Friday, February 27, 2015
AINA YA VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA ILI KUEPUKA MARADHI YA KISUKARI
Pamoja na kufanya mazoezi ili kuepukana na maradhi ya kisukari, pia inahitajika kujua aina gani ya vyakula unavyotakiwa kula.
Hii imesisizwa sana vyakula ambavyo havikobolewi ikiwemo dona badala ya sembe na aina nyingine ni kama ulezi, mtama na matunda.
Halikadhalika kuepukana na vinywaji ambavyo huwekwa sukari nyingi kama vile soda,pombe na juisi kwa sababu vinywaji hivi huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu isivyo kawaida.
Hivyo basi vyakula ambavyo havikobolewi huchukua muda kusagika na kwenda kwenye utumbo mwembamba hivyo husagwaswagwa vyema na kuenda kwenye matumizi ya mwili.
Halikadhalika yale makapi ambayo hutokana na hivyo vyakula husaidia kuzuia kupata kansa ya utumbo.
Namna moja ya zoezi la push up ili kuepuka maradhi ya kisukari
Step Aerobics kwa ajili ya kuweka mwili afya na kuepuka maradhi.
Monday, February 16, 2015
UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI ILI KUEPUKA MARADHI YA KISUKARI
Mara nyingi sisi binaadamu hatufanyi kitu bali kwa manufaa fulani tena pale unapozidiwa na kushuriwa na daktari ndipo tunazinduka.
Mazoezi ni jambo la muhimu sana kwa binaadamu yeyote yule kufanya ili kuepukana na maradhi ambayo yanasumbua binaadamu.
Leo nizungumzie maradhi ya kisukari kwa ufupi ni namna gani yanakupata na jinsi ya kuepuka.
Kuna umuhimu wa kila mtu kufanya mazoezi yasiyopungua muda wa dakika 30 hadi saa moja kila siku katika maisha yake ili kuepuka maradhi haya ya kisukari, hii inasaidia mwili wote ikiwa pamoja na misuli kufanya mazoezi na kutokwa na jasho ambayo husaidia hutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.Hii ni kwa sababu mwili wa binadamu huzalisha sukari kila siku na inatakiwa ile sukari itumike ipasavyo bila kuwa na kusanyiko mwingi wa sukari mwilini.
Mzoezi ya rowwing namna unavyoanza
Mazoezi ya rowwinng unapomalizia hufanya kwa dk 25 tu.
Subscribe to:
Posts (Atom)