MAMBO MUHUMU UNAYOPSWA KUYAJUA KABLA HUJAANZA MAZOEZI KWA MTU YEYOTE
Yapo mambo mengi ambayo unapaswa kujua kabla ya kuanza mzoezi, lakini leo nakujuzu baadhi ya mambo muhimu.
1.Hakikisha kama una tatizo la moyo au tatizo la afya yako ukamuone kwanza daktari kwa ushauri.
2.Kama huna tatizo la kiafya basi unaweza kuanza kufanya mazoezi kwa kuzingaztia unaanza kwa kupasha mwili joto(warm up) kwa ajili ya kuutayarisha mwili wako kwa zoezi lifuatalo.
3.Baada ya kumaliza mazoezi ni muhimu sana kunyoosha misuli yako,(stretching) hii husaidia kutoa aina ya lactic acid ambayo husaidia kuondoa maumivu kwenye misuli na pia kunyambulika(kulainisha) kwa misuli yako na kuwa na ukubwa unaotakiwa.
4.Jaribu kuusikiliza mwili wako kama unakubaliana na zoezi ulolifanya kama kuna maumivu makali ambayo hayaishi pindi ufanyapo mazoezi acha na kufuata ushauri wa mwalimu wa mazoezi.
No comments:
Post a Comment