Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, February 17, 2012

KWA NINI SUKARI NI MUHIMU MWILINI MWAKO

Tukizungumzia sukari ni muhimu kwa binadamu yeyote yule nina maama sukari pia ni uhai au ni moja wapo ya kiungo kinachoupa nguvu misili yako.

Hii ni pamoja nakukupa nguvu na uhai kwenye misuli ya moyo wako.Pamoja na hayo kwa wale wanaofanya mazoezi kila siku ni muhimu kutumia sukari ya kawaida nikuwa na maana kuwa mchujo wa sukari kwenye mwili wake ni wa haraka sana na wa kuaminika kuliko wale wasiofanya mazoezi kabisa.

Sababu ni kwamba anayefanya mazoezi hutokwa na jasho na pia hutumia nguvu katika misuli yake ya mwili hivyo sukari huhitajika mara dufu ya yule asiyefanaya mazoezi ya aina yoyote ile.

Dalili unazosikia kama hauna sukari ya kutosha mwilini hujisikia kuwa na mchoko usioisha kwenye mwili hata kama utajipumzisha kwa siku kadhaa.

Halikadhalika ukiwa unafanya mazoezi utajikuta unakosa nguvu za kuendelea na mazoezi kwa muda mfupi hata wakati huo moyo unakwenda mbio na jasho kukutoka huku ukijisikia vibaya sana na mwili kukosa nguvu.mpaka upate huduma ya kwanza kwa kupatiwa glucose(sukari) ndipo unajisikia vema.

Hii ni tahadhari kwa wale wanaoanza kufanya zoezi la aina yoyote.

No comments: