Monday, December 22, 2014
SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WANA MAZOEZI WOTE
,,,,,,,,NAWATAKIA KILA LA KHERI NA FANAKA KATIKA KUSHEREKEA ,,,,,,,
,,,,,,,,, SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA WA 2015,,,,,,,,
,,,,,,,,,, UWE WENYE HERI NA MAFANYIKIO KATIKA,,,,,,,,,
--------- MSIMU HUU WA MAPUMZIKO---------
,,,,,,, KWA WANA MAZOEZI,,,,,,
Thursday, November 27, 2014
MAMBO MUHIMU KWA ANAYEFANYA MAZOEZI YA KUJENGA MISULI(BODY BUILDING)
(Body building) Mjenga misuli ni muhimu sana awe na mwenzake wa kumsimamia wakati akiwa anafanya mazoezi(msaidizi) hii inasaidia kumlinda asije umia kwa uzito anaobeba kumshinda kunyanyua na kumrudia shingoni hii ni hatari inaweza kusababisha kupoteza maisha pao hapo.
Hii pia humsaidia yule mwana mazoezi kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito mkubwa akitegemea kuwa na msaidizi nyuma yake na kumsaidia kunyanyu hadi kufikia lengo lake, na kumpa moyo mnyanyuaji uzito.
hii hapa ni namna unavyoanza.
mwana mazoezi mwenzako.
Friday, November 21, 2014
AINA YA MAZOEZI YA KUONDOA MAFUTA NA KUJENGA MISULI YA TUMBO UKIWA NYUMBANI.
Mazoezi ya kuondoa tumbo kama usemi unaotumika ni zoezi ambalo unatakiwa kuwa na moyo wa kufanya zoezi hilo na kupania kiukweli kwa kuwa na ari ikiwa inafuatiwa na shauku kubwa ya kujenga misuli yake (six pax).
Yafuatayo ni baadhi ya mazoezi ambayo unashauriwa kuyafanya marakwa mara na kila siku katika picha.
Ikiwa kila zoezi unalofanya unatakiwa uwe na uwezo wa kufanya mara mia sita kwa mpangilio utakao jipangia mwenyewe.
Mazoezi haya aina tatu ni namna unavyoanza na kumalizia
unapeleka mikono kama unakata panga
Aina ya pili ya mazoezi inayojulikana kama side cranch
ikionysha unavyoanza na kumalizia unafanya mara hamsini
bila ya kupumzika.
Zoezi hili pia ni la tumbo iukitumia mpira maalum kwa
kuunyanyuka nao na kurudi chini kama picha zinavyoonyesha

Thursday, November 20, 2014
MWALIMU SHWAHIBU (ANDUNJE) ALIYEBOBEA KATIKA KUFUNDISHA MAZOEZI YA AEROBICS.
Bila shaka nikimzungumzia mwalimu Andunje kwa wakazi wale wa Dar es salaam sio jina geni hususan kwa wale wanaofanya mazoezi ya aerobics kwenye club mbalimbali hapa jijini.
Mwalimu Andunje alianza kufanyisha mazoezi katika ukumbi wa vijana pale mango garden na baadae alijiendeleza alipokuwa Kelken gym iliyopo chan'gombe na nyerere road.
Hapo alikutana na mkongwe wa mazoezi ya aerobic ambaye hivi sasa anafundisha chuo kikuu mlimani na kufuzu.
Mwalimu Shwahibu aliye maahiri katika mzoezi ya aerobics
na pia hutegemea sana kwa kumuingizia kipato.
Hapo akionyesha mazoezi ya kunyoosha viungo kwenye
gym ya UDSM.
Mwalimu Andunje akiwa kwenye darasa lake akionyesha
mazoezi na kufuatilia kwa makini
Tuesday, October 21, 2014
SIRI YA MAFANIKIO YA KUWA MWANA MAZOEZI BORA YA KUJENGA MISULI
Yafuatayo ni namna ya kuepuka makosa ya kawaida wakati ukifanya mazoezi ya kujenga misuli;
1. Usiache wala kupuuzia mazoezi ya kupasha mwili moto(warm up)
Mara nyingi misuli ambayo inapata maumivu makali ni ile ambayo imekosa mazoezi ya kupasha misuli moto(warm up) kuliko yule aliyeanza na mazoezi ya kupasha moto.
Kabla ya kufanya zoezi la kujenga misuli ni muhimu kupasha misuli kwa muda wa dakika tano hadi kumi kama vile kuendesha baiskeli au zoezi la aerobic ili kupandisha joto la mwili na kuwa tayari kwa kunyanyua uzito.
2.Usiharakishe unapofanya mazoezi ya kujenga misuli.
