Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, June 4, 2014

MASHINDANO YA KUMTAFUTA MR. MASCULAR MAN IN TANZANIA 2014 YAFANA SANA



SHINDANO LA KUMTAFUTA MWANA MISULI  THE MOST MUSCULAR MAN IN TANZANIA
                                                                                   
Hili likiwa ni shindano la aina yake pekee kuanzishwa hapa Tanzania na ni shindano  litakaloendelezwa kila mwaka chini ya uongozi wa mkurugenzi wa Tanza-Ned Fitness studio Mr. Mohamed Ally ambaye ndiye mwenye mamlaka nayo yaani( Hatimiliki).
Nikizungumzia hivi nina maana shindano hili halihusiani na yale ya Mr. Tanzania kama yaliyopita miaka ya nyuma.
Hivyo  vijana mjitayarishe kwa mashindano yafuatayo mwakani na mshindi alikuwa kijana chipukizi Mohamedali ambaye anatokea gym ya Tanzaned iliyopo gymkhana, aliondoka na kitita cha sh.500,000/
pamoja na kilo 5 za protein powder. na kupata udhamini wa kufanya mazoezi katika gym ya Tanzaned Fitness Studio mwaka mzima.
                                                                               


                 Washiriki wakionyesha utunishaji wao wa misuli katika six mandatories




                              Wanamisuli wakiwa katika free pose kupata mshindi fainali.




Tuesday, June 3, 2014

MAZOEZI NA FAIDA ZAKE BAADAE HUONEKANA

Mara nyingi mtu hufanya mazoezi kwa ajili ya afya yake, matokeo yake huwa  hayaonekani kwa muda mfupi .Bali huchukua muda fulani mpaka kuona matokeo yake, na hapo ndipo unapofurahia ma kujiona kumbe nilijitahidi kufanya mazoezi.
Pindi upatapo matokeo mazuri ndipo unagundua ya kuwa mazoezi ni muhimu sana kwako, hivyo basi kusimama kwako mazoezi kunakuwa hakupo na kuendelea kufanya mazoezi bila ya kukosa.
Ukiwa unakwenda kufanya mazoezi kwenye gym yoyote ile huwa unaweza kupata ushauri wa nini cha kufanya chini ya uangalizi wa mwalimu.lakini ukiwa unafanya mazoezi peke yako mara nyingi unakata tamaa labda kwa kutojua malengo yako.
Mazoezi huwa mazuri pale upatapo mshauri au mwangalizi wako pindi unapofanya mazoezi, hii ikiwa na maana kuwa na mwalimu wa mazoezi.