Mara nyingi mtu hufanya mazoezi kwa ajili ya afya yake, matokeo yake huwa hayaonekani kwa muda mfupi .Bali huchukua muda fulani mpaka kuona matokeo yake, na hapo ndipo unapofurahia ma kujiona kumbe nilijitahidi kufanya mazoezi.
Pindi upatapo matokeo mazuri ndipo unagundua ya kuwa mazoezi ni muhimu sana kwako, hivyo basi kusimama kwako mazoezi kunakuwa hakupo na kuendelea kufanya mazoezi bila ya kukosa.
Ukiwa unakwenda kufanya mazoezi kwenye gym yoyote ile huwa unaweza kupata ushauri wa nini cha kufanya chini ya uangalizi wa mwalimu.lakini ukiwa unafanya mazoezi peke yako mara nyingi unakata tamaa labda kwa kutojua malengo yako.
Mazoezi huwa mazuri pale upatapo mshauri au mwangalizi wako pindi unapofanya mazoezi, hii ikiwa na maana kuwa na mwalimu wa mazoezi.
No comments:
Post a Comment