Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Monday, August 31, 2015

MASHINDANO YA WATUNISHA MISULI (BODY BUILDER) THE MOST MUSCULER MAN 2015


Mashindano yliyofana sana ambayo yalikuwa na washiriki kutoka Tanzania Bara na Visiwani  Zanzibar.

Hii ikiwa ni mara ya pili kufanyika  Dar es salaam na mwasisi Mohamed Ally ambaye ni mkurugenzi wa Tanzaned  Fitness iliyoko Gymkhana.

                     

                            Mkuu wa stegi Omar swai akiwa na Mr.India 
                            ambaye alialikwa kama mgeni katika kutunisha


Wanamisuli wakiwa katika mshindano ya kuonyesha
misuli ya tumbo kama picha inavyoonyesha




 

 
                         
 
 
 
 

 
                                Wshiriki  wakiwa wanasubiri kuingia katika gwee yao



 Mukurugenzi wa Tanzaned akiwa na mkuu wa wilaya ya
 Kinondoni wakimkabidhi zawadi ya cheki ya sh. 1500,000 
mshindi Omary aliyetokea mkoa wa Mbeya

 
 
 

Sunday, August 23, 2015

MWANA MAZOEZI ANATAKIWA MARA NGAPI KWA WIKI KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO.

Mara nyingi katika suala la kufanya mazoezi kwa wana mazoezi  huwa na sintojua, mara ngapi kwa wiki unatakiwa kufanya mazoezi  ni wakati gani unatakiwa kuupumzisha mwili kwa ajili ya kujenga seli ambazo zimekufa katika mwili wa mwana mzoezi.

Mwana mazoezi anatakiwa kufanya mazoezi mara tano kwa wiki au mara tatu kama huwezi kufanya kwa siku tano. Nikisema hivyo nina maana mwili unahitaji kupumzishwa kutosha,ikiwa na kuhakikisha unalala sio chini ya masaa nane.

Pamoja na yote hayo kunywa maji ya kutosha kila siku ikiwa sio chini ya lita mbili,ni muhimu sana haswa kwa yule anayefanya mazoezi kila siku sababu mwili wa binaadam ni pasenti 60 ya maji.

Tuesday, August 11, 2015

WANAMAZOEZI WA AEROBICS UDSM WAKIWA NA KASI YA KUFANYA MZOEZI KWA AFYA ZAO


Mazoezi ni jambo la muhimu sana katika maisha ya kila siku.

 Ikiwa unataka kuishi kwa raha fanya mazoezi na pia yanarefusha umri wako.

                                                          Mazoezi ya Hi/Lo Aerobics 
                             

                                     


                               Wadau wa Aerobics wakifanya mazoezi hayo kwa umakini

                                H/ Lo Aerobics

Thursday, August 6, 2015

NI NAMNA GANI UNAWEZA KUPUNGUZA UZITO ULOKITHIRI

Watu wengi huona ugumu wa kupunguza uzito wa mwili wao lakini wengi wao hawajui madhara ya kuwa na uzito ulokithiri. Hii husababisha kuwa na tatizo la presha na kisukari.

Inatokea mpaka daktari akushauri kupunguza uzito, hapo ndipo anapoanza kuhangaika kuupunguza uzito ambao umemzidi na kusababisha madhara mwilini mwake.

Kuna njia muafaka wa kukufanya usiwe unaongezeka uzito mara kwa mara na njia yenyewe ni kubadilisha tabia ya kula hovyo na kuendekeza kusikia njaa na muda wa kupata maakuli ni bado.

Jaribu kula kwa wakati mmoja kama uliamua kula chakula cha mchana saa saba muda huo usipitilize ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha chakula unachokula kila siku.Hii itakusaidia kupunguza uzito ulokithiri,bila kusahau kufanya mazoezi ambayo yatakufanya kutoa jasho japo kwa muda wa dakika thelathini, kama una tabia ya kupenda kula kila wakati basi uwe unapata matunda pindi unapojisikia hivyo.

Usisahau wakati wa usiku pata chakula chepesi na uwe unakunywa maji kwa wingi japo lita mbili kwa siku, utakuwa na afya nzuri na uzito wako ulokithiri utapungua na hakikisha unalala muda wa saa nane wakati wa usiku.