Wakati wa kubeba uzito ni muhimu kutofanya kwa haraka haraka, fanya pole pole kunyanyua uzito usiwe na haraka kwani kufanya mazoezi tartibu husaidia kujenga msuli husika kwa uhakika zaidi na kuusikia.
3.Epuka kufanya zoezi likazidi kipimo cha uwezo wako.
Wanamazoezi wajenga misuli hufanya zoezi aina moja ka muda mrefu na kufanya kujisikia zoezi hilo linachosha hii sio sahihi, Fanya mazoezi ya kujenga misuli kwa mzunguko unaotakiwa.
4.Usipuuze maumivu ya misuli pindi uyasikiapo jichunguze.
Kama utasikia maumivu makali wakati unafanya mazoezi ya kujenga misuli, unashauriwa kupumzika siku hiyo au kupunguza uzito unaobebe.
5.Usifanye mazoezi ya kujenga misuli bila ya kuvaa viatu vya mazoezi
Viatu husaidia sana kuepuka kuteleza wakati ukiwa unafanya mazoezi ya kunyanyua uzito,ni muhimu sana kuvaa.
Monday, September 22, 2014
MAZOEZI YA TUMBO NA UMUHIMU WAKE
Kuna aina nyingi ya mazoezi ya tumbo na namna ya kuyafanya hii ikiwa ni kuondoa yale mafuta ambayo yapo juu ya tumbo.
Kuna watu wengine husema kuna zoezi tumbo la juu na la chini au pembeni lakini zoezi ni la aina moja tu kwa sehemu hizo zilizotajwa hapo juu.
Kwa utafiti zaidi ujaribu kufanya zoezi hilo utagundua ni sehemu zote zinakuwa na uhusiano sawa (kukaza kwake),hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa wataalamu wa mazoezi.
Mazoezi ya tumbo kwa kugusa goti ikiwa ni upande
(Oblique mascles) jinsi unavyoanza zoezi hilo.
Zoezi hili lonyesha namna ya kulikamilisha kwa
kugusa goti kwa kutumia mkono mmoja.
Zoezi hili hapa likiwa ni aina ingine ya kunyoosha
mikono na kuanza kwa zoezi hilo kama inavyoonyesha
Hapa picha inaonyesha jinsi ya kumaliza zoezi kwa kugusa magoti yote
Mazoezi ya pembeni mwa mbavu(Oblique)
kama picha ikionyesha hapo juu.
Tuesday, August 26, 2014
MAMBO AMBAYO MTUNISHA MISULI(BODY BUILDING) ANAPASWA KUFANYA NA KUONEKANA AMEJENGA VEMA
Mambo muhimu ambayo anapaswa kuyajua mtunisha misuli(bodybuilding)
(a)Awe na malengo wakati wa kufanya mazoezi ya kujenga misuli na ajielewe,
(b)Anatakiwa ajue vyakula vya kula wakati akifanya mazoezi haya ya kujenga misuli kwa sababu mwili haujengeki kwa kubeba uzito tu bali ikiwa inakwenda sambamba na lishe bora na iwe ya kutosha sio kujinyima.
(c)Awe anapata vyakula vya aina ya protin kwa wingi ili kusaidia kujenga na kukuza misuli pamoja na chakula cha wanga kwa kuleta nguvu mwilini.Hii ikiwa na nyama kwa wingi pamoja na mayai yasiyopungua 9 wakati wa chai ya asubuhi.
(d) Usikae mpaka ukasikia tumbo halina kitu unatakiwa ujisikie wakati wote una chakula tumboni kwani wakati wote mwili wako unahitaji chakula kwa ajili ya kujenga misuli imara na mikubwa.
(e)Kufanya mzoezi kwa kuongeza uzito unaonyanyua kila seti.
(f) Pata muda wa kutosha kupumzika wakati umalizapo mazoezi ili kuupa mwili nafasi ya kujenga misuli.
Haya ndio matokeo ya mazoezi ya kujenga misuli pamoja na lishe bora
Wednesday, August 6, 2014
MAZOEZI NI KIUNGO MUHIMU KATIKA MAISHA YA KILA SIKU BILA SHAKA
Nimezungumzia kuhusu hilo kwa sababu unapopata mlo ni lazima utumike ipasavyo kwenye mwili wa kila binadamu, hiyo nikiwa na maana baada ya kupata mlo huo inachukua saa tatu tu chakula hicho kusagwa na kwenda kwenye sehemu husika ya mwili wa binaadamu.
Hivyo basi ni muhimu kuhakikisha wakati wa usiku unapata mlo mwepesi ambao hautakuathiri na kukuletea athari ya afya yako, pia jaribu kutembea kwa muda wa dakika 15 au 20 mwendo wa haraka kama huna muda wa kwenda gym au kama una baskeli ni vema uendeshe kwa muda wa dakika 20.itakuwa umeondoa kaloriz ambazo zimezidi mwilini mwako.
Bila shaka inawezekana kufanya hivyo na kutetea afya yako isiharibike na mwili wako kuwa katika afya njema.

Friday, July 11, 2014
WANAFUNZI WAMALIZA MAFUNZO YAO YA AEROBIC DANCE UDSM KITENGO CHA PHYSICAL EDUCATION SPORTS SCIENCES
Kama kawaida kozi hii hufanyika semista ya ya pili kwa wanafunzi wa mwaka wa pili wa kitengo husika hapa Chuo Kikuu cha Mlimani
Pindi wamalizapo mafunzo haya huwa tayari kwa kufundisha aerobic dance, na somo hili huchukua mafunzo nadharia kwa jumla ya saa 30 na kwa vitendo darasani ni saa15.amabayo huchukua miezi mitatu.
Wanafunzi wa mlimani wakiwa katika darasa Aerobic Dance
Wanafunzi wa Pess wakiwa wanaanza mazoezi ya step kwa kupasha mwili
Wanafunzi wakiwa na hamu ya kujua kufanya aerobic step wakifurahia mafunzo hayo
Wednesday, June 4, 2014
MASHINDANO YA KUMTAFUTA MR. MASCULAR MAN IN TANZANIA 2014 YAFANA SANA
SHINDANO LA KUMTAFUTA MWANA MISULI THE MOST MUSCULAR MAN IN TANZANIA
Hili likiwa ni shindano la aina yake pekee kuanzishwa hapa Tanzania na ni shindano litakaloendelezwa kila mwaka chini ya uongozi wa mkurugenzi wa Tanza-Ned Fitness studio Mr. Mohamed Ally ambaye ndiye mwenye mamlaka nayo yaani( Hatimiliki).
Nikizungumzia hivi nina maana shindano hili halihusiani na yale ya Mr. Tanzania kama yaliyopita miaka ya nyuma.
Hivyo vijana mjitayarishe kwa mashindano yafuatayo mwakani na mshindi alikuwa kijana chipukizi Mohamedali ambaye anatokea gym ya Tanzaned iliyopo gymkhana, aliondoka na kitita cha sh.500,000/
pamoja na kilo 5 za protein powder. na kupata udhamini wa kufanya mazoezi katika gym ya Tanzaned Fitness Studio mwaka mzima.
Washiriki wakionyesha utunishaji wao wa misuli katika six mandatories
Wanamisuli wakiwa katika free pose kupata mshindi fainali.
Tuesday, June 3, 2014
MAZOEZI NA FAIDA ZAKE BAADAE HUONEKANA
Mara nyingi mtu hufanya mazoezi kwa ajili ya afya yake, matokeo yake huwa hayaonekani kwa muda mfupi .Bali huchukua muda fulani mpaka kuona matokeo yake, na hapo ndipo unapofurahia ma kujiona kumbe nilijitahidi kufanya mazoezi.
Pindi upatapo matokeo mazuri ndipo unagundua ya kuwa mazoezi ni muhimu sana kwako, hivyo basi kusimama kwako mazoezi kunakuwa hakupo na kuendelea kufanya mazoezi bila ya kukosa.
Ukiwa unakwenda kufanya mazoezi kwenye gym yoyote ile huwa unaweza kupata ushauri wa nini cha kufanya chini ya uangalizi wa mwalimu.lakini ukiwa unafanya mazoezi peke yako mara nyingi unakata tamaa labda kwa kutojua malengo yako.
Mazoezi huwa mazuri pale upatapo mshauri au mwangalizi wako pindi unapofanya mazoezi, hii ikiwa na maana kuwa na mwalimu wa mazoezi.

Monday, May 12, 2014
UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU
Kufanya mazoezi kila siku ya maisha yako ya kila siku, hii ikiwa na maana kuwa kuna umuhimu sana kwa ajili ya afya njema na kujirefushia maisha yako.
Pia hukusaidia kukuondolea na kukukinga na maradhi madogodogo ambayo husumbua sana .
Kwa kushauri mtu uwe unafanya mazoezi kwa ajili ya kuondoa kaloriz ambazo zimezidi mwilini kwako ili uwe na afya njem.
Thursday, April 17, 2014
WANAFUNZI WAALIMU WA AEROBIC DANCE WAANZA KOZI YA WAALIMU WA AEROBICS CHUO KIKUU MLIMANI
Chuo kikuu cha Mlimani ambacho hutoa mafunzo kwa waalimu wa mazoezi ya viungo chini ya idara ya Elimu Kuu kitengo cha michezo na sayansi (Physical Education Sport Sciences)
kwa wanafunzi ambao wamechagua kozi hiyo ya Aerobics instructor ambayo ikiwa ni mojawapo ya kozi zinazotolewa UDSM.
kwa wanafunzi ambao wamechagua kozi hiyo ya Aerobics instructor ambayo ikiwa ni mojawapo ya kozi zinazotolewa UDSM.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani ambao wanachukua kozi ya
Aerobics dance wakiwa na waalimu wao.
Wednesday, April 2, 2014
MAFUTA YATOKANAYO NA MIZIZI,MAUA NA MATUNDA YANAVYOSAIDIA KUONDOA TUMBO KWA KUPAKAA.
SLIM & SASSY Essential Oil Suplment
Mara nyingi watu hufanya mazoezi na kupungua,lakini huchukua muda mrefu kupunguza mafuta ambayo yamezidi mwilini hata baada ya muda fulani ukiacha kufanya mazoezi yale mafuta hurejea kwa nguvu zaidi na kuongezeka mara dufu.Lakini kwa sasa kuna suluhisho la tatizo kama hilo limepatikana hii ikiwa ni aina ya mafuta ya Slim Sassy ambayo unapakaa zile sehemu korofi tu na kufanya mazoezi yako kama kawaida na kupunguaza mafuta kama vile tumbo mikono na kadhalika .
Mafuta haya hayana madhara ya aina yoyote kwa vile imetokana na mimea.
mafuta haya yaligunduliwa na mtaalam Daktari David Hill kutoka Amerika na ambaye pia yeye ni mwenyekiti wa hiyo kampuni ya doTERRA.Kuna mafuta yanayotibu maradhi mbalimbali pia ikiwemo pumu,kisukari mumivu yasiyoisha ya mwilli na kadhalika.
ukita kufanya oda na maelezo wasiliana kwenye email omarysway@gmail.com
Aina ya mafuta ya Slim Sassy ambayo husaidia kuondoa mafuta kwa kupakaa
Tuesday, February 4, 2014
MWANA MAZOEZI ALIYEPATA FAIDA KUBWA KUFANYA MAZOEZI YA AEROBICS
Mwana mazoezi Charles Mapima amefaidika sana katika kufanya mazoezi ya aerobics ambayo yamemsaidia kiasi kikubwa katika maisha yake ya kila siku.
Akitoa ushuhuda kwangu mie kuwa alikuwa akisumbuliwa na presha pamoja na maimivu makali ambayo alikuwa anapata wakati wa kutembea na hata kukaa kwenye nyonga.
Lakini alipofanya mazoezi ya aerobics takriban miezi sita iliyopita yale maumivu ya nyonga yamekwisha bila ya kutumia dawa yoyote ile.Hata lile tatizo la presha limekwisha kabisa alipokwenda kumuona daktari wake kupima,amekuwa ni mtu wa furaha na afya bora kutokana na umri wake mkubwa.
Mwana mazoezi mzee Charles Mapima akiwa katika mazoezi ya step aerobics
akiwa kalowa jasho tishet yake hii husaidia kukata kalori zilizozidi mwilini.
Monday, January 27, 2014
NAMNA YA KUTUMIA JUISI YA MBOGA MBOGA NA MATUNDA ZINASAIDIA KUPUNGUA UZITO WA MWILI
Leo nachukua nafasi hii kukujulisheni ni namna gani Juisi hii husaidia kupunguza uzito wa mwili hii ikiwa na kuzingatia mazoezi japo mara tatu kwa wiki..
Kuna watu wengine wanafikiria au wanaelewa kuwa unaweza kupungua kwa kutumia hii juisi bila ya kufanya mazoezi kwa kutegemea kuacha mazoezi, la hasha mazoezi ni muhimu sana, na wengine walidiriki kuniandikia aina nyingine ya juisi ambayo wao wametoa kwenye mitandao mingine, hao pia nakubaliana nao lakini wajue kuna aina nyingi za juisi ambazo husaidia kupunguza uzito, ninapoandika huwa nina uhakia wa ninachofanya.
Hebu jaribu kufuatilia jinsi ya kutengeneza hiyo juisi kwa kutumia juice maker machine ambayo ni mahsusi kwa ajili hiyo wala sio hizi blender za kawaida, kwani mchanganyiko huo wa juice hukupa virutubisho vyote na kujisikia umepata mlo.Natosha.nashukurani zangu za thati kwa wale walioniandikia na kwa wale waliojaribu kutumia na kupata matokeo mazuri.

Subscribe to:
Posts (Atom)