KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI GYM NYINGI HUWA ZIMEPWAYA WANACHAMA KUTOKANA NA FUNGA.
WANACHAMA AMBAO HUENDA KUFANYA MAZOEZI IWE KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO AU KUJENGA MWILI MARA NYINGI HUPUMZIKA MAZOEZI. HII NI KUTOKANA NA UCHOVU ANAOUPATA KUTOKANA NA KUFUNGA, INABIDI AFANYE NINI ILI UZITO USIZIDI.
HASWA NIKIZUNGUMZIA KWA WALE KINA MAMA AMBAO MWEZI HUU HAWANA
MUDA WA KUFANYA MAZOEZI KUTOKANA NA MAJUKUMU YAO KUWAZIDI.
JAMBO LA MUHIMU NI KUJITAHIDI KULA CHAKULA AMBACHO HAKINA MAFUTA MENGI PIA AWE NA MUDA WA KUTEMBEA KWA MUDA WA DAKIKA 15 HIVI ITASAIDIA KUKUFANYA UWE MCHANGAMFU NA KUSAIDIA MSAGO WA CHAKULA.
AU KWA WALE AMBAO WANASWALI SALA YA TARAWEHE HUWA WANAFAIDIKA ZAIDI MAANA TARAWEHE NI KAMA ZOEZI AMBALO HUDUMU KWA MUDA WA DAKIKA45 MPAKA SAA MOJA KWA WALE WAUMINI WA DINI YA KIISLAM.
NA PIA KULA MATUNDA KWA WINGI WAKATI WA DAKU PAMOJA NA MBOGA ZA MAJANI.KWA WALE WANOPATA GESI WATUMIE JUICE YA MATANGO KAMA GLASI MOJA NDOGO.
NAWATAKIA MFUNGO MWEMA*RAMADHAN KARIM*
No comments:
Post a Comment