Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, June 20, 2012

TOFAUTI YA MAZOEZI YA AQUA AEROBICS NA KUOGELEA






Watu wengi wanashindwa kutofautisha  kati ya Aqua Aerobics na  kuogelea.
Kuna tofauti kubwa kati ya haya mazoezi mawili hata kwa kuangalia picha hapo,
kwa vile zoezi hilo hufanyika ukiwa kwenye maji.
Zoezi la aqua  unafanya kama vile zoezi la aerobics uwapo darasa la kawaida yaani
bila maji,lakini zoezi hili hukulinda kutokuumia magoti kwa urahisi.na pia mtu yeyote
anafanya hata kama hajui kuogelea,na pia umalizapo zoezi hilo ambalo linachukua
takriban ya dakika 40 tu utasikia misuli  na viungo vyako vya mwili vimepata
zoezi tosha

 Mazoezi ya kuogelea inabidi ujue namna ya kuelea kwenye maji na hii pia inahitaji
mafunzo maalum ili umudu kuogelea.Pia hilo ni zoezi la mwili ambalo linasaidia pia.






















Katika picha ya juu inaonyesha mazoezi ya Aqua aerobics darasa maalum
 katika bwawa la chuo kikuu (UDSM) N mwalimu Swai.



















Mazoezi ya kuogelea kwa kuelea juu ya maji.




Zoezi la kuogelea kama picha inavyoonyesha  hapo juu chuo kikuu (UDSM)

Friday, June 1, 2012

MAOEZI YA AQUA AEROBICS YAANZA CHUO KIKUU MLIMANI

 Mazoezi ya Aqua yakiwa yamefana sana katika bwawa la kuogelea la Chuo Kikuu ch Mlimani (UDSM).
Mazoezi haya hufanyika kila siku ya Jumatano katika bwawa hilo chini ya Mwalimu O.Swai.
 Zoezi hilo ni kwa mtu yeyote hata kama hajui kuogelea humudu kulifanya bila ya matatizo.Hivyo wadau wengine kutoka popote pale mnakaribishwa.


















 Mwalimu wa mazoezi ya Aerobics O.Swai akiwa na
wadau wa Aerobics katika bwawa la UDSM.
(aliyevaa nguo nyekundu akifundisha aqua aerobics)















Wadau wa mazoezi wakifuatilia kwa mkini zoezi hilo.
















Baada ya zoezi la kwenye maji sasa ni nje ya maji.















Wadau wakimalizia  mazoezi ya kunyoosha viungo
baada  ya  zoezi husika.