Tuesday, August 26, 2014
MAMBO AMBAYO MTUNISHA MISULI(BODY BUILDING) ANAPASWA KUFANYA NA KUONEKANA AMEJENGA VEMA
Mambo muhimu ambayo anapaswa kuyajua mtunisha misuli(bodybuilding)
(a)Awe na malengo wakati wa kufanya mazoezi ya kujenga misuli na ajielewe,
(b)Anatakiwa ajue vyakula vya kula wakati akifanya mazoezi haya ya kujenga misuli kwa sababu mwili haujengeki kwa kubeba uzito tu bali ikiwa inakwenda sambamba na lishe bora na iwe ya kutosha sio kujinyima.
(c)Awe anapata vyakula vya aina ya protin kwa wingi ili kusaidia kujenga na kukuza misuli pamoja na chakula cha wanga kwa kuleta nguvu mwilini.Hii ikiwa na nyama kwa wingi pamoja na mayai yasiyopungua 9 wakati wa chai ya asubuhi.
(d) Usikae mpaka ukasikia tumbo halina kitu unatakiwa ujisikie wakati wote una chakula tumboni kwani wakati wote mwili wako unahitaji chakula kwa ajili ya kujenga misuli imara na mikubwa.
(e)Kufanya mzoezi kwa kuongeza uzito unaonyanyua kila seti.
(f) Pata muda wa kutosha kupumzika wakati umalizapo mazoezi ili kuupa mwili nafasi ya kujenga misuli.
Haya ndio matokeo ya mazoezi ya kujenga misuli pamoja na lishe bora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment