NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA TUMBO
Katika picha (a)1 inaonyesha namna ya kuanza kufanya mazoezi ya tumbo na maelezo yake.
Unalala chali kuhakikisha mgongo wako umekandamiza chini kabisa na mikono yako yote miwili ikiwa nyuma ya shingo yako na viwiko vyako vikiwa umenyoosha pande zote, halafu unavuta pumzi ndani kwa kutumia pua kabla ya kunyanyuka
Picha(a)1
Katika picha (b)1 unanyanyuka juu kwa
kunyanyua sehemu ya mabega yako yote
wakati huo unahakikisha unakaza misuli
yatumbo lako pindi unapokuja juu na hapo
ndipo unatoa pumzi kwa kupitia mdomoni
mwako ukiwa una fikia juu na kurudi chini
tena nakuanza kama picha (a)1 invyoonyesha
mara kumi .
unafanya seti 5x10
Picha (b)1
Zoezi la pili la tumbo picha (a)2 inaonyesha
namna ya kuanza hilo zoezi.
Unakunja muguu yako yote miwili huku
umeweka mikono yako nyuma kwa ajili
ya kujizuia usende nyuma zaidi na kubalasi
mwili wako wakati wa zoezi lenyewe.
Picha(a)2
Halafu unanyoosha miguu yako kabla ya kufikia kunyooka
unarudia tena kukunja kama picha (a)2 inavyoonyesha.
Kwa kufanya hivyo unatakiwa ufanye mara kumi seti tano
5x10 baada ya hapo unapumzika kwa dakika moja na kurudi
tena.
Usisahau kuvuta pumzi ndani pindi ukunjuapo na kupumua nje
unyooshapo miguu yako.
Picha (b)2
No comments:
Post a Comment