFUNGUA KINYWA (A MEAL OF A DAY IS BREAKFAST)
Kwa nini nazungunzia Mlo wa siku ni kifungua kinywa' Nikimaanisha kwa wale ambao wanahitaji kujenga miili yao hawana budi kupata chai nzito ikiwa imeshehena matunda,protini ikiwa ni kama nyama kiasi cha nusu kilo asubuhi hii ni kwa ajili ya wale wenye kujenga misuli kwani wanahitaji protini ya kutosha kwa ajili ya kupata virutubisho vya kujenaga misuli.
Halikadhalika awe anapata miilo zaidi ya mitatu nikimaanisha mara tano kwa siku awe anakula .Kila baada ya zoezi unatakiwa kupata aina ya chakula cha wanga, hii ikiwa ni mahitaji ya mjenga misuli anahitajika kula kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kurudishia viambatanino vilivyotumika wakati wa mazoezi.
Mwili uliojengwa kwa mazoezi na kula ipasavyo.(Body Builder)
Wednesday, October 12, 2016
MAZOEZI YA KUJENGA MKONO BICEPS CURL KWA KUTUMIA CABLE MACHINE
Kuna aina nyingi za kufanya mazoezi ya kujenga mikono kwa wakati mwingine unafanya kwa kutumia free weight, kama vile dumbell au barbell.
Kwa leo tunaanza na mazoezi ya mkono kwa kutumia cable mashine namna unavyoanza na kumaliza.Mazoezi haya unafanya seti tatu kwa hesabu ya kumi na tano kila mkono
kumalizia kama picha zikionyesha juu na chini
Baada ya kubadilisha mkono wako nakufanya
zoezi hilo hilo la biceps curl seti 4x15..
Tuesday, September 13, 2016
MAZOEZI AMBAYO WAWEZAFANYA HATA UKIWA NYUMBANI HASWA KAMA HUJAWAHI KUFANYA MAZOEZI
Mara nyingi watu hufikiria kuanza kufanya mazoezi pindi akiwa na tatizo la uzito au daktari kamshauri aanze kufanya mazoezi.
Mimi nashauri isifikie hapo maana mazoezi ni jambo la muhimu mtu yeyote yule anayekula vizuri na pia ni dawa, hukufanya kuwa mchangamfu wakati wote wa maisha yako.
kama unaruka ukirudi chini unakunja goti lako na
unafanya kwa sekunde 30 halafu unabadili miguu.
Zoezi la jumping lunge kumalizia mguu mwingine
Picha hizi mbili zikionyesha namna ya kufanya zoezi la tumbo
ukiwa umesimama kwa kuanza mguu wako nyuma na kupandisha
juu huku goti lako limejikunja na mikono yako kwenda nyuma
kama picha ya juu ikionyesha unavyoanza na ya chini ukimaliza
unafanya kwa muda wa sekunde 45 halafu unapumzika na kurudia
tena.
Zoezi hili linaitwa Side bridge ukiwa umelala upande na
kunyanyuka juu kwa kutumia mkono mmoja unakaa kwa
sekunde 30 kama picha inavyoonyesha na kubadilisha upande
mwingine
Monday, August 8, 2016
AINA YA MAZOEZI YA TUMBO NA FAIDA ZAKE KWA MUDA WA DAKIKA 20 TU.
Yapo aina mbalimbali ya mazoezi ya kuondoa tumbo ambalo limekuwa likisumbua kutopungua.
Yafuatayo ni aina mbalimbali ya mazoezi ambayo yanasaidia kwa kufanya kwa muda wa dakika 20 tu.
Zoezi la Bicycle crunh ambalo unafanya kwa muda
wa sekunde 60 kama zoezi linavyoonyesha hapo juu,
Zezi hili la Glute bridge leg rise unafanya zoezi hili kwa sekunde
30 na kubadili mguu mwingine kwa muda huo.
Zoezi hili linaitwa Dorsal rise unafanya kwa muda wa
sekunde30 halafu unapumzika kwa sekunde15 na kuanza tena,
Tuesday, July 26, 2016
NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA TUMBO NI KITU GANI HUSABABISHA KUWA NA TUMBO KUBWA .
Kutokana na maumbile yako ulozaliwa nayo na umbo lako la mwili, hii hukuwezesha wewe kuwa na mafuta ambayo ni muhimu kwa matumizi ya umbile lako. Kwa mfano mwanamke huwa ana asilimia kubwa ya mafuta kuliko mwanaume hii ni kwa ajili ya maumbile yake ya kuweza kuwa na uwezo wa kubeba mtoto tumboni bila tatizo.
Lakini hata hivyo mkusanyiko huwa unakuwa sehemu ya tumboni mara nyingi na ikizidi kiwango chake husababisha maradhi ya moyo.
Hata hivyo ukijitahidi kufanya mazoezi mara kwa mara unaweza kuepukana na maradhi haya na mengineyo.
yako nyuma ya kichwa kwa kukuwezeshakunyanyua sehemu ya
mabeba yako juu.
Namna ya kumalizia zoezi la kwanza na unafanyahivyo mara
20 x5 kukamilisha zoezi.
Zoezi hili unanyooka huku umekunja mikono yakona kuhesabu
hadi 50 unarudi chini na hakikisha unakaza tubo
Unaendelea na zoezi lingine kama hili kwa kuzingatiamfumo wa
hesabu kama la mwanzoni
Monday, June 20, 2016
MAMA GYM AU AGNES WA CLUB YA MAZOEZI CHUO KIKUU CHA UDSM AMBAYE NI MWANAMAZOEZI ALIYEFANIKIWA NA MAZOEZI YA AEROBICS
Mwana mazoezi mkongwe mama Gym wa clabu ya mazoezi ambayo iko chuo kikuu cha Dar es salaam Pess.
Mfanikio ya mazoezi ya mama gym aka Agnes. ni makubwa ambayo yamemfanya ajivunie kufanya mazoezi ya aerobics.
Mama Gym akiwa kwenye cross training mashine
Monday, May 23, 2016
WANAFUNZI WA PESS WAKIWA KATIKA MAZOEZI KWA VITENDO YA WALIMU WA AEROBICS KUTOKA NETHERLAND
Katika ushirikiano wa taaluma ya michezo Netherland pia kuna waalimu wa mazoezi ya aerobics ambao wakishirikiana na mkufunzi wa Aerobics UDSM Pess Mkufunzi Swai akiwa na Anu kutoka Netherland wakishirikiana kutoa mafunzo ya nadharia ya Aerobics.
Thursday, May 5, 2016
KOZI YA MAFUNZO YA WAALIMU WA AEROBICS YAANZA KUPAMBA MOTO UDSM PHYSICAL EDUCATION SPORT AND SCIENCES (PESS)
Mafunzo ya Aerobics ambayo yanafanyika katika chuo kikuu cha Mlimani UDSM kila mwaka.
Wanafunzi wa Pess wakiwa na waendeshaji wa hiyokozi nyuma kushoto Dr.Maro na Mkufunzi O.Swai
Wanafunzi wa Pess wakifuatilia mafunzo ya Aerobic
Chuo kikuu cha Mlimani UDSM
Thursday, April 21, 2016
FAIDA ZA KUNYWA MAJI KATIKA MAISHA YAKO YA KAWAIDA KILA SIKU
OK BODY SHAPE
HIZI HAPA NI FAIDA UNAZOPATA UKINYWA MAJI KILA SIKU
-Kunywa maji glasi 2 asubuhi inasaidia kuamsha seli hai za mwili.
-Kunywa glasi 1 ya maji kabla hujala chakula husaidia msago wa chakula kwa wepesi zaidi.(digestion)
-Ukinywa glasi moja ya maji kabla ya kwenda kuoga inasidia kujikinga na shindikizo la damu(high blood pressure)
-Ukinywa maji glasi 1 kabla hujaenda kulala husaidia kujikinga na kupooza mwili (strokes heart attacks)
EPUKA MATATIZO KWA KUNYWA MAJI UTAKUWA SALAMA.
Friday, March 18, 2016
MWANA MAZOEZI WA SIKU NYINGI LUKUMAI AKIWA ANAFANYA MAZOEZI YA ROWING
Mkongwe wa mazoezi ya aerobics mzee Lukumai ni mwana mazoezi aliyebobea katika mazoezi, japo umri umeenda lakini hakosi kufanya mazoezi na pia amekuwa ni mtu mwenye malengo katika kufanya mazoezi.
Hivyo tujue mazoezi hayana uzee wala kukata tamaa. ufanyapo mazoezi ndipo unajiwekezea afya yako ya uzeeni kwa kutougua mara kwa mara na kuonekana kijana kila siku na mchangamfu.
Mwana mazoezi Lukumai akifanya zoezi la rowing mashine
Thursday, February 25, 2016
MWALIMU DULLA KASHAIJA WA MAZOEZI YA AEROBICS AMEFUNGUA GYM ILALA.
Malimu Dulla K. wa mazoezi ya Aerobics akiwa na wanamazoezi wake katika gym yake Ilala.
Mwalimu Kashaija akiwa na class yake ya stepakiwa mbele ya darasa.
Wanamazoezi na wapenzi wa Aerobics wakifanya tizi
Wana mazoezi ya aerobics waliobobea katika mazoezi hayo
Tuesday, January 26, 2016
MAZOEZI YA KUPUNGUZA TUMBO KWA KUTUMIA AINA TOFAUTI ZA MASHINE
Mara nyingi wakati wa mazoezi jaribu kubadili zoezi husika kwa matokeo chanya,hapa chini ni mazoezi ya tumbo kwa kutumia mashine.
Aina ya mazoezi haya ufanye mara mbili kwa wiki kupata matokeo mazuri
Mazoezi ya tumbo kwa kutumia mashine ya
kebo namna ya kuanza na kumaliza
Picha hii ikionyesha namna ya kuanza na kumalizia
zoezi lenyewe kwa kutumia mashine aina ya farasi.
Thursday, January 21, 2016
MAMBO MUHUMU UNAYOPSWA KUYAJUA KABLA HUJAANZA MAZOEZI KWA MTU YEYOTE
Yapo mambo mengi ambayo unapaswa kujua kabla ya kuanza mzoezi, lakini leo nakujuzu baadhi ya mambo muhimu.
1.Hakikisha kama una tatizo la moyo au tatizo la afya yako ukamuone kwanza daktari kwa ushauri.
2.Kama huna tatizo la kiafya basi unaweza kuanza kufanya mazoezi kwa kuzingaztia unaanza kwa kupasha mwili joto(warm up) kwa ajili ya kuutayarisha mwili wako kwa zoezi lifuatalo.
3.Baada ya kumaliza mazoezi ni muhimu sana kunyoosha misuli yako,(stretching) hii husaidia kutoa aina ya lactic acid ambayo husaidia kuondoa maumivu kwenye misuli na pia kunyambulika(kulainisha) kwa misuli yako na kuwa na ukubwa unaotakiwa.
4.Jaribu kuusikiliza mwili wako kama unakubaliana na zoezi ulolifanya kama kuna maumivu makali ambayo hayaishi pindi ufanyapo mazoezi acha na kufuata ushauri wa mwalimu wa mazoezi.
Subscribe to:
Posts (Atom)