Ni kawaida yetu kufanya mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ulokithiri,hii ikiwa ni lengo la muda mrefu mpaka kufikia uzito ambao unakubalika.
Haya matatizo ya kuongezeka uzito huwa yanajitokeza pindi unapokula bila ya mpangilio wowote ule,ikiwa ni pamoja ya kula bila mpangilio na bila kujua chakula cha aina gani na wakati gani.
Leo niwakumbushe kwamba unaweza kufanya mazoezi madogodogo kama vile kujihusisha na shughuli ndogondogo hapo nyumbani kwako,ikiwa ni kufanya zoezi la kufanya usafi kama kufyeka bustni na kupalilia maua au kukata majani kwa kutumia mashine ya kukatia huku ukitembea. Haya ni mazoezi tosha kwa wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda gym.Usisahau kupunguza mlo na kupata mlo mwepesi wakati wa mlo wa usiku.
No comments:
Post a Comment