Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, May 23, 2012

JINSI UNAVYOTAKIWA KUFANYA MAZOEZI NA MUDA WAKE

Kuna baaadhi ya watu ambao wanafanya mazoezi kwa kupita kiasi,kwa maana hiyo hufikiria kufanya mazoezi kwa muda unaozidi saa moja ndio utakuwa unapunguza uzito na wengine hudiriki kufanya mara saba kwa wiki tena sio chini ya saa mbili.

Hii  siyo sahihi kwa sababu mwili wa binadamu unahitaji muda wa kupumzika na kuupa nafasi ya kujenga misuli ya mwili kwa mpangilio ulosahihi kutokana na maumbile yake.

Muda maalum unaotakiwa kufanya mazoezi usizidi saa moja na ikwa imepungua ni dakika 30 kwa siku mara tano kwa wiki,hii inasaidia kupunguza kaloriz ambazo hazihitajiki  mwilini.Kwani binaadamu anatakiwa awe anapata kaloriz 1500 kwa siku kutokana na chakula anachokula hii humsaidi awe na afya njema na kutokuwa namaradhi yanayosababishwa na mafuta  kwa wingi mwilini.

Madhara wanayopata wale wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu bila ya kupumzika huwa yanawafanya kuonekana wamechoka muda wote huonekana kuzeeka hararaka haswa sehemu ya uso wake.
Epuka kuzidisha mazoezi na pata muda wa kuupumzisha mwili ili kujenga seli mpya za mwili.
















Katika picha inaonyesha baadhi ya mazoezi ya 
viungo  namna unavyoanza na kumalizia.
Je wewe waweza haya mazoezi.JARIBU LEO;

Monday, May 14, 2012

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUWA NAYO KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU

Mambo matatu  unayopaswa uyazingatie katika maisha yako ya kila siku ili kuepukana na uzito  uliokithiri.

1. USIWE UNALALA  WAKATI UNAWEZA KUKAA KITAKO

2.USIKAE WAKATI UNAWEZA KUSIMAMA.


3.USISIMAME SEHEMU MOJA WAKATI UNAWEZA KUSOGEA

Hii nikiwa na maana unapokuwa kazini uwe unazingatia hayo mambo matatu,utakuwa umeokoa maisha yako katika ogezeko la uzito wa mwili usiohitajika na kuwa na afya njema wakati wote wa maisha yako.
Mara nyigi ukiwa ofisini jitahidi  kufanya mambo mengi bila ya kutegemea msaada kwa msaidizi, kama vile kunyanyuka na kwenda kuchukua faili kwenye shelfu, kunyanyua kitu au kuzungumza na simu kwa muda mrefu umekaa kwenye kwenye kiti jitahidi uwe  unasimama na kutembea huku unazungumza..
Pia wakati wa kwenda kupata chakula cha mchana jitahidi uende mwendo kidogo ili uupe mwili mazoezi ya kutembea , hii itakusaidia katika usagaji wa chakula kwa wepesi zaidi na kujisikia mchangamfu wakati wote wa maisha yako.


Wednesday, May 9, 2012

SULEIMAN KIULA MWANA MAZOEZI WA WIKI















Katika picha mwisho kulia mwana mazoezi aliyevaa tisheti
nyekundu na bukta ya rangi nyeupe yenye mistari pembeni
ndiye Mwana Mazoezi wa wiki anaitwa Suleiman Kiula
ambaye anafanya kazi SUMAJKT  na Meneja wa fedha.


















 Suleiman akionekana na wanamazoezi wenzake
katika darasa la Aerobics yuko mwisho kulia.