Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Sunday, August 23, 2015

MWANA MAZOEZI ANATAKIWA MARA NGAPI KWA WIKI KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO.

Mara nyingi katika suala la kufanya mazoezi kwa wana mazoezi  huwa na sintojua, mara ngapi kwa wiki unatakiwa kufanya mazoezi  ni wakati gani unatakiwa kuupumzisha mwili kwa ajili ya kujenga seli ambazo zimekufa katika mwili wa mwana mzoezi.

Mwana mazoezi anatakiwa kufanya mazoezi mara tano kwa wiki au mara tatu kama huwezi kufanya kwa siku tano. Nikisema hivyo nina maana mwili unahitaji kupumzishwa kutosha,ikiwa na kuhakikisha unalala sio chini ya masaa nane.

Pamoja na yote hayo kunywa maji ya kutosha kila siku ikiwa sio chini ya lita mbili,ni muhimu sana haswa kwa yule anayefanya mazoezi kila siku sababu mwili wa binaadam ni pasenti 60 ya maji.

No comments: