NI NAMNA GANI UNAWEZA KUPUNGUZA UZITO ULOKITHIRI
Watu wengi huona ugumu wa kupunguza uzito wa mwili wao lakini wengi wao hawajui madhara ya kuwa na uzito ulokithiri. Hii husababisha kuwa na tatizo la presha na kisukari.
Inatokea mpaka daktari akushauri kupunguza uzito, hapo ndipo anapoanza kuhangaika kuupunguza uzito ambao umemzidi na kusababisha madhara mwilini mwake.
Kuna njia muafaka wa kukufanya usiwe unaongezeka uzito mara kwa mara na njia yenyewe ni kubadilisha tabia ya kula hovyo na kuendekeza kusikia njaa na muda wa kupata maakuli ni bado.
Jaribu kula kwa wakati mmoja kama uliamua kula chakula cha mchana saa saba muda huo usipitilize ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha chakula unachokula kila siku.Hii itakusaidia kupunguza uzito ulokithiri,bila kusahau kufanya mazoezi ambayo yatakufanya kutoa jasho japo kwa muda wa dakika thelathini, kama una tabia ya kupenda kula kila wakati basi uwe unapata matunda pindi unapojisikia hivyo.
Usisahau wakati wa usiku pata chakula chepesi na uwe unakunywa maji kwa wingi japo lita mbili kwa siku, utakuwa na afya nzuri na uzito wako ulokithiri utapungua na hakikisha unalala muda wa saa nane wakati wa usiku.
No comments:
Post a Comment