Gym maarufu ambayo inaongoza kwa kutoa mafunzo ya waalimu wa aerobics hapa Tanzania na ambayo ina mwalimu aliyebobea katika mazoezi haya hapa Tanzania mwalimu O.Swai inafana kila kukicha kwenye mazoezi haya.Hivyo akitoa wito kwa wanamazoezi kujiunga katika gym hiyo iliyopo chuo kikuu na kupata mazoezi yaliyokwenda shule kama usemi wetu usemavyo Elimu Kwanza.
Mwalimu O.Swai akiwa kwenye darasa lake la step aerobics
chuo kikuu cha mlimani
Wadau wa aeobics wakifuatilia bila kukosea mazoezi ya step
Likiwa ni darasa lililoja wadau wa mataifa mbali mbali
wakifuatilia kwa makini mazoezi.
Kushoto mwanzo ni mdau wa mazoezi Isabellah akifuatilia kwa makini
Mwalimu Swai akiwa kwenye mwendo mdundo katika mazoezi.
Tuesday, April 30, 2013
Wednesday, April 24, 2013
CLUB YA MAZOEZI YA AEROBICS YA VETA (DSMRVTSC) SASA YAVUMA
Ni kwa nadra sana kusikia wafanyakazi kuamua kufanya mazoezi na kwa moyo kama club ya VETA ambayo inavuma kwa sasa kwa ajili ya kufanya mazoezi, hii ni kwa sababu hata viongozi wao wanapenda mazoezi na kuwathamini wafanya kazi wenzao.
Klabu hii hufanya mazoezi mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu,Jumatano na Ijumaa wakifundishwa na mwalimu O.Swai akishirikiana na msaidizi wake mwalimu Sukamba.
Mwalimu Sukamba akiwa kwenye darasa lake la aerobics.
Wanawake wafanyakazi wa veta pia wanashiriki ipasavyo
Wafanyakazi wa veta wakiwa na kiongozi wao baser wa chiuo
aliyevaa tishet njano msitari wa kwanza.
Wafanyakazi wengi hufurahia mazoezi na kupata matokeo
mazuri na kuwa na afya njema.
Tuesday, April 23, 2013
MWALIMU WA AEROBICS ABDALA HERRI ANAVYOWIKA ABUDHABI KATIKA KUTOA AINA MBALI MBALI YA MAZOEZI YA VIUNGO
Mwalimu Abdala Herri ni kijana aliyebobea sana katika mazoezi haya ya aerobics, hata katika mazoezi ya spin yaani kuendesha darasa la baskeli maalum kwa mazoezi ya mwili yaitwayo spin bike.
Siyo hayo tu pia huendesha darasa la NRG ambalo unatumia barbell na uzito kwa ajili ya kuondoa manyama uzembe.
Pia hutoa ushauri kwa wateja wake ambao wana matatizo mbali mbali ya afya zao.
Hivi sasa Abdala yukoAbudhabi akifundisha kwenye Gym ya jeshi la huko na anatarajia kufungua gym hapa Tanzania na huko Mombasa Kenya.
Mwalimu Abdala yuko mbele kavaa tisheti nyekundu akiwa anafundisha darasa la spin
Hili ni darasa la NRG ambalo Abdala anafanyisha mazoezi yake ya mapaja.
(squat)kwa ajili ya kujenga misuli wa mbele ya paja
Abdala Herri akionyesha mazoezi kwa ajili ya kujenga misuli ya mgongo
Zoezi likiwa limepamba moto yakiongozwa na mwalimu Abdala. Herri.
Friday, April 12, 2013
KOZI YA AEROBICS INAYOFANYIKA CHUO KIKUU MLIMANI YAFANA SANA MWAKA HUU 2013
Katika kitengo cha Physical Education and Sport Science(PESS) Ambayo iko chini ya Shule Kuu ya Elimu hapa Chuo Kikuu Mlimani(School of Educatio) hutoa mafunzo maalum ya aina yote ya michezo kwa waalimu ikiwemo mafunzo ya mpira wa miguu, kuogelea,long tenise, basketball handball netball, badminto, mpira wa meza(table tenis), riadha, american foot ball na pia hutoa mafunzo ya Aerobics kwa waalimu wa mazoezi ya viungo.
Kozi ya Aerobics mwaka huu imependwa sana na kushiriki wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa hapa nchini Tanzania, China na nchi za Scandnavia pia wameshiriki kozi hii ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae pindi wamalizapo chuo kwa kupata ajira au kufundisha mashuleni.
Kwenye kozi hii akiongozwa na mkuu wa kitengo cha Michezo na Sayansi Dr.S. Maro akisaidiana na Mwalimu wa Fitness O.Swai kimekwisha toa mafunzo kwa wanafunzi wasiopungua 70 ambao walimaliza hapa mafunzo yao ikiwa ni pamoja na Aerobics and Fitness.
Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wake kutoka China ambao wako na furaha.
Mwalimu mwanafunzi akijaribu kutoa mazoezi aliyofundishwa katika hio somo.
Mwanafunzi Safia kutoka China akiongoza darasa mazoezi ya Aerobics.
Hapa Safia akionyesha ujasiri wa kufundisha darasa la mazoezi ya viungo (aerobics)
Hili ni darasa mchanganyiko wa wanataaluma wa mazoezi ya viungo wakifuatilia kwa makini.
Kila mwanafunzi hufurahia wanavyopata mavunzo kutoka kwa mwalimu O.Swai na kumuelewa vema
Subscribe to:
Posts (Atom)