Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, September 28, 2012

AINA YA VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA ILI KUPUNGUZA TUMBO KWA KUFANYA ZOEZI

Mara nyigi binadamu huwezi pungua mwili bila ya kufanya mazoezi ikiwa imeambatana na kupunguza mlo unaokula.

Aina ya vyakula ambavyo  unatakiwa kula ni kujaribu kupata chakula ambacho hakina mafuta mengi,pia kupunguza ulaji wa sukari nyingi na hata chimvi ujaribu kupunguza katika maisha yako ya kila siku, hali kadhalika  kupunguza vyakula vya wanga.
Jambo lingine ni kufanya mazoezi ya tumbo kila siku uamkapo asubuhi na jioni ili uondoe manyama uzembe.


















Mazoezi ya tumbo namna ya unvyoanza ukiwa umekaa
kitako na kukunja miguuyako kama  picha inavyoonyesha


















Hapa ni namna ya kumalizia zoezi la tumbo kwa
kunyoosha na kukunja tena kama mwazo mara 50






Monday, September 17, 2012

AINA YA MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO (KITAMBI)

Mara nyingi sana katika maisha watu wengi hupata tatizo la kuwa na tumbo kubwa na baadae humletea madhara. Ili kuepuka tatizo hili ni kuamua kufanya mazoezi  kupunguza  ya mafuta katika chakula na kufanya mazoezi ya tumbo hii ndio njia pekee hakuna njia mbadala.

                                                           
                                        Zoezi hili ni kufanya kwa kutumia mashine(abs board)





Hapo ni zoezi ambalo utumia mpira maalum. uanzapo;

                                            Zoezi  la mpira maalum umaliziapo kwa kunyaua juu.




                                         Hapa ni mazoezi ya tumbo kwa kutumia mpira maalum




                                          Kwa kutumia bench la zoezi la tumbo unavyoanza

                                          Namna unvyomalizia  zoezi kwa kunyanyuka.




                                          Zoezi la tumbo kwa kutumia hypic chair unavyoanza.

                                         Zoezi la tumbo unavyomalizia kwa kutumia hypic chair





                                         Zoezi la aina nyingine kwa kutumia mpira wa zoezi hilo

Monday, September 10, 2012

MAZOEZI HAYANA UMRI WA KUYAFANYA HATA WAZEE WANAHITAJI MAZOEZI NI MUHIMU

Watu wengi hudhani mazoezi ni kwa ajili ya mtu au watu wenye umri fulani tu , hiyo hapana pia ni fikra potofu kwa wale ambao hawajui au hawajawahi kufanya mazoezi kwenye maisha yao yote.

Mazoezi ni muhimu sana haswa pale umri unapoenda kwa sababu utakuwa hufanyi tena kazi au kuwa na pilika pilika kama ulipokuwa kijana.

Mazoezi madogodogo husaidia watu wenye umri mkubwa kujisikia kijana kila siku aamkapo na pia kutosumbuliwa na mardhi ya mara kwa mara.

Pia mazoezi husaidia watu wenye umri mkubwa kuwa na nguvu hata kumlinda kuwa na kumbukumbu zake bila kusahau mambo.

 Mzee Alhaj Juma Mtale akiwa katika mazoezi 
                                           ya kunyoosha mgongo ni mzee mwenye umri zaidi ya                       
                                            miaka70 pia hujisiki poa akifanya mazoezi yake.


                                                                                                                                                                        
















Mzee Alhaj Juma Mtale akiwa kwenye
aina nyingine ya mashine cross training










y

Monday, September 3, 2012

MAZOEZI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUTUMIA SPIN BIKE

Mazoezi ya spin bike yamekuwa na msisimko mkubwa sana hapa Dar es salaam, imekuwa hivyo kutokana na kuwa na wapenzi wengi wa mazoezi hayoambayo yanasaidia sana katika kupunguza uzito kwa muda mfupi na kukuweka kuwa na pumzi na kuwa na afya bora.
Mazoezi hayo yametokea kuwa na umaarufu lakini kukiwa na waalimu wachache sana ambao wanafundisha zoezi hilo.
Hivyo hima waalimu wajitokeze katika kujifunza namna yakuendesha zoezi hilo ambalo linaongozwa kwa kutumia muziki maalum kwa kweli ni burudani tosha.

















Katika picha hapo juu ni wadau wa mazoezi ya spin bike.
















Hapa ni wadau wa mazoezi ya spin bike waliobobea katika zoezi

















Amakweli zoezi la spin bike limetokea kupendwa sana hapa Bongo