Wadau wa mazoezi ya viungo leo ngoja niwakumbushe umuhimu wa kufanya mazoezi ya kupasha mwili moto(warm up) kabla ya kuanza zoezi lolote.
Umuhimu wa kufanya hilo zoezi la kupasha mwili moto(WARM UP) ni kuutayarisha mwili kwa mazoezi. Pia husaidia kuongeza usambazaji wa damu katika viungo pamoja na misuli ya mwili pamoja na kuupa mwii joto kwa matayarisho ya mazoezi utakayofanya ambayo husaidia kulainisha viungo vyako vya mwili, hata hivyo husaidia kulainisha mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kusaidia kulinda misuli isipate madhara pamoja na mifupa.
Vilevile kupasha mwili moto(warm up) husaidia kuongezeka upatikainaji wa hewa ya oksijen kwenye misuli na mishipa ya fahamu kwa binaadamu anayefanya mazoezi.
Hivyo mdaua wa mazoezi huo ndio umuhimu wa kupasha mwili moto( warm up) kabla ya kufanya mazoezi.
No comments:
Post a Comment