Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, February 27, 2015

AINA YA VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA ILI KUEPUKA MARADHI YA KISUKARI


Pamoja na kufanya mazoezi ili kuepukana na maradhi ya kisukari, pia inahitajika kujua aina gani ya vyakula unavyotakiwa kula.
Hii imesisizwa sana  vyakula ambavyo havikobolewi ikiwemo dona badala ya sembe na aina nyingine ni kama ulezi, mtama na matunda.
Halikadhalika kuepukana na vinywaji ambavyo huwekwa sukari nyingi kama vile soda,pombe na juisi kwa sababu vinywaji hivi huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu isivyo kawaida.
Hivyo basi vyakula ambavyo havikobolewi huchukua muda kusagika na kwenda kwenye utumbo mwembamba hivyo husagwaswagwa vyema na kuenda kwenye matumizi ya mwili.
Halikadhalika yale makapi ambayo hutokana na hivyo vyakula husaidia kuzuia kupata kansa ya utumbo.


                        Namna moja ya zoezi la push up ili kuepuka maradhi ya kisukari


                      Step Aerobics kwa ajili ya kuweka mwili afya na kuepuka maradhi.

No comments: