Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, August 18, 2012

JINSI YA KUCHUNGA KUONGEZEKA UZITO WA MWILI ULOKITHIRI BILA YA KUFANYA MAZOEZI.

Ni kawaida yetu kufanya mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ulokithiri,hii ikiwa ni lengo la muda mrefu mpaka kufikia uzito ambao unakubalika.
Haya matatizo ya kuongezeka uzito huwa yanajitokeza pindi unapokula bila ya mpangilio wowote ule,ikiwa ni pamoja ya kula bila mpangilio na bila kujua chakula cha aina gani na wakati gani.
Leo niwakumbushe  kwamba unaweza kufanya mazoezi madogodogo kama vile kujihusisha na shughuli ndogondogo hapo nyumbani kwako,ikiwa ni kufanya zoezi la kufanya usafi kama kufyeka bustni na kupalilia maua au kukata majani kwa kutumia mashine ya kukatia huku ukitembea. Haya ni mazoezi tosha kwa wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda gym.Usisahau kupunguza mlo na kupata mlo mwepesi wakati wa mlo wa usiku.

Wednesday, August 8, 2012

AINA YA MAZOEZI YA SURCKET TRAINING YANAVYOTAKIWA KUFANYA



Katika picha zinzonyesha namna ya kufanya zoezi la surcket training huwa unafanya mazoezi aina mbalimbali kwa muda wa takribani dakika 40 . Ikiwa kila zoezi unachukua dakika  nne na kuhamia zoezi lingine na kuanza tena.Zoezi hili unaweza kukata kalori 860.














Hapa juu ni mazoezi ya kukimbia kwenye mashine ya
treadmill na total body power mshine



















Hapa ni zoezi la step aerobics ambalo huwa
linakwenda sambamba na mazoezi mengine




















Katika picha hapo juu ni zoezi tofauti, juu kabisa
ni zoezi linalosaidia kukukuza sehemu ya misuli ya nyuma
ya mikono(tricept muscles).


















Hapa ni zoezi la kukuza au kuondoa manyama uzembe
upande wa mgongo na upande(obliq muscle)
Zoezi hili hutegemea uzito unaoweka yaani uzito mdogo
kwa ajili ya kuondoa mafuta.
Na uzito mkubwa kwa ajili ya kujenga sehemu ya mgongo
(lat pull down)