Friday, February 22, 2013
NAMNA YA KULA MLO WAKATI UNAPOTAKA KUPUNGUA UZITO ULIOZIDI NA MAZOEZI
Kupunguza uzito ulokithiri huchukua muda mpaka kupata matokeo yake,ukiwa unazingatia kufanya mazoezi kama vile kutembea, kuendesha baiskeli na kufanya mazoezi ya aerobics ambayo hukupa matokeo haraka zaidi kuliko mazoezi yoyote yale.
Nikizungumzia mazoezi ya aerobics huwa nina maana kila sehemu ya kiungo cha mwili wako hufanyishwa mazoezi.
Ukizingatia kuanzia mwanzo wa zoezi hilo unaanza na kupasha mwili moto halafu ndio unaendelea na mazoezi mengine huku ukifuatilia ikienda sambamba na muziki maalumu kwa mazoezi tofauti.
Hii hukupa wewe mwanamazoezi kufanya na kufurahia,baada ya hapo ikifuatiwa na mazoezi kuunnyoosha mwili na kuondoa uchovu kwa kipindi chote cha mazoezi.
Na kumalizia na zoezi la kuondoa tumbo.
Lakini mazoezi yanatakiwa uende sambamba na kupunguza chakula kwa mfano ulikuwa unakula sahani iliyojaa unakula nusu yake. Hata hivyo uwe umepata kifungua kinywa cha kutosha itakisaidia kutokula hovyo hovyo.Mchana utakula kiasi tu ukipata matunda kwa wingi.
Wakati wa usiku ujitahidi upate chakula chepesi kwani maranyingi chakula cha jioni huongeza uzito kwa sababu ukishakula unaenda kulala na msago wa chakula huwa umesimama hadi kesho yake saa 12 asubuhi.
Pia jitahidi kupunguza mafuta kwenye chakula hata sukari iwe kiasi na chumvi pia itakusaidia kupunguza uzito.
Aina ya mazoezi ambayo unatakiwa kufanya kama picha inavyoonyesha
Kuna aina nyingi ya mazoezi ambayo husaidia kukupunguza kwa kutumia mashine
Thursday, February 7, 2013
AINA MBALI MBALI YA MAZEOZI YA VIUNGO(AEROBICS)
Katika kufanya mazoezi ya viungo unaweza pia kufanya mazoezi kwa kucheza utakavyo ili mradi unaendana na midundo.
Hivi sasa waalimu wa mazoezi haya ya viungo wamegundua namna ya kuwavutia wadau wa mazoezi haya kwa kuwapa mtindo na aina ya muziki
Hapa ni namna ya kuanza zoezi la kick box
Namna ya kutupa ngumi pamoja kufuatilia mdundo
Jinsi ya kutumia mateke au kutumia goti uku ukienda na muziki
Mwalimu Swai akitoa mafunzo namnkukunja na kutupa ngumi
Subscribe to:
Posts (Atom